Heko mradi wa SGR Serikali ijipange kuimarisha ulinzi wa miundombinu

nyotanjema

Senior Member
Sep 24, 2011
137
35
Hongera Watanzania na serikali kwa kutumia kodi na kuwezesha mradi kuanza kufanya kazi kwa kipande cha Dar-Moro, Dar-Dodoma safari iliyoanza leo.

Napenda kuwashauri watanzania wenzangu huu mradi ni kwa kodi zetu tuwe na uchungu nao tusikubali kufumbia macho uhujumu wowote utakaopangwa maana sasa hivi mtu kupanda basi afike Dodoma au atoke Dodoma kwenda Dar itakuwa ngumu kidogo washindani wa usafirishaji wasije wakaanza uhujumu ndio maana naiomba mamlaka na kila mtanzania kuulinda kwa wivu mkubwa huu mradi.

Hongera sana watanzania na Serikali mhe Rais Mama Samia, Hongera pia huko alipo apate pumziko jema Rais JPM.
 
Sidhani kama shida ni miundombinu. Shida ni usimamiaji. Ukosefu wa maadili kazini utasababisha hata hii reli iishie kule kule mashirika mengine ya umma yalikoishia.
Hii reli iendeshwe kibiashara. Laasivyo tutavuna tena yale yale tuliyozoea kupanda
 
TRC wakianza kupokea mizigo midogo na mikubwa na wakaweka mifumo bora kabisa ya kutuma na kupokea kuliko ma bus au kama ma bus watapiga sana pesa sababu muda mfupi mzigo unapokea ila wasilete ukiritimba tu mfanyakazi badala ya kuhudumu huku ana tabasamu anakunja uso kama unampa talaka. waweke customer care bora kabisa huu ni mradi mkubwa na huduma zinatakiwa ziwe kubwa.
 
Tukupe tabasamu kama nani?Hutaki kupanda acha..sisi kazi ni ujiko...hebu kwanza nitoe buku ya soda..unataka uondoke saa ngapi?Bado Mlinzi hajakupiga mzinga hapo..: Malezi ya Ma_ CCM.
 
Naona wanataka kukosea wanaposema abiria haruhusiwi kusafiri na mzigo mkubwa. Wapokee hata mizigo mikubwa ila isafirishwe peke yake kama "left luggage" au liwepo behewa maalumu la mizigo mikubwa hoja iwe kuilipia.
 
Back
Top Bottom