The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,047
- 1,709
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara John Heche amewataka vijana na Watanzania kwa ujumla kuiunga mkono CHADEMA katika mchakato na dhamira yake ya kuiletea nchi maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Heche ameyasema hayo hivi karibuni katika Jimbo la Mafinga Mjini, wilayani Mufindi mkoani Iringa akisisitiza kuwa chama tawala kimeshindwa kutengeneza mifumo ambayo itaweza kuwapatia vijana ajira za kudumu.
Amewataka wananchi kuilinda na kuichangia CHADEMA ili kushiriki katika mageuzi ya mfumo wa uchaguzi kupitia kampeni ya No Reforms No Election kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
"Tukienda kwenye uchaguzi tutashinda nchi hii na tutabadilisha maisha yenu. Tutajenga uchumi ambao utabadilisha maisha ya vijana kiasi kwamba hakutakuwa na kijana atakayekuwa kwenye betting (michezo ya kubahatisha), mtakuwa kwenye viwanda mkifanya kazi, mtakuwa kwenye mashamba, na siyo mashamba ya kilimo cha jembe la mkono", ameeleza Heche.