Lakasa chika7
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 454
- 1,264
- Thread starter
- #21
Mipangomingi hoja yako mzuri sanaKobelo una mapenzi sana kwa serikali hii kiasi ambacho hata ikikosea, wewe hauko tayari kukiri na kurekebisha. Mimi pia ninayo lakini ikikosea sipo tayari kutetea pale inapokosea.
Huo ufananisho unaousema hauna "causation effects" yoyote ya Tanzania nayo kufikia mafanikio hayo eti kwa kuwa tunatumia "take-off" ileile. Wewe (probably) ni mchumi na unajua namna uchumi ilivyo na kawaida ya kutegemeana. Mwaka 2010 nilikuwa Vietnam na timu moja nayofanyia kazi, nachoweza kukwambia jiridhidhishe na "contributing factors" zilizoifanya Vietnam iwe hapo ilipo.
Pili, Vietnam "kiasili" ni agrarian economy ikihusisha uuzaji nje wa bidhaa za misitu (forestry) na crude oil, pamoja na uvuvi kutokana na fisheries resource abundant walionayo. Na mpaka sasa bado ni wazalishaji wazuri. Mchele wa Vietnam ni mfano mzuri wa commitment ya Vietnam kwenye kilimo.
Tatu, Vietnam imenufaika na vitu viwili ambavyo vimeisaidia sana kupata mafanikio ya viwanda unavyoviona. Baadhi wanaita "overflowed" FDI kutoka nchi za Asia kulikosababishwa na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji katika nchi za NIECs, Japan pamoja na China pia. Idadi ya watu, rasilimali, strong govt export strategy, stable macroeconomic policy ambazo hazikuwa zikiendeshwa na "who is in the power" na sera ya serikali ya kuhimiza elimu hasa kutoka vyuo vya nje ya Vietnam (scholarships Ulaya, Asia na America) kumefanya wawekezaji waliokuwa wakikimbia gharama za uzalishaji katika nchi hizo kutupia jicho nchi hiyo(kitu ambacho tumeshindwa kukitumia hapa kwetu). Tukubali ukweli, graduates wetu hawaajandaliwa kufanya kazi za uzalishaji. Kubwa wanachoweza ni "ukada" ima wa chama tawala au vya upinzani. Kwa uchache, Mhe. Rais angefungua ukurasa mpya sana kama yale mabilioni ya Ndege (kama unakumbuka hata IMF wametilia shaka jambo hili) yangetumika kujenga walau "very modern institutes of technology/schools of engineering" 5 ambapo program zingeendana na kile tunachotaka kuzalisha na kuuza kani pia zingekuwa center za ukuzaji wa teknojia za viwanda na uzalishaji.
Kwa kawaida nchi yoyote inayotaka kuingia kwenye uchumi wa viwanda ni lazima ijibu maswalia ya masingi ambayo ni (1) Tunataka kuwa specialized wa kuzalisha nini? (2) Tunatarajia kuuza katika soko lipi na how stable soko hilo na je ni akina nani washindani wetu katika soko hilo? Usiniambie Soko la Afrika Mashariki ambalo 80% ya prospect consumers ni ama informal au hawana permanent and stable income. (3) Ni nani atazalisha bidhaa hizo(government, PPP au wholly private?), (4) Je tunao wataalam wa kuzalisha bidhaa husika? (5) Ni wapi tunakusudia kuchukua Teknolojia ya bidhaa hizo? (6) Je tuna service industry ya kutosha ya ku-support viwanda hivyo? (7) Very common, mahitaji ya Nishati katika uzalishaji. haya ni mambo saba ambayo kila moja linaandaliwa "empirical strategy" yake. Bila majibu ya maswali ya namna hii nchi ya viwanda itabaki kuwa slogan kama slogans zilizopita.
Nne, Vietnam na nchi nyingi za Asia zina geografia nzuri ya uzalishaji kama zilivyo za Ulaya na America.
Tano, Vietnam ilijitenga na "siasa" za majitaka ima kimataifa au kitaifa. Na hili ni muhimu sana, Uchumi wa uzalishaji hautaki kutengeneza matabaka kati ya "wao" na "sisi". Unahitaji strong policy credibility and well coordinated and inclusive politics ambapo raia wote bila kujali vyama vyao, makabila yao au rangi yao wanashiriki katika kuijenga nchi yao. Hizi siasa za mtu A kwa kuwa hayuko au yupo affiliated na siasa fulani hana nafasi ya kushiriki maendeleo ya nchi yake haijawahi kufanikiwa popote.
Sita, Vietnam haikupuuza role ya wafanyakazi ikiwa pamoja na incentives ili kuchochea innovation. Hili ni jambo ambalo limepewa msukumo na nchi zote zilizopata mafanikio ya kiuchumi. Mfanyakazi anayekwenda kazini ili kutimiza siku usifikirie akama anaweaza kusimamia mapinduzi ya viwanda. Wafanyakazi wenu hawako "motivated" kabisa. This is very fundamental ikiwa tunataka mabadiliko ya kweli. Kama wafanyakazi wamezidi, ni bora hata Serikali ikafanya 'retrenchment exercise" ili kubakiwa na wachache lakini iwalipe vizuri ili wafanye kazi. Ni bora kutumia mabilioni kadhaa kuwalipa wafanyakazi fidia kuliko kubaki na wafanyakazi unawalipa kidogo lakini hawako motivated. Wafanyakazi wamekuwa vidampa wa wanasiasa.
Kobelo ndugu yangu, Tanzania nchi yetu sote lakini tukubali there are some progress which are commendable, lakini kuna makosa mengi sana ya kimkakati tuko nyuma nayo ambapo suluhu yake sio "ndiyo mzee" hususan kwa wale ambao wapo Serikalini. Maendeleo dunia ya sasa ni jambo lililorahisishwa, kuna extensive resources and technology copying ambapo nchi kama zetu zinaweza kuzitumia. Hebu fanyeni simple survey hizi nchi za China, Korea, Taiwan, Vietnam, Malaysia, Singapore nk zimefanyaje badala ya kila mmoja kuja na nchi yake ya marejeo. Mtangulizi wa sasa alikuwa na Malaysian Model wewe naona unasema tunakwenda na Vietnam Model!!!!! Hii nini maana yake?
Anyway, usiharibu utaalam wako kwa kuwa kibaraka wa wanasiasa.