Hatimaye Damu yetu haikumwagika Bure Uganda, Tunalipwa!

una matatizo ww sio bure....akili zako zimekaa ki cult cult tu!
Hana matatizo Ila wewe huna weledi wa kuainisha mada hujui Kenya Uganda Rwanda Burundi walikaa pamoja mpaka JK akaongea na taifa hatujitoi,pia hujui Kenya kuna al-shab na walushasema hawaipigi bongo kwanini asipitishe bomba huku
Acha kufikiri kwa kutumia makalio
 
Barbarosa,

..subiri kwanza mpaka utakapoona mkandarasi yuko site na ujenzi umeanza.

..at that time sote tutakuwa na sababu ya kushangilia.

..Museveni alishakuja Tz na kutupa matumaini kuhusu mradi wa reli ya Tanga-Musoma kwa ajili ya mizigo ya Uganda.

..baadaye Museveni huyohuyo akajiunga na genge la CoW lilokuwa likiinanga Tz.

..labda kwasababu Magufuli ni mfuatiliaji mzuri huenda miradi hii ikazinduliwa karibuni.
 
Raisi Museveni wa Uganda amesema sababu za nchi yake kuamua kupitisha bomba la mafuta nchini mwetu ktk Tanga mpaka Uganda badala ya nchi ya Kenya ni kulipa fadhila kwetu kwa kazi kubwa na isiyo ya kibinafsi tulioifanya huko Uganda ya kumtoa Idi Amini!

Leo hii Uganda ni nchi nzuri inayostawi kwenye ngazi zote, uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa na hii yote ni kwa sababu tulijitoa mhanga kwa ajili yao, hivyo kama tusemavyo Waswahili wema hauozi, hatimaye Raisi Museveni amelitambua hilo!

Hili Bomba kwa mujibu wa Raisi Magufuli lina thamani ya 4 bilion US dollars na litazalisha ajira kwa watu zaidi ya elfu 15! TanZania ya viwanda hiiyo inajongea kwa kasi kabisa!

Sasa Bandari yetu ya Tanga itapata kazi na kuwa busy na hii ni neema kubwa kwa Mji na Mkoa wa Tanga!

Come babe come!!!!!

HAPA KAZI TU!
Hizo ajira15,000 katika nafasi gani? Sehemu kubwa watakuwa vibarua na watanzania tulivyo wavivu kutwa tutagoma kudai tunaonewa. Bora Jumuiya ianze kufanya kazi mapema tupate nguvu kazi.

Naona hiki kitu kimekuexcite sana. Check the underlined!! Ama kweli kila mtu na starehe yake.
 
Kwa hiyo kama ungekuwa wewe ndiyo Raisi ungefanyaje labda? Ungewakatalia Uganda kujenga Bomba la mafuta na kutumia Bandari ya Tanga?
Ningewaruhusu kwa MKATABA ULIO NA FAIDA KWA WOTE. Ila sio kuiweka kisiasa zaidi
HONA huyu mleta mada anavyojipendekeza eti wwnalipa fadhila! wakati ipo kawaida tu. Kipaumbele kama rais ningeweka kipaumbele uchunguzi ww mafuta nchini
 
Sasa kama ni kweli unavyosema huwo Ujinga uko wapi? Au ndiyo staili ile ile ya kutokuelewa maana ya upinzani kwamba ni kupinga kila kitu hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo?

Haijalishi sababu ni ipi ile tu kwamba nchi ya Uganda itatumia Bandari yetu ya Tanga ni sababu tosha ya sisi kusherehekea kwani Bandari yetu itapata kazi ya uhakika!
Hili Bomba litagharimu dola Bilion 4 za Kimarekani ina maana sehemu ya hii fedha itawekezwa Tanzania yetu, hapo ni win win situation kwetu kuanzia mafundi wa ujenzi wa bomba mpaka mama lishe wa kuuza vyakula site kuendelea mpaka kwa wahandisi
watu wetu watapata ajira za moja kwa moja na zingine zisio za moja kwa moja!

Na hata kama Uganda wakiuza mafuta kwetu hauoni kwamba watakuwa wametusaidia sana badala ya sisi kuimport? tena hili Bomba litakuwa limejengwa siyo kwa fedha zetu ina maana litatuletea mafuta nyumbani!
hivi hufikirii hata ardhi yetu itakayotumika? hivi ni maekeari mangapi yatapotea kwa kuruhusu upitishaji wa bomba hili. sio kila kitu ni kukimbilia tu kusifia. au litapita angani hilo bomba?
 
Nafikiri labda haujaelewa suala zima linahusu nini!

Ni hivi Uganda wanataka tu kutumia Bandari na ardhi yetu kusafirishia Mafuta yao kwa kifupi hakuna tofauti na Zambia wanavyotumia Bandari yetu kusafirishia Shaba yao, hivyo sisi tutalipwa kwa matumizi ya bandari yetu na pia bomba kuwa kwenye ardhi yetu sasa sielewi hapo tatizo lako liko wapi?
 
duhh!! Huyu ndugu haoni faida ya bomba la mafuta kupita nchini kwetu kweli? Siamini ninachokisoma. Tuwe tunafanya tafiti kabla ya kujirusha hewani. Wengine tunachafukwa roho haraka, tusaidiane kwani hatupendi kurusha makombora.
hivi lile bomba la TAZAMA linafanya kazi hata sasa?
 
hivi hufikirii hata ardhi yetu itakayotumika? hivi ni maekeari mangapi yatapotea kwa kuruhusu upitishaji wa bomba hili. sio kila kitu ni kukimbilia tu kusifia. au litapita angani hilo bomba?

Kwani linapitishwa bure kwenye ardhi yetu?
 
Kwani linapitishwa bure kwenye ardhi yetu?
Wamesema watatulipa shilingi ngapi?

Je ilo bomba linajengwa kwa fedha za Uganda au tunachangia ujenzi?

Pia ningependa kujua ramani ya mradi huo, Je unapitia maeneo gani hadi ufike Uganda?

Mwisho huo mradi utaanza lini na wanategemea kuukamilisha baada ya muda gani? au bado ni proposed project?
 
Mwanzoni huwo ndiyo ulikuwa mpango yaani kupitishia Bomba Kenya lkn kikwazo kikubwa kwenye hili wala siyo Raisi Museveni bali ni kampuni ya Total ambayo ndiyo wawekezazi, wao hawataki kabisa kupitishia Kenya kwa sababu ambazo wamezisema za kiusalama!

Wanahofia usalama wa mali zao huko Kenya hivyo CEO wa Total siku zote alitaka kupitishia Bomba Tanzania badala ya Kenya lkn sasa nafikiri siasa za kenya na Uganda zikawa zinaingilia kumbuka kwamba Ug
hapa ndipo faida ya al shabaab naiona
 
Sasa kama ni kweli unavyosema huwo Ujinga uko wapi? Au ndiyo staili ile ile ya kutokuelewa maana ya upinzani kwamba ni kupinga kila kitu hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo?

Haijalishi sababu ni ipi ile tu kwamba nchi ya Uganda itatumia Bandari yetu ya Tanga ni sababu tosha ya sisi kusherehekea kwani Bandari yetu itapata kazi ya uhakika!
Hili Bomba litagharimu dola Bilion 4 za Kimarekani ina maana sehemu ya hii fedha itawekezwa Tanzania yetu, hapo ni win win situation kwetu kuanzia mafundi wa ujenzi wa bomba mpaka mama lishe wa kuuza vyakula site kuendelea mpaka kwa wahandisi
watu wetu watapata ajira za moja kwa moja na zingine zisio za moja kwa moja!

Na hata kama Uganda wakiuza mafuta kwetu hauoni kwamba watakuwa wametusaidia sana badala ya sisi kuimport? tena hili Bomba litakuwa limejengwa siyo kwa fedha zetu ina maana litatuletea mafuta nyumbani!
Kwa mara ya kwanza leo nakuunga mkono.. Mipumbavu inaona ni heri tununue mafuta kwa waarabu kuliko jirani yetu.. Tena kama ndio hivyo waanze kuchimba hata kesho hayo mafuta ili pesa yote ibaki hapahapa East Africa
 
nilipata kuhudhuria mkutano mmoja wa wadau wa afrika mashariki hili pia lilikuwa kwenye Plan ukweli Uganda wanatumia bandari hii kwa ukaribu ukilinganisha na Mombasa kingine in kuangalia fursa zaidi ambazo Uganda inaweza kufaidika nazo ukichukulia tuna ardhi kubwa ya bure isiyiyodhibitiwa kwa wageni kikamilifu achilia ajira za kumwaga ambazo matajiri wa Tanzania wanadharau wazawa na kuthamini wageni na uraia usiosumbua kivile na rushwa za kumwaga!
 
Mwaka huu mtajinyonga kwa wivu...
Avatar yako vinalandana na huyu ndugu
1457022812031.jpg
 
duhh!! Huyu ndugu haoni faida ya bomba la mafuta kupita nchini kwetu kweli? Siamini ninachokisoma. Tuwe tunafanya tafiti kabla ya kujirusha hewani. Wengine tunachafukwa roho haraka, tusaidiane kwani hatupendi kurusha makombora.

Nimecheka sana
 
Wamesema watatulipa shilingi ngapi?

Je ilo bomba linajengwa kwa fedha za Uganda au tunachangia ujenzi?

Pia ningependa kujua ramani ya mradi huo, Je unapitia maeneo gani hadi ufike Uganda?

Mwisho huo mradi utaanza lini na wanategemea kuukamilisha baada ya muda gani? au bado ni proposed project?

Bomba linajengwa na Kampuni ya Total ambayo ndiyo wenye mafuta au niseme waliowekeza Uganda, sisi kazi yetu ni kusafirisha tu mafuta yao na kuvuta mkwanja hasa kwenye kodi bandarini pindi mzigo wao uingiapo au kutoka!
 
Raisi Museveni wa Uganda amesema sababu za nchi yake kuamua kupitisha bomba la mafuta nchini mwetu ktk Tanga mpaka Uganda badala ya nchi ya Kenya ni kulipa fadhila kwetu kwa kazi kubwa na isiyo ya kibinafsi tulioifanya huko Uganda ya kumtoa Idi Amini!

Leo hii Uganda ni nchi nzuri inayostawi kwenye ngazi zote, uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa na hii yote ni kwa sababu tulijitoa mhanga kwa ajili yao, hivyo kama tusemavyo Waswahili wema hauozi, hatimaye Raisi Museveni amelitambua hilo!

Hili Bomba kwa mujibu wa Raisi Magufuli lina thamani ya 4 bilion US dollars na litazalisha ajira kwa watu zaidi ya elfu 15! TanZania ya viwanda hiiyo inajongea kwa kasi kabisa!

Sasa Bandari yetu ya Tanga itapata kazi na kuwa busy na hii ni neema kubwa kwa Mji na Mkoa wa Tanga!

Come babe come!!!!!

HAPA KAZI TU!
Ungesubiri kidogo kabla ya kushangilia. Hadithi ya Uganda na reli ya Tanga, bomba la mafuta la Tanga, bandari ya Tanga ni ya muda mrefu na haina mwisho - "It is a never enfing story"
 
Back
Top Bottom