Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,884
- 31,943
KIMBUNGA HIDAYA MAWINGUNI WATOTO WANACHEZA MPIRA WA MAKARATASI PEKUPEKU MTAANI
Jioni inakimbilia Maghrib na kama kungekuwa na jua mtu angeweza kuliona limebadilika rangi linaenda kuzama upande wa magharibi.
Toka asubuhi hali ni ya mawingu na baridi baada ya mvua ya usiku kucha na upepo mkali jana.
Hali hii ya leo si ya kawaida Dar es Salaam.
View: https://youtu.be/ZkTLHAj_KOw?si=4LCpDR_mR13qXwSN
Binafsi hali inanikumbusha hali kama hii Glasgow miaka mingi iliyopita.
Taa zimewashwa hata zile za mitaani saa saba mchana unadhani usiku.
Watu wanakuwa hawana raha na hawa ni wenyeji wameishi maisha hayo ya giza kuingia mchana na baridi kali toka kuzaliwa kwao.
Kwangu mgeni upweke ule wa kutoona watu nje kama kawaida inaongeza ukiwa na majonzi.
Afadhali ukiwa London au mji wowote ule lakini si Glasgow, Uskochi tangia mwanzo ni mji ambao kwa kiasi fulani umejiinamia na watu weusi wachache sana.
Nimekaa kibaraza cha Masjid Nur jirani na kwangu naangalia watoto wanacheza mpira barabarani.
Umeme hakuna toka asubuhi.
Ndani nyumbani giza tupu.
Naogopa kuwasha taa ya solar isije ikesha chaji na usiku ikawa tabu zaidi.
Majonzi.
Watoto hawa mimi nilipokuwa umri wao nacheza mpira kwenye kiwanja na nimevaa Adidas na bukta na sichezi mpira wa makaratasi kama huu wanaocheza wao.
Hapa nazungumza mwaka wa 1966 si leo 2024.
2024 watoto wanacheza mpira pekupeku tena wa makaratasi.
Nashusha pumzi.
Nimeelemewa kwa fikra.
Nimetoa simu yangu nawapiga video hawa watoto huku nikowaombea dua wasianguke kwani wanacheza mpira sehemu ya mbele ya nyumba ambayo mwenyewe kwa kutafuta usafi ameweka zege sawa na upana wa nyumba yake.
Kawatengenezea watoto kiwanja cha mpira cha zege mtaani watoto wamepate mahali pa kucheza.
Fikra imerudi kwa Hidaya.
Si hidayi kimbunga.
Hidaya alikuwa mtoto mwenzangu tunasoma darasa moja la kwanza Lutheran Primary School, Moshi baadae shule hii ikawa Stanley Primary School.
Kila siku asubuhi nakutana na Hidaya njiani tunaongozana kwenda shule pamoja.
Sisi wawili peke yetu njia nzima.
Sote tuna umri wa miaka saba.
Nikaondoka Moshi kuja Dar es Salaam niko darasa la tano.
Miaka mingi ikapita nafanya kazi Tanga na wateja wangu wasafirishaji kahawa kupitia bandari ya Tanga wako Moshi na Arusha.
Nikawa sipungui Moshi na kila nikifika Moshi nikawa wakati mwingine napita nje ya nyumbani kwa kina Hidaya lakini haikunijia fikra ya kumuuliza.
Siku moja nikiwa Moshi kwenye barza yangu ya hapo mjini ambayo wengi wa wanabarza ni wenzangu ambao tulisoma sote utotoni shule ya msingi nikamuuliza Hidaya.
''Hidaya kafariki siku hizi za karibuni alikuwa nurse Mawenzi Hospital.''
Hili ndilo jibu nililopewa.
Huwezi kuhisi ni kiasi gani moyo uliniuma kwa majonzi.
Miaka zaidi ya 40 imepita nilipokuwa na Hidaya tukienda shule pamoja.
Leo nikiwa pale kibaraza cha Masjid Nur 'mood'' yangu iko chini kwa hali ya hewa achilia mbali ile kuwa nawatazama watoto wanacheza mpira wa makaratasi pekupeku mwaka wa 2024.
Ubongo ni injini ya ajabu sana.
Uwezo wake ni mkubwa unaweza kukupeleka kwingi ukiwa hapo ulipokaa bila ya hata kunyanyua mguu.
Kulikuwa na fundi mshoni Magomeni Mtaa wa Dosi na Jaribu jina lake Hidaya.
Hidaya maana yake ni zawadi na ni jina la kike.
Fundi Hidaya alikuwa mwanamme.
Hidaya alikuwa mshoni wa nguo bingwa.
Leo kwa Fundi Hidaya ilipokuwa barza kubwa ya vijana watoto wa mjini hakuna mtu.
Ndiyo nikiwa pale nikawa nimesafiri hadi Uingereza 1990s nikarudi Dar es Salaam 1960s na Moshi nikienda shule asubuhi nimeongozana na marehemu Hidaya.
Hivi namaliza kuandika mvua imeanza kunyesha na nasikia Adhana Sala ya Isha kutoka Masjid Nur.