MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,542
- 28,234
Hii ni orodha tukufu ya watanzania wenye umri chini ya miaka 50 walioweza kufanya mapinduzi makubwa kupitia jinsi walivyojaliwa na muumba.
1. ZITTO KABWE
Haina ubishi Zitto ndo aliamsha wengi kuona inawezekana kuwa mwanasiasa mkubwa mwenye umri mdogo tena kupitia upinzani. Zitto aliingia bungeni akiwa na miaka 29 kama mbunge wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA mwaka 2005. Baada ya yeye vijana wengi waliingia kwenye siasa wakiwa wadogo na kufanya makubwa.
2. MBWANA SAMATTA
Huyu kijana hadi sasa ndo anashikilia rekodi ya mwanasoka aliyefanya makubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Ni namba moja karibu kwenye kila kitu. Kupitia yeye vijana wengi wamejua kila kitu kinawezekana hata kucheza EPL ukiwa mzaliwa wa Mbagala.
3. NASEEB ABDUL (DIAMOND PLATINUMZ)
Kama vile Samatta anavyoshikilia rekodi za kuwa mwanasoka aliyepambana na kuweka rekodi ambazo hazikuwahi kuwepo basi Diamond naye kafanya hivyo kwenye muziki. Kaamsha wengi sana.
4. MILLARD AYO
Huyu chalii wa Ara hakuna mtu atamwambia kitu oote kwenye biashara ya media. Mapinduzi aliyofanya kwenye media imesababisha kuwa na online media nyingi sana. Ni role model hado kwa wakongwe wa hiyo tasnia.
5. FRED NGAJILO (VUNJABEI)
Kimsingi Fred na mwenzie Frank Knows ndo kioo cha wajasiriamali wapya karibu wote. Ufanyaji wao wa biashara umeleta mapinduzi makubwa kwenye namna ya kufanya biashara hasa kwenye kipengele cha upangaji bei. Fred kabadili fikra za wajasiriamali wengi.
6. MamaSamia2025
Nikiwa kijana mdogo wa miaka 38 ninaweza kutamka wazi nina mchango mkubwa hasa hapa JF kupitia nyuzi na comments zangu. Nyuzi na comments nyingi hutumika kama mwongozo wa mambo mbalimbali.
7. LAUREL KIVUYO
Huyu binti ni mwanaharakati wa mambo ya mazingira. Ni graduate wa MUHAS. Katika umri mdogo sana wa chininya miaka 25 tayari kashashiriki mikutano mikubwa ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Halafu ni wa kutoka Arusha na sio Chato.
8. JOKATE MWEGELO
Hakuna asiyemfahamu kidoti ambaye kwa sasa ni boss wa UVCCM. Kina Laurel wanafanya makubwa sana baada ya dada Jokate kuonyesha mfano.
9. JORAM MKUMBI
Huyu mzee wa ulumbi kaonyesha sio lazima iwe msanii au mwanasiasa ili kuleta impact kwenye jamii. Kupitia tu lugha ya kiswahili kaweza kuhamasisha raia kujifunza zaidi lugha yao. Joram ni mfano wa kuigwa.
10. LUCAS MWASHAMBWA
Huyu jomba anapigwa vita sana hapa JF ila wanaompiga vita ndo haohao wanamkubali mbaya mbovu. Kila akishusha uzi lazima nzi wajae.. Lucas katuonyesha wazi kuwa unaweza kuwa mwanaCCM na ukajenga hoja za kukubaliwa na pande zote.