Heri ya mwaka mpya 2013! Nawashukuru, Nawaomba radhi!

Status
Not open for further replies.
Mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wenye changamoto nyingi, mafanikio makubwa ya kisiasa kama vile kushinda uchaguzi mdogo Arumeru na chaguzi kadhaa za Udiwani Kwa upande wa chama. Bungeni ulikuwa mwaka wenye rekodi za kujivunia ikiwemo hoja ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu iliyopelekea mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri, hoja binafsi za Mkonge, ugawaji Ardhi na utoroshwaji wa Fedha nje ya nchi. Sheria ya kulinda kazi wasanii, Sheria ya "capital gains tax", Sheria ya kulinda viwanda vya maziwa vya ndani na viwanda vya nguo na Sheria kufutwa Kwa msamaha wa VAT Kwa kampuni za madini.

Hata hivyo kuna changamoto kadhaa zimejitokeza. Muhimu kuliko yote ni kwamba Kwa njia moja ama nyingine nitakuwa nimewakera, kuwaudhi au kuwakatisha tamaa. Mimi ni binaadam, sijakamilika. Naomba radhi Kwa mapungufu yangu yote.

Mwaka 2013 ni mwaka utakaogubikwa na suala la Katiba. Kwa Mara ya kwanza tutaona rasimu ya Katiba mpya ya nchi yetu. Tutaweka nguvu na akili zetu Huko. Ajenda za Uwajibikaji, vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali za Taifa, ujenzi wa chama chetu na utalii vitakuwa sehemu ya vipaumbele.

JF nawashukuru sana Kwa kunipa fursa ya kuwasiliana na Watanzania. Mijadala yote humu ni funzo kwangu. Licha ya kutekeleza haki yangu ya kukasirika, lakini baada ya hasira huwa ni funzo kwangu. The interview was a world record, 9600 words interview is just short of a masters thesis. I humbly thank the team and especially the interviewer dada AshaDii for great job.

Muwe na mwaka mwema. Tujenge nchi yetu nzuri sana. Tanzania yenye Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji inawezekana!

Zitto

Hii inastahili hadhi ya "post of the year". Asante Zitto, heri ya mwaka mpya kwako pia na ubarikiwe mno mno.
 
Heri ya mwaka mpya kwako pia!

Tunategemea mwaka huu utaendelea kuibana serikali katika mambo ya maana na kuibua yale yaliyojificha ambayo watanzania wengi hatuyafahamu. Ni busara kuomba msamaha hasa pale unapojua/kuhisi umekosea hope watu wote wamekusamehe, ila sijui Nape kama amekusamehe

God be with u
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom