Heri ya mwaka mpya 2013! Nawashukuru, Nawaomba radhi!

Status
Not open for further replies.

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,885
Mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wenye changamoto nyingi, mafanikio makubwa ya kisiasa kama vile kushinda uchaguzi mdogo Arumeru na chaguzi kadhaa za Udiwani Kwa upande wa chama. Bungeni ulikuwa mwaka wenye rekodi za kujivunia ikiwemo hoja ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu iliyopelekea mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri, hoja binafsi za Mkonge, ugawaji Ardhi na utoroshwaji wa Fedha nje ya nchi. Sheria ya kulinda kazi wasanii, Sheria ya "capital gains tax", Sheria ya kulinda viwanda vya maziwa vya ndani na viwanda vya nguo na Sheria kufutwa Kwa msamaha wa VAT Kwa kampuni za madini.

Hata hivyo kuna changamoto kadhaa zimejitokeza. Muhimu kuliko yote ni kwamba Kwa njia moja ama nyingine nitakuwa nimewakera, kuwaudhi au kuwakatisha tamaa. Mimi ni binaadam, sijakamilika. Naomba radhi Kwa mapungufu yangu yote.

Mwaka 2013 ni mwaka utakaogubikwa na suala la Katiba. Kwa Mara ya kwanza tutaona rasimu ya Katiba mpya ya nchi yetu. Tutaweka nguvu na akili zetu Huko. Ajenda za Uwajibikaji, vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali za Taifa, ujenzi wa chama chetu na utalii vitakuwa sehemu ya vipaumbele.

JF nawashukuru sana Kwa kunipa fursa ya kuwasiliana na Watanzania. Mijadala yote humu ni funzo kwangu. Licha ya kutekeleza haki yangu ya kukasirika, lakini baada ya hasira huwa ni funzo kwangu. The interview was a world record, 9600 words interview is just short of a masters thesis. I humbly thank the team and especially the interviewer dada AshaDii for great job.

Muwe na mwaka mwema. Tujenge nchi yetu nzuri sana. Tanzania yenye Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji inawezekana!

Zitto
 
Last edited by a moderator:
Mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wenye changamoto nyingi, mafanikio makubwa ya kisiasa kama vile kushinda uchaguzi mdogo Arumeru na chaguzi kadhaa za Udiwani Kwa upande wa chama. Bungeni ulikuwa mwaka wenye rekodi za kujivunia ikiwemo hoja ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu iliyopelekea mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri, hoja binafsi za Mkonge, ugawaji Ardhi na utoroshwaji wa Fedha nje ya nchi. Sheria ya kulinda kazi wasanii, Sheria ya "capital gains tax", Sheria ya kulinda viwanda vya maziwa vya ndani na viwanda vya nguo na Sheria kufutwa Kwa msamaha wa VAT Kwa kampuni za madini.

Hata hivyo kuna changamoto kadhaa zimejitokeza. Muhimu kuliko yote ni kwamba Kwa njia moja ama nyingine nitakuwa nimewakera, kuwaudhi au kuwakatisha tamaa. Mimi ni binaadam, sijakamilika. Naomba radhi Kwa mapungufu yangu yote.

Shukran Mkuu,

Uwe na mwaka mpya mwema na wewe pia......All the best!
 
Good luck MR. ZITTO KABWE, let the past pass and remain a lesson for future takeover.

HAPPY NEW YEAR, 2013, TO ALL JF MEMBERS.
 
Asante sana nasi twakutakia heri , lakini mwaka 2013 tujenge chama chetu kwa pamoja bado tunakuhitaji.
 
Zitto

Sawa, for the sake of CHADEMA na ubinadam mm ni miongoni mwa wa kwanza kukusamehe kwa kuwa ni miongoni mwa wale tuliokwaruzana moja kwa moja kimaneno.

Nakutakia kila la heri na tuzid kujenga chama.

Haya maneno yangu ya signature huku chini nitayafuta kama si kuya edit! CHADEMA daima mbele.

Njoo tuungane kuitetea gesi Mtwara kama tulivoanzisha hii harakati kwa pamoja
 
Last edited by a moderator:
Asante mhe. Zitto, heri ya mwaka mpya kwako pia. Mungu akuzidishie busara, hekima na mafanikio mwaka 2013. Wenye nia mbaya juu yako wote washindwe kwa jina la YESU
 
Mkuu Zitto nikiwa miongoni mwa wanaJF na wanaChadema ambao walikereka na baadhi ya mambo uliyofanya ama kuhusishwa nayo, kwa tamko lako hili la kukiri udhaifu na kuomba radhi, basi nakubaliana kabisa na wewe.

Nachotarajia kutoka kwako kuanzia 2013 ni mshikamano, upendo, masikilizano na ushirikiano wa hali ya juu baina yako na wanachadema wote.

Napenda kutumia maneno ya mdau mmoja kwamba adui yetu ni CCM. Tushirikiane kumuangamiza kwa mustakabali wa Taifa letu.

Nikutakie heri ya mwaka 2013!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom