Hawa Nghumbi amrudisha John Mnyika Mahakamani...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Mapambano yanaendelea. Hawa Nghumbi amekata rufaa dhidi ya ubunge wa John Mnyika. sasa ngoma mahakama ya rufaa.

Tausi Ally na James Magai | Mwananchi | 13 June 2012

ALIYEKUWA mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng'umbi amewasilisha hati ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyompa ushindi John Mnyika.

Ngh'umbi, alifungua kesi dhidi ya Mnyika wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akipinga matokeo yaliyompa ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu kanuni na sheria ya uchaguzi katika uchaguzi huo .

Lakini Mahakama Kuu katika hukumu yake ilitupilia mbali madai na maombi ya Ngh'umbi na badala yake ikamthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo la Ubungo. Katika hukumu hiyo aliyoisoma Mei 24, 2012, Jaji Upendo Msuya alisema kuwa Ngh'umbi alishindwa kuthibitisha madai yake na kuonesha jinsi madai hayo yalivyoathiri matokeo ya uchaguzi huo.

Baada ya hukumu hiyo Ngh'umbi alielezea kutokuridhika na uamuzi huo na kudai kuwa anakwenda kujadiliana na wakili wake ili kuona ni hatua gani ya kuchukua. Jana Ngh'umbi kupitia kwa wakili wake, Issa Maige, alianza rasmi mchakato wa kupinga hukumu hiyo baada ya aliwasilisha Mahakama ya Rufani hati ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

MY TAKE:

Hivi kweli huyu Mama hakubali tu asubiri mwaka 2015 na kujipanga vizuri??
 
magamba bwana, mtahangaika sana, ila inaonekana magamba wameshajiandaa kufanya vitu tofauti hapa haiwezekani mtu na akili zake aendelee na kesi isiyo na kichwa wala miguu
 
magamba bwana, mtahangaika sana, ila inaonekana magamba wameshajiandaa kufanya vitu tofauti hapa haiwezekani mtu na akili zake aendelee na kesi isiyo na kichwa wala miguu
kuna kesi za maana na wenye haki hawapati haki, halafu huyu mama anaona ni mwafaka kwenda kuhangaika tena mahakamani

this is a waste of time and resources....

tatizo kubwa sana hili
 
magamba bwana, mtahangaika sana, ila inaonekana magamba wameshajiandaa kufanya vitu tofauti hapa haiwezekani mtu na akili zake aendelee na kesi isiyo na kichwa wala miguu

mkuu chitalula nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa hapa, huenda wameona baada ya kushindwa plan A, sasa ni zamu ya plan B ambayo lazima watawin. tungoje tuone
 
Last edited by a moderator:
Huu upuuzi utaisha lini?

Halafu huyo wakili naye, duuuuh! Sijui ndiyo kuganga njaa huko....

Huu si upuuzi ni delaying tactic ya magamba wanataka Mnyika awe muda wote anashugulika na kesi aache kushugulikia maendeleo ya Jimbo lake ili 2015 ajenda yao iwe kuwa mbunge wenu alitumia muda wote kushugulkia kesi ona hakuna maendelo, Magamba hawafanyi kitu bila objective hata kama objective ya kijinga au ya kiovu!!
 
kuna kesi za maana na wenye haki hawapati haki, halafu huyu mama anaona ni mwafaka kwenda kuhangaika tena mahakamani

this is a waste of time and resources....

tatizo kubwa sana hili

Kama kweli sisi tunaheshimu utawala wa sheria na demokrasia pia lazima tukubali kuwa ni haki yake kikatiba kukata rufaa! Acheni aende huko mahakamani tena haki ndio itapatikana huko! sasa kama mahakama zetu hazipo huru ( kama wengi tunavoamini na tulivoshuhudia segerea et al) basi hilo ni swala jingine la kushugulikia kwenye katiba mpya kwamba tufanyeje ili mahakama ziwe huru zisiwe remote controlled bna wanasiasa walio madarakani??
 
A typical Mary go round scene
 
Attachments

  • sVillageKidsPlaying%5B1%5D.jpg
    sVillageKidsPlaying%5B1%5D.jpg
    23.6 KB · Views: 94
Kama kweli sisi tunaheshimu utawala wa sheria na demokrasia pia lazima tukubali kuwa ni haki yake kikatiba kukata rufaa! Acheni aende huko mahakamani tena haki ndio itapatikana huko! sasa kama mahakama zetu hazipo huru ( kama wengi tunavoamini na tulivoshuhudia segerea et al) basi hilo ni swala jingine la kushugulikia kwenye katiba mpya kwamba tufanyeje ili mahakama ziwe huru zisiwe remote controlled bna wanasiasa walio madarakani??

Wengi tuliingia kwenye mtego huu wa kila tatizo kuligeuzia kwa katiba mpya lakini tnashindwa fahamu kuwa hata hiyo katiba mpya nayo ni tatizo maana mchakato wa kuunda sheria haukuwa shirikishi, hivyo tusitarajie jipya under the CCM regime. The regime is more about cronyism than serving a country.

Hawa Ngumbi atakuwa amehemewa na kulipa gharama za kesi baada ya kuona kuwa alifungua kesi ya kupinga kitu kisichokuwepo kwa kufuata ushauri mbaya wa kisiasa aliota Rajabu Makamba (Former katibu wao). Nafikiri watakuwa wamemtosa alipie gharama na njia pekee kaona huenda akate rufaa ki-note cha Ikulu kinaweza tumika kumwepusha na kulipa gharama. Lakini pia anatakiwa kujua kuwa ni bora kulipa gharama za kesi kuliko kuwa na gharama za kuandaa uchaguzi mwingine ambao pasi na shaka CCM itashindwa vibaya tu, maana vijana wameisha gundua formula ni kulinda kura. Kama kulinda kura ni kosa kwa mtazamo wa CCM basi 2015 wajiandae kwa kesi zaidi ya 200 katika majimbo watakayopoteza.
 
Kuna Kutafuta Haki na Kuna kutafuta Upuuzi, Huyu mama sasa ni Upuuzi, Hajali maendeleo ya watu wa Ubungo, kama ana akili angetumia muda mwingi kuwa karibu na wananchi kufanya shughuli za maendeleo na sio kuhamia mahakamani, nadhani she is attention seeker, bahati mbaya she is getting a wrong attention.
 
Hata uchaguzi ukiitishwa leo tukaweka Hawa na Mbwa,
Mbwa anashinda kwa kishindo.
 
Amekosa U-DC na Ubunge Lol.Je atapata ulaji wapi, kweli nimeamini hana kazi nyingine anayoweza kufanya zaidi ya hivi vyeo vya kupewa.Aende akalime, si viongozi wengi wanasema vijijini kuna fursa nyingi za Kilimo, aende kijijini kwao akawakomboe ndugu zake kama kauli mbiu ya ma RC na dc (Si alishakuwa DC)
 
Huyu mama hatumtaki ubungo, analazimisha nini? Tena saizi ndio tumeshaelewa uwezo wake mdogo. Anapoteze fedha na muda.
 
Hii mbinu ya kumuumiza kisaikolojia mnyika kipindi hiki cha bunge lakini ndo inazidi kumwimarisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom