chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,679
- 27,929
Ilitarajiwa Wizara ya habari kupitia taasisi zake na wasemaji wake wahakikishe ujumbe wa serikali unafika na unaeleweka kwa Watanzania.
Mtihani mkubwa kwa wizara hii ni kuelezea bajeti ya nchi kwa lugha rahisi ieleweke, sio bajeti tu, bali maamuzi mbalimbali ya serikali.
Lakini kitu nilichoona katika tozo ya miamala, Mwigulu aliachwa peke yake, hii wizara pamoja na msemaji mkuu wa serikali, hawakuonekana popote kuisemea serikali, ambalo ni jukumu lao la msingi.
Hawa ni watu wa mwendazake ambaye Sera zake na za awamu ya sita ni mbingu na ardhi, naweza kuhisi wanahujumu kiaina ili maamuzi ya awamu ya sita yasieleweke sawia kwa wananchi.
Pia ninahisi hawa watu wa mwendazake walishibishwa propaganda na marehemu kiasi kwamba hawawezi kugeuka nyuma wakawa jiwe la chumvi.
Ni bora mama akatafuta na kusuka kikosi bora cha habari ambacho kitahakikisha maamuzi ya serikali yanaeleweka, hayapotoshwi.
Msigwa na Hassan Abass wamepwaya, Msigwa apewe ukurugenzi wa halmashauri, Hassan Abass atafutiwe kazi nyingine.