Ripoti ya Richmond 'kuanikwa' leo
Na John Daniel, Dodoma
HATIMAYE hamu ya wabunge kutaka kuona na kujua wahusika katika mkataba wenye utata wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond itakidhiwa leo wakatakapokabidhiwa rasmi ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa Katika mkutano uliopita.
Habari za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali zilieleza kuwa hadi jana asubuhi, kazi ya kukamilisha ripoti hiyo ilikuwa ikiendelea na ilitarajiwa kumalizika jioni na kuwasilishwa mezani kwa Spika leo na baadaye kugawiwa kwa wawakilishi hao wa wananchi.
Ripoti ile ni kubwa sana, si kama zile ambazo tulizoea kutoka kwa mawaziri (kauli za mawaziri), kuanzia wiki nzima inafanyiwa kazi ya maandalizi na leo (jana) ilikuwa kwenye hatua za kuwekwa majalada ili kesho (leo) wagawiwe wabunge, kilisema chanzo chetu.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, hakukataa wala kukubali kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo na kusisitiza kuwa atatangaza kila kitu leo asubuhi.
Nitatangaza kila kitu kesho (leo) saa nne asubuhi, kikubwa tu mtu wako asikose kuwapo, alisisitiza Bw. sitta na kuomba mwandishi wa habari hizi kuvuta subira mpaka leo atakapoweka mambo hadharani.
Wakizungumza na Majira baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda majina yao yatajwe, walisema wao hawana taarifa hizo, ila wamepata matumaini mapya kama itakuwa hivyo, hasa baada ya Spika kusitisha ziara yake ya Marekani na kusisitiza kuwa ndicho walichokuwa wanasubiri kwa hamu.
Ni wazi, kwamba hizo ni habari njema sana kwetu na kwa wananchi waliotutuma kuwasemea, lakini nakuhakikishia kuwa hatutamlinda mtu yeyote atayeonekana alishiriki kinyume na taratibu, alisema mmoja wa wabunge wa CCM.
Kuanzia juzi, vikao kadhaa vya wabunge wa CCM vilikuwa vikiendelea huku jambo kubwa ikidokezwa kuwa ni juhudi za kutaka kuweka mambo sawa, hasa baada ya joto zaidi kupanda, hata wabunge kugoma kujadili muswada wa umeme na biashara ya mafuta, hadi watakapopokea ripoti ya Richmond na kujua kilichomo.
Katika hali iliyoonekana kuwa si ya kawaida, kikao cha Kamati ya Uongozi ya CCM, pia kilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, ambapo ilidaiwa kuwa ajenda kuu ilikuwa ni kujipanga kwa ajili ya ripoti ya Richmond.
Awali akitoa matangazo baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Naibu Spika wa Bunge, Bi Anna Makinda, alisema kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM ambacho kilipangwa kufanyika jana sasa kitafanyika leo saa 2 usiku.
Kwa hali ilivyokuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa ndicho chanzo cha kuahirishwa kwa kikao chetu leo (jana), kuna mambo ambayo yalikuwa hayajakaa sawa, hivyo ilibidi kwanza kiahirishwe mpaka hayo yakamilike kwanza, kilisema chanzo chetu kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.
Habari zaidi zilieleza kuwa Kamati ya Uongozi ya chama hicho kilichofanyika juzi, kilihoji uwezekano wa wabunge wa CCM kukutana kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo na kwamba yaliyomo ni lazima yajadiliwe kwanza na wabunge hao kabla ya kutoa mawazo yao bungeni kesho.
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwasili mjini hapa kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri huku kukiwa na taarifa kwamba baada ya kikao hicho, kutakuwa na jambo jipya linaloweza kuleta mabadiliko makubwa katika siasa na uongozi wa nchi.