Kaka kuilinganisha subaru na harrier ni kuikosea heshima subaru,, subaru ni subaru tu hebu tutake radhi sisi wazee wa subaru lakini ni kwasababu umesema umeendesha subaru kidogo tu ulivyokuwa mwanza kwa hiyo bado hujaijua vizuri. Gari ina speed sana ile halafu iko stable, kingine haichagui barabara hlf haina tofauti kwenye tambarare wala mlima speed ni ile ile. Halafu ni all weather road yaani kwa kifupi ni gari yenye power sana. Mimi namiliki subaru forester ya 2004 ni gari nzuri sana halafu ni nyepesi kuchanganya kwa sababu nikiondoka kwa kasi inanichukua sekunde 8 tu mshale wa speed kutoka 0 to 100. Na kuhusu mafuta ni utumiaji wako wewe mwenyewe kwa sababu nikiamua kukimbia sana huwa kweli linanipiga mafuta lakini nikiliendesha kistaarabu wala halinipigi. Kwenye spea zake ndo kuna gharama kidogo na ni kwa sababu spea zake ni genuine ukifunga utasahau. Lakini kwa ushauri wangu subaru ni gari zuri sana na halina magonjwa yakijinga kijinga na ikitokea limepata tatizo muone fundi anayejua subaru kwani ukipeleka tu kwa fundi mradi ni fundi utajuta kitakachokupata