Hawa ndiyo warithi wa rais Magufuli

unaweza kuwa na jambo jema ukakosea tu muda wa kulitenda. sina hakika kama anachofikiri bwana JPM na Mpango, lakini nina uhakika kuwa approach yao sio sawa! Jambo la kwanza baada ya uchaguzi ilipaswa kuwa umoja wa kitaifa na maridhiano. hatua ya pili mikakati ya kiuchumi kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi na ahadi, tatu utekelezaji wa ahadi, nne tathimini ya utekelezaji, tano maandalizi ya uchaguzi ujao.
mimi baada ya uchaguzi nimeona kuzima bunge live, marufuku mikutano ya siasa, wanasiasa kufungwa, vyombo vya habari kuzimwa, wafanyabiashara kutishwa, maduka kufungwa, wafanyakazi kutumbuliwa, kilimo kuchechemea, mifugo inakufa, kufukua makaburi ya kodi huku tukiacha ya mafisadi na kuyasiliba zaidi. kweli uchaguzi ujao taambulia kitu?
 
Mbowe anahangaika kuwanasa wauza sura instagram eti kwakuwa wanapata like nyingi anafikir ndio atakavyoshawishi watu kuipigia kura cdm...
Kichaa pekee ndiye ataweza kuwa na fikra Kama hyo
Do not underestimate the power of fools in a large group..Wema may look like a "blondie"lkn ana wafuasi nyuma ambao hata wema akinyaa wanazoa ndo hao watakaopigia kura chadema kama walivopigia ccm.Usimdharau Influence anayo pamoja maupuuz take yote ! Usijifariji sana ni ukweli mchungu
 
Ulianza vizuri,ila hapo kwenye 2020 Mbowe kuandaa safu kuchukua nchi ndo umeleta ndoto zako za weekend hii.Hivi huwa hamjiulizi na kushauri kwanini badala ya upinzani kupigania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi wapo bize na kumpokea Wema Sepetu na upuuzi mwingine?,halafu chaguzi zote huwa wanadai wameibiwa mbona wanaendelea kushiriki?,.,hivi vyama vitawafanya mchizike,hawa jamaa akina Mbowe and Co.LTD wapo kwa ajili yao na familia zao tu,hawana uchungu na mwananchi wa chini yeyote,ndo maana JPM alivyopiga mkwara kwenye UKUTA watangulize wake zao na watoto wao,wakaona kawapatia wakahairisha,za kuambiwa jumlisha na zakwako.
UKIWA NA HAKILI ZA KURUSHIWA , MATOKEO YAKE NDO HAYA. JITAFAKARI MKUUU
 
Do not underestimate the power of fools in a large group..Wema may look like a "blondie"lkn ana wafuasi nyuma ambao hata wema akinyaa wanazoa ndo hao watakaopigia kura chadema kama walivopigia ccm.Usimdharau Influence anayo pamoja maupuuz take yote ! Usijifariji sana ni ukweli mchungu
Dada unaamini kwenye kuhesabiwa kura mpaka leo?,.,Ok tuseme chama fulani kina akina Wema kama 100 hivi na wafuasi wao,baada ya kupiga kura let say 2020 wanaambiwa wakae mbali,matokeo yanapangwa na mshindi anatangazwa,unaenda wapi kulalamika?,tume ya uchaguzi ni hii hii na katiba ni hii hii,na Mbowe na wenzake wanajua hayo yote,kinachofanyika sasa hivi ni Wema anapewa kama Mil 100,kwenye makaratasi ya chama zinaandikwa kapewa mil 200,wanagawana na maisha yanaendelea,hivi vyama visiwafanye mapoyoyo,hawa jamaa wapo kipesa zaidi,nyie huku mkiwa na imani na chama.Hizi kesi unazoziona za CDM usifikiri wanazichukia,zinawapa nafasi ya kujilipa posho kibao za ruzuku,wenyewe wakifurahia nyie huku mkichukia kwa hasira,za kuambiwa changanya na zako.
 
Ndani ya majani kuna nyufa. Zile nyufa alizowahi kuzizungumzia hayati baba wataifa.

Lazima mbegu hii iote upya kuna taasisi izaliwe upya ili nchi iweze kusonga mbele kwa kupata mawazo mapya.

Yuko wapi Malema wa Tanzania?
 
Watanzania bwana wanavituko sana, hivi kuna presidential material hapo? Nadhani tunapaswa kufuata mfumo wa Marekani wa electoral college votes hili kukwepa kuchaguliwa maraisi ambao ni wanasifa za kuwa wenyeviti wa mitaa. Nchi za dunia ya tatu wananchi wake wengi ni wajinga, so wanachagua mtu kwa kuangalia upepo, wakienda mbali ni ukabila au udini.
 
Back
Top Bottom