Hawa ndio wafanyabiashara wakubwa wa sukari nchini

Umetoa maelezo mazuri lakini utambue kuwa behind any government there is a team of rich men. Hilo sharti ulitambue. Kwa hiyo hata serkali imara kama Marekani, Urusi, Uingereza, n.k. msingi wake umesimama kweye nguzo za kundi la matajiri. Hivyo vyovyote tutakavyofanya, hili kundi tunalihitaji

Nenda kajielimishe tena kuhusu na uje hapa utuambie je kundi hilo la watu matajiri ni lazima wawe raia wa nchi husika au unaweza kuchukua hata raia wa nje. Je kundi hilo la watu tajiri wanatakiwa wafanye biashara halali au haramu
 
Said Amin Shamo si ndio mmiliki wa Shamo tower zote mbili za mbezi beach? Wengi tulijua msomali mhamiaji kumbe ni balozi? Hii chain inatisha sana ....JPM kweli anahitaji maombi kama kweli huna unafiki.
Hii ni ngoma nzito lakini katika watu wasiotaka kushindwa, Rais Magufuli ni mmojawapo.
 
hujaeleweka nani anayenunua sukari kwa 110000 au 120000?
na je ni sukari yawapi inayonunulika kwa bei iyo?
ninafsi nanunuaga kilo 25 kwa sh 38000/= bei hii ni ya jumla na kabla haijaadimika. sijatembelea maduka toka ianze kwuwa adimu nikajua soko likoje.
Mzabuni hununua sukari ya ndani kwa tsh 110000 ukiweka Na gharama za uchukuzi wa kufika mahala husika huwa inaongezeka Na kua umenunua sukari kwa tsh120000 alafu bei mpya ya mkataba wa Gpsa unasoma sukari kwa tsh1800@kg ...Na pia SAA ingine huwa adimu kabisa ...

Sent from my D2502 using JamiiForums mobile app
 
Uhujumu uchumi ni kosa washughulikiwe tu. Watu hawaelewi kuwa biashara haina maana tuwe unethical. ...utafichaje kitu kwa maslahi yako binafsi?
 
Rais Magufuli ana vita pevu kuhusu mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini.

Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha.

Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji.

Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini.

Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar.

Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake.

Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali.

Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake.

Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na mwagizaji mkuu wa sukari kwa ajili ya soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari

Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu.

GO9G5020.JPG

tanzania uchumi tutaurudisha sifuri kwa staili hii.

hivi hawa tunaowaharasi wakiamua kuondoa motaji yao na kuipeleka kwingine tunapata nini au huyu kapuku anayekuja kuwaharasi hawa ataagiza sukari ikiwa inahitajika?

lazima tuone ukweli kuwa hapa tulipo hawa wametusaidia sana, kama mizani ya biashara haijakaa sawa ni ujinga tulioulea kwenye jamii yetu na sio kosa lao.

tunachokitaka ni hawa kuendelea kutoa mchango wao huku jamii ikijinga kuwainua na hawa makapuku wanaopiga kelele wapate mitaji.

sijui tunafikiri maswala haya ni kupanga foleni tu na tunachojaribu ni kuwatoa walioko mbele yetu ili sisi tulioko mbali tufike. sio rahisi ki hivyo.

tujipange taratibu na mitaji ya hawa itatusaidia kufika tunakokwenda.

kwa mtaji huu wa kuwaharasi wafanyabiashara nchi hii wakati mnajigamba kuingia katika uchumi wa viwanda mtaviua hata vilivyopo na kuelekea kwenye zero
 
Mzabuni hununua sukari ya ndani kwa tsh 110000 ukiweka Na gharama za uchukuzi wa kufika mahala husika huwa inaongezeka Na kua umenunua sukari kwa tsh120000 alafu bei mpya ya mkataba wa Gpsa unasoma sukari kwa tsh1800@kg ...Na pia SAA ingine huwa adimu kabisa ...

Sent from my D2502 using JamiiForums mobile app
iyo ya sh 110000 ni sukari kiasi gani kg 100?
 
Hapo red kwann usingesema tu ni Lizaboni adi useme ni mwanamke? Ina maana wanawake uwezo wetu wa kufikiri ndo uko kusini kabisa ama? umenikera kwa kauli hiyo.

nirudi kwenye mada kuu, sina hakika na swala la JK kuwa muingizaj wa zukar ilihali sijaona kama ame classify kama hao wengine kama ana exclusive permit ama ni kwasababu ya viwanda vyake.

sikubaliani na dhana kwamba kwakua hawa waningiza sukar basi ndio maana sukari haipatikan kwan Mengi, Bakhressa, Dewji, wao wanaingiza za viwanda vyao na kwa hili hawapaswi kupewa lawama kwani moja wapo ya malighafi zao ni sukari. hao aliosema wana exclusive permit ni watu wawili tu ambao pia sidhan kama wanaweza kusatisfy soko na sukari la nchi hii ambayo mahitaj yake ni tani laki 6 na mpaka sasa viwanda vyetu vyote vinauwezo wa kutengeneza tani laki 3 tu.

Istoshe kuna watu ambao sijaona akiwataja hapa kama huko Moshi tumeskia kuna mtu ana miliki hadi jana tanzi zaid ya elfu 2 za sukari, na kwenye list yake huyu Mangi hajawekwa. Pia amesahau mikoa ya mpakan kama Mbeya na Arusha kuna sukari nyingi zana inayotoka Zambia na Kenya inaingia nchini kwa njia za panya hii inasadikiwa ndiyo inayofanya kwenye maeneo haya sukari ya ndani kuwa na bei kubwa ilihali hiyo ya nje kuwa na bei ndogo kwsabbu hailipiwi kodi.

labda niseme hivi tatizo la sukari hapa nchini hili ni janga, toka enzi za Nyerere. sababu kubwa ikiwa ni ufinyu wa utengenezaji kwenye viwanda vyetu ambao wao wamebaki na technolojia ya kutumia miwa tu, ambao hata uotaj wake kwa miaka hii ya sasa unachangamito nyingi sana. kuna vitu vingi ambavyo bado pia vingeweza kutumika kutengeneza sukari kama vile beet roots ambazo kwa nchi za Ulaya hii ni malighafi hasa kwenye uzalishaj wa sukari,

jambo jingine ni viwanda husika kutokuwa na uwezo wa kujiendesha kama ipasavyo kwa kipindi chote cha mwaka. mfano mzuri Mtibwa sugar ni kama mwez wa 8 sasa hawafanyi kazi wamefungiwa na NEMC kisa mazingira yao sio mazuri. mwekezaj alowekeza pale ni mtanzania ila anaanguka kwenye lile kundi la wawekezaj wazawa wasojua nini maana ya biashara na vipi ifanyike ili faida iwe sustainaible. inamaana sasa tunatengemea Ilovo na TPC na Kagera na hivi vyote bado uzalishaj kwao ni mdogo sana ni tani laki 3 tu wakati matumiz yetu ni tani laki 6.

inabidi juhudi za makusudi zifanyike ili kunusuru hali hii manake kwasasa hata kwenye maduka ya kina mangi mtaan sukari hakuna kabisa.
Suluhisho ni aidha kuongeza uzalishaji kwa kujenga viwanda vipya au kuongeza uzalishaji wa miwa ili kukidhi hitajio la malighafi viwandani au kuingiza sukaribkutoka nje. Hakuna suluhisho zaidi ya hapo.
 
Na ni vema tukumbushane kwamba, Mzee Mugabe alianza hivyo, sasa hivi Zimbabwe ni nchi yenye njaa kuliko zote kusini mwa Afrika mwaka huu

Mhhhhhhhhhhhhhhhh prophets of doom...Ni kweli vita anayopigana JPM ni nugumu lakini hivi kweli unataka kuilinganisha Zimbabwe na Tanzania?!
 
Mzabuni hununua sukari ya ndani kwa tsh 110000 ukiweka Na gharama za uchukuzi wa kufika mahala husika huwa inaongezeka Na kua umenunua sukari kwa tsh120000 alafu bei mpya ya mkataba wa Gpsa unasoma sukari kwa tsh1800@kg ...Na pia SAA ingine huwa adimu kabisa ...

Sent from my D2502 using JamiiForums mobile app
Hueleweki unachoeleza. Hivi data ulizoweka hapo unaona mtu anaweza kuzitumia kufanya ulinganifu wa kimahesabu?? Kajipange upya.
 
Suluhisho ni aidha kuongeza uzalishaji kwa kujenga viwanda vipya au kuongeza uzalishaji wa miwa ili kukidhi hitajio la malighafi viwandani au kuingiza sukaribkutoka nje. Hakuna suluhisho zaidi ya hapo.
mie najiuliza for more than 50yrs bado utegemez wetu wa sukari umebaki kwenye miwa tu. tell me viwanda vyote vinavyotengenza sukari mashamba yao ndo yanayotumika kuzalisha miwa hakuna mtu baki anayeuza miwa kwenye hivi viwanda. sababu kubwa ni land scarcity, na maeneo ambayo yamekuwa cleared kwa ajili ya kilimo yamebaki kuwa ni ya kilimo cha mazao ya chakula zaid kuliko mazao ya biashara.

Istoshe viwanda vyetu vina matatizo sana hakuna technolojia mpya miundo mbinu mibovu nk. Nashauri MARI waje na aina mpya ya mazao yanayoweza kutumika kuzalisha sukari zaid ya miwa.

pia rais asiendeshe nchi kama ni familia yake na Janeth ajue kabisa hii ni nchi apende kuskiliza ishu kutoka kwa watu wanaofaham mambo. soon ya zimbabwe yatakuja hapa
 
Ndugu yangu kiufupi ni hivi sukari dukani imepanda sana mfuko wa kg50 ni tsh 110000 Na bei nnayoenda kuiuza ni tsh90000 kwa mfuko huo huo nasukari yenyewe imekua adimu sana ....Usipoelewa ni wapi
 
Rais Magufuli ana vita pevu kuhusu mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini.

Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha.

Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji.

Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini.

Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar.

Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake.

Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali.

Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake.

Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na mwagizaji mkuu wa sukari kwa ajili ya soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari

Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu.

GO9G5020.JPG
Good story,observation yangi ni kuwa hawa Sir Chande,Mwapachu na Lowassa umelazimisha tu kuwaLink/kuwataja kwy hii kashfa ya sukari ,ni wazi kuwa hawaconnect hapo,mnyonge anyongwe na haki yake apewe!
 
mkuu,tema mate!naomba tusifike uko!

Tutafika huko sio muda mrefu.
Sheria ya uhujumu uchumi haifai kwenye soko huria.
Magufuli ameingia na mawazo yake kutawala nchi yenye watu mil.45 na bahati mbaya washauri wake nao hawataki tena kufikiri kwa kina zaidi ya kumshangilia kwa kila jambo analofanya.

Wenzetu wanasonga mbele kwa kutumia mfumo huu huu wa soko huria sisi tunaingiza siasa kwenye mambo ya kitaalam.
Soko huria linatakiwa lidhibitiwe kwenye kodi tu na ubora wa bidhaa lakini sio vitisho na propaganda.

Eti wanaficha sukari ili mwezi wa ramadhani sukari ikosekane halafu wapandishe bei. Wale wasio waislam wanakubaliana na propaganda hizo bila kufikiri zaidi kuwa haijawahi kutokea kwa matajiri wakiislam kufanya ulanguzi wakati wa mwezi wa Ramamdhani na pia kwa nini tusifikiri kuwa hawa matajiri walikua wanahofia kukosekana kwa sukari mwezi wa ramadhani ukizingatia kuwa sukari iliyopo inaweza kutumika kwa siku nne tu.

Sheria ya uhujumu uchumi iliwekwa wakati wa chama kushika hatamu na wakati huo serikali ilikuwa inafanya biashara zote kubwa. Ilitungwa ili kuweka mazingira ya kuzuia watu kuhujumu biashara za serikali.
 
hakuna jambo baya kwenye maisha kama kupania.
JPM amepania sana kumu outsmart JK ila amesahau kabisa kwamba hata yeye sio malaika
 
Umasikini ni mbaya,lkn umasikini wa fikra ni mbaya zaidi..!! Umasikini wa mleta mada na wa watu wa aina yake ndo umasikini unaomfanya mtu awe mchawi. Asili ya uchawi ni umasikini wa fikra.

Watu wanaagiza sukari kwa pesa zao,na unasema wana viwanda vyao,tatizo lao ni nini sasa!!? Huu utaratibu wa kununua na kuweka ni utaratibu uliopo duniani kote. Wahindi wengi wamefanikiwa kwa kuweka akiba ya dhahabu wanasubiri ipande bei. Nenda kule ifakara na shinyanga,kuna wafanyabiashara wananunua mpunga maelfu ya tani kila msimu wanasubiri bei.

Punguza wivu kijana,utakuwa mchawi..!! Mwambieni Rais aruhusu waagize sukari hizi comedy zenu hazitupeleki popote.
Mkuu umeongea pointi sana.. maana kuna watu wanadhani mfanyabiashara hana haki ya kuweka akiba..
 
Ndugu yangu kiufupi ni hivi sukari dukani imepanda sana mfuko wa kg50 ni tsh 110000 Na bei nnayoenda kuiuza ni tsh90000 kwa mfuko huo huo nasukari yenyewe imekua adimu sana ....Usipoelewa ni wapi
sasa umeona hapa umeweka iyo 110000 ni kwa uzito wa kg 50. Hili ndilo ulilokuwa unakosa kuliweka toka mwanzo.
well kama bei ya sukari imepanda kwenye soko la dunia basi bodi ya sukari inalazimika kutuambia hilo, na hapa inabidi wamshauri rais na hata wataalam wa mambo ya uchumi inabidi wawefocused jaman wanaipeleka nchi kubaya.
 
Back
Top Bottom