TGInnocent
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 1,088
- 578
Maprofesa wa ukweli, (achana na hao waliojichanganya kwenye siasa za TZ) huongea mambo kwa upeo wa hali ya juu sana. Big up kwa constructive comments kutokana na post hii. My opinion: Prof Shivji hapa naona kuwa ana challenge hiyo hatua ya kuwafukuza kazi hao wenye vyeti fake. Nafikiri ni jambo la kujiuliza, je kwa cheti fake alichonacho mhusika kinathibitisha kuwa na elimu ya cheti hicho hana? Mfano kijana hakufaulu darasa la saba, akatafuta kurudia darasa kwa jina lingine halafu akaendelea kufanya vizuri mpaka akafaulu, yamkini mpaka kufanikiwa kupata professional recognitions. Je huyu tunamlinganishaje na yule ambaye baba yake, mjomba and whatever alikuwa ndiye afisa elimu, balaza la mitihani, nk, akabebwa akaingia chuo akafaulu kwa madesa na kuandikiwa papers, halafu kwa kuwa wazazi ni watu wa system akapewa kuwa boss mahali fulani. Ndiye ameachwa kazini! Maoni yangu nikikopa mawazo ya Prof., uhakiki ungejikita katika kuangalia utendaji wa wafanyakazi, namna ajira zao zilivyopatikana, uhusiano wa cheti na elimu ya mwenye cheti, jeee amesoma? Halafu ndio ukawekwa utaratibu huu wa kudhibiti vyeti vya waajiliwa wapya sambamba na kutengeneza mfumo wa elimu wenye kuboresha output ya elimu.