Hashim Rungwe Sipunda: Huyu mnayemuita fisadi si mumkamate au nyie waongo?

Wana JF, Hivi kweli maoni ya mtu kama huyu nayo yanaletwa JF! hajui hata Universities zilikuwaje miaka 10 iliyopita halafu naye eti alitaka kuwa rais!

Ajabu kuna mtu mbele yake anaitikia kwamba katoa points. Ktk miaka kumi ya utawala ni trilioni ngapi za bajeti zimetengwa ktk serikali? Matumizi yake yalikuwa ni UDOM, barabara ya kijitonyama, uwanja wa songwe, uwanja wa Mwanza, Uwanja wa Dar, BRT basi! Hivi kweli huyu angekuwa ni rais, nini tungeona. Hajui kwamba hayo mambo yalianza kabla ya miaka 10 na mengine hayajafika mwisho hadi leo.
Kuna mafisadi mbona hamuwakamati na tumewapa kila kitu? Majeshi, mapolisi, kodi mnakusanya mbona mmeshindwa kuwakamata hao mafisadi?
 
Hoja ya Mzee Rungwe imejikita kwenye nadharia kuwa nchi ilipinda. Yeah, ukitazama kwa ualhalisia, mzee awam ya nne ameacha Legacy, leo Dar ina mambo mengi ya kisasa, majengo,BRT,Daraja la Kisasa na la kipekee, kila binadam ana mapungufu yake. Kipekee nasema awam iliyopita ilijitahidi, ilipasa kuendelea pale tulipoishia na kusonga mbele, ila kuwa awamu iliyopita ni kama haikuacha legacy bali ni kupinda tu, hapo hapana.


Ndo maana nasema huyo Rungwe binafsi amenifurahisha sana kwani yeye kama Mpinzani amekiri kwamba Serikali ya CCM imefanya makubwa sana nchi hii na ameyeorodhesha kinyume na baadhi ya watu wanavyopotosha kwamba CCM haijafanya chochote miaka 50 ya Uhuru, kuhusu Awamu ya V sijawahi kusikia yoyote akisema Serikali ya CCM ya Awamu V haijafanya chochote hata raisi Magufuli mara nyingi sana amesema Mzee Kikwete na Serikali yake wamefanya kazi kubwa sana muacheni apumzike!
 
Bavicha mnahangaika sana masikini. Hata chizi akimkosoa rais mtakuja na thread kumuunga mkono kwasababu mnafanana tabia
Unaelimu gani wewe ya kulinganisha na Hashimu Rungwe?
 
Kwa size na hadhi ya hoja, ni Moses Machali au Felix Mkosamali wanastahili kumjibu mwenzao.
 
Tatzo people who think kama mzee wangu jiran Yangu na mtani wangu spunda hawana a room to give there thoughts matokeo Yake wote wanakuwaga wagombea tu vYama vinakuwa vingi
 
Mimi namjibu kwa haraka na urahisi kabisa kwamba yote aliyoyataja ambayo ni mambo mazuri kabisa kufanywa na Serikali ya CCM, yamefanyika kwa kipindi cha miaka 10 pamoja na Awamu nyingine zilizopita yaani II na ya III, hivyo kutegemea kwamba ndani ya Mwaka I Awamu ya V ifanye mengi zaidi ya Awamu tatu zilizopita ni ujinga na kwanza hakuna mashindano kwani wote ni Viongozi wa CCM na wanatekeleza Ilani za CCM!

Ila nimefurahia kwamba Upinzani wamekubali kwamba CCM imefanya makubwa Tanzania kinyume na wengine ambao husema kwamba miaka 50 hakuna kilichofanyika, hivyo nimefurahi kwamba mme bow down kwamba Nchi yetu inasonga mbele tena kwa kasi ya ajabu kama Mpinzani alivyosema!
Bado hujajibu hoja za Wakili Nguli na na Msomi wa Mahakama ya Rufaa, Rungwe Hashim Spunda.
Mwenyekiti wenu anasema nchi imepinda,How ????
Imepinda wapi ?
To which Direction ?
 
Sijui waswahili tuna laana ya wapi. Hivi hii nchi maendeleo yake hupimwa kwa mifano aliyoitoa Rungwe? Kuwa Kariakoo inang'aa? Kuwa barabara zote lami? Kuwa university ziko zaidi ya 40? Kuwa viwanja vya ndege vinapanuliwa? Kuwa kuna mwendo kasi? Ndio vipimo vya maendeleo hivyo?

Hivi ukubwa wa kiwanja cha ndege unanisaidiaje mimi mwananchi wa kawaida ikiwa watalii na wafanyabiashara wa kimataifa wanatumia viwanja hivyo kutorosha nyara za serikali na kupitisha dawa za kulevya?

Hivi maghorofa ya kariakoo yaking'aa yanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida ikiwa wafanya biashara hao wanatoa rushwa na kukwepa kodi hivyo kuwa na faida mara dufu?

Hivi bara bara za lami zikiwa nchi nzima kwanini reli nayo isifanye kazi ya kusafirisha mizigo mizito kutoka pwani kwenda bara ili bei ziwe nafuu na barabara zidumu kuepusha gharama kubwa ya matengenezo ya barabara hizo kwa fedha ninayolipa kodi? Reli ilifia wapi? Mbona yenyewe haing'ai?

Hivi kuwa na vyuo vikuu 40 vibavyojazwa na watu wasio na sifa mpaka elimu inalazimishwa kuonekana nzuri wakati ni hovyo kwa kuweka mpaka division 5? Graduated wanaotoka katika vyuo hivyo 40 wanaenda wapi? Kuna mazingira ya ajira hata kujiajiri?

Mwendo kasi unamsaidia nini mwananchi wa Bunda?

Hivi hali ya huduma za afya mahospitalini Rungwe anaijua vizuri?? Hata sasa kaangalie huduma hata Bugando uone zilivyo mbovu (mbovu).

Majibu gani Rungwe ajibiwe? Kusoma hamjui hata picha?
 
Hakuna namna awamu hii kufanya hata nusu tu ya alofanya kikwete. Itabaki maneno tu. Nikiangalia
Dart mwendokasi
Uwanja nyerere inter 3
Bara bara 60% ya nchi
Chuo kikuu muhimbili Mkomanzi
UDOM
Flyover ubungo
Flyover Tazara
Heart Institute muhimbili
Barabara ya kisasa mbezi bahari beach
Songwe airport mbeya
MOI 2 muhimbili
School za secondary kila kata
Heshma kimataifa
Uhuru wa bunge
Uhuru wa kukosoa
Kunterezi 1 and 2 umeme wa gas
Upanuzi hospital za temeke mwananyamala
Ujenzi wa nyumba na NHC
Miradi mikubwa ya nyumba ya NSSF
Daraja la Kigambini
Miradi mikubwa kama bandari kubwa ya bagamoyo
EPZ ya mkapa
Fedha na biashara kukua siku hadi siku
Imani ya wawekezaji
Ukuaji wa viwanda binafsi mfano Azam juice nk
University kibao zaid ya 30

Sidhani kama haya tutayafika ....
 
Back
Top Bottom