PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 956
- 1,038
ROYAL TOUR: Tuzinguane kwa Hoja
Mjadala mkali unaendelea mitandaoni, maofisini na vijiweni juu ya filamu ya Royal Tour. Tumegawanyika na tunazinguana kuhusu filamu hii.
1. Wapo wanaomjadili Mama. Mhusika mkuu wa filamu hii. Alipaswa au hakupaswa?
2. Wapo wanaomjadili Peter Greenberg. Muandaaji na msimulizi wa filamu hii.
3. Wapo wanaojadili vitendo maalum katika filamu hii. Nani kamshika nani? Katembeaje? Kasema nini na kasema kwa njia ipi?
4. Wapo wanaojadili gharama. Ni ngapi? Nani kazichanga na kwa nini? Mbona nyingi?
5. Wapo wanaojadili wazo zima la kutengeneza filamu kama ni muhimu ama la!?
Tungeyajua saa ngapi haya? Tungezinguana saa ngapi? Tunasahau upesi kuwa tulikotoka hata kuzinguana hakukuruhusiwa.
Haiwezekani yule akawa sahihi na huyu akawa sahihi. Haiwezekani huyu akawa sahihi na yule akawa sahihi.
TUKUBALIANE (Kama tukipenda)
a. Royal Tour inahusu Njoo Muone kuliko Njoo Mchukue (Tourist destination).
b. Royal Tour inahusu Karibu Tupo kuliko Hakuna penginepo, Hapa ni Mtakuja tu.
c. Royal Tour ni tokeo la ndoto ya mtu. Tuiunge mkono ashidwe mwenyewe. Akishindwa, tumeshindwa. Akishinda, tumeshinda.
d. Royal Tour imefunua ukweli mwingine. Kuna watu walikuwa waigizaji maarufu wa filamu, umaarufu wa uigizaji ukawapa urais. Hapa tuna rais ambaye urais umempa uigizaji wa filamu katika SULUHU ya changamoto za nchi. Umaskini hauna baunsa!
Wanaokosoa, wanaokosolewa, wasio na upande, wote ni sehemu ya Royal Tour. Tuzinguane kwa hoja.
UTAJIRI USIOTUMIKA NI SAWA NA UMASKINI UNAOTUMIKA.