Hawa ni watanzania 10 chini ya umri wa miaka 50 walioleta mabadiliko chanya kwenye jamii kupitia vipaji na vipawa vyao walivyojaliwa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
12,580
28,286
Hii ni orodha tukufu ya watanzania wenye umri chini ya miaka 50 walioweza kufanya mapinduzi makubwa kupitia jinsi walivyojaliwa na muumba.

1. ZITTO KABWE
Haina ubishi Zitto ndo aliamsha wengi kuona inawezekana kuwa mwanasiasa mkubwa mwenye umri mdogo tena kupitia upinzani. Zitto aliingia bungeni akiwa na miaka 29 kama mbunge wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA mwaka 2005. Baada ya yeye vijana wengi waliingia kwenye siasa wakiwa wadogo na kufanya makubwa.

2. MBWANA SAMATTA
Huyu kijana hadi sasa ndo anashikilia rekodi ya mwanasoka aliyefanya makubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Ni namba moja karibu kwenye kila kitu. Kupitia yeye vijana wengi wamejua kila kitu kinawezekana hata kucheza EPL ukiwa mzaliwa wa Mbagala.

3. NASEEB ABDUL (DIAMOND PLATINUMZ)
Kama vile Samatta anavyoshikilia rekodi za kuwa mwanasoka aliyepambana na kuweka rekodi ambazo hazikuwahi kuwepo basi Diamond naye kafanya hivyo kwenye muziki. Kaamsha wengi sana.

4. MILLARD AYO
Huyu chalii wa Ara hakuna mtu atamwambia kitu oote kwenye biashara ya media. Mapinduzi aliyofanya kwenye media imesababisha kuwa na online media nyingi sana. Ni role model hado kwa wakongwe wa hiyo tasnia.

5. FRED NGAJILO (VUNJABEI)
Kimsingi Fred na mwenzie Frank Knows ndo kioo cha wajasiriamali wapya karibu wote. Ufanyaji wao wa biashara umeleta mapinduzi makubwa kwenye namna ya kufanya biashara hasa kwenye kipengele cha upangaji bei. Fred kabadili fikra za wajasiriamali wengi.

6. MamaSamia2025
Nikiwa kijana mdogo wa miaka 38 ninaweza kutamka wazi nina mchango mkubwa hasa hapa JF kupitia nyuzi na comments zangu. Nyuzi na comments nyingi hutumika kama mwongozo wa mambo mbalimbali.

7. LAUREL KIVUYO
Huyu binti ni mwanaharakati wa mambo ya mazingira. Ni graduate wa MUHAS. Katika umri mdogo sana wa chininya miaka 25 tayari kashashiriki mikutano mikubwa ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Halafu ni wa kutoka Arusha na sio Chato.

8. JOKATE MWEGELO
Hakuna asiyemfahamu kidoti ambaye kwa sasa ni boss wa UVCCM. Kina Laurel wanafanya makubwa sana baada ya dada Jokate kuonyesha mfano.

9. JORAM MKUMBI
Huyu mzee wa ulumbi kaonyesha sio lazima iwe msanii au mwanasiasa ili kuleta impact kwenye jamii. Kupitia tu lugha ya kiswahili kaweza kuhamasisha raia kujifunza zaidi lugha yao. Joram ni mfano wa kuigwa.

10. LUCAS MWASHAMBWA
Huyu jomba anapigwa vita sana hapa JF ila wanaompiga vita ndo haohao wanamkubali mbaya mbovu. Kila akishusha uzi lazima nzi wajae.. Lucas katuonyesha wazi kuwa unaweza kuwa mwanaCCM na ukajenga hoja za kukubaliwa na pande zote.
 
Bwana MENEMENE TEKERI NA PERESI amekuwa kijana wa umri wa miaka 46 kugundua kuwa dawa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI Al maarufu PEP , Sio lazima zitumike siku 28 ,zinaweza kutumika kulingana na vile mmefanya mapenzi na style mlizopeana hivyo kuamua utumie wiki au siku kadhaa au siku ishirini na nane .

Hivyo natumia jukwaa hili kumuita mvumbuzi wa mambo magumu nchini Tanzania akiwa na umri mdogo sana , apewe kongole tafadhali
 
1.Reginald Mengi (media)
2.Bakhresa (food industry)
3.Getrude Rwakatare(private schools)
4.Samia Suluhu (leadership)
5.Benjamin Mkapa (privatization)
6.Mbwana Samata (football)
7.Charles Kimei (banking and finance)
8.George Waitara (military and sport (golf)
9.John Joseph Pombe Magufuli (Leadership)
10.Jakaya Mrisho kikwete (Politics and leadership)
Hawa naona walitengeneza njia ambayo ilileta matunda kwa jamii na wengine wakachuma matunda hayo
 
Kukosekana watu kama diamond, Mo Dewji, Hassan Mwakinyo, Eng Hersi, Mange Kimambi n.k inaonyesha dhahiri umekurupuka
 
Kukosekana watu kama diamond, Mo Dewji, Hassan Mwakinyo, Eng Hersi, Mange Kimambi n.k inaonyesha dhahiri umekurupuka
Hahahaha yes diamond nimemfikiria sana kama ningeweka 11 angekuwepo ila hao wengine hapana ni WA kawaida ila diamond na kanumba hao nakubaliana wameleta mabadiliko
 
Hahahaha yes diamond nimemfikiria sana kama ningeweka 11 angekuwepo ila hao wengine hapana ni WA kawaida ila diamond na kanumba hao nakubaliana wameleta mabadiliko
Mkuu hadi Mo dewji?...tukatae tukubali huyu mtu ameleta evolution sana katika mpira wa kitanzania. Tukisema tuangalie kwa fields basi kama umemtambua samatta huna budi kumtambua mwakinyo kwenye boxing japo nidhamu yake sio kubwa
 
Kwenye banking muweke kimei.
 
Na the likes kama Millard Ayo ukiangalia sasa hiv kuna utitiri wa YouTube TVs kuna kitu kikubwa ameshawishi jamii
Mkuu hadi Mo dewji?...tukatae tukubali huyu mtu ameleta evolution sana katika mpira wa kitanzania. Tukisema tuangalie kwa fields basi kama umemtambua samatta huna budi kumtambua mwakinyo kwenye boxing japo nidhamu yake sio kubwa
 
namba 1,4 na 10 hapana,

diamond aingie anamuwakilisha kanumba kwenye tasnia ya burudani,mapinduzi ya media kafanya bakhresa group huyo mwengine hayupo,politics ya ubepari /uwekezaji ni mkapa huyo kikwete na samia wote waomba misaada nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…