Hapa uchawi unahusika?

Jibu ni rahisi sana. Kama wewe ni mkristo tafuta watumishi wa mungu wakuombee (watumishi hasa sio wale ambao matendo yao yanakinzana na maneno yao).
Kama ni muislam fuata taratibu za kufanyiwa dua.
Hapo utatatua tatizo lako.
 
kwa vile umeshamjua mbaya wako,nakushauri umrudie muumba wako fanya sala kwa bidii nakuhakikishia ndani ya mwezi mmoja maisha yako yatanyooka
 
Uchawi upo,nothing is impossible under the sun.Muombe msamaha dadako kwa lolote ulilomkosea,mwachie vya urithi then sikilizia.
 
kaka sijamdhulum chochote yaan mi nlikuwa msaada mkubwa kwake wakati nasoma boom langu ndilo lilikuwa linaendesha maisha yake na yaangu mpaka pale mahakama ilipoidhinisha usimamizi wa mirathi uwe kwake ndipo alipoanza hizo fujo na huwa anasema mimi si mtoto wa yule baba hivyo sina haki ya chochote,hilo la mali mimi sikujihusisha nalo maana nilikuwa natafuta zangu na nilifanikiwa ila mzozo ulipanda kwa kuambiwa si wa baba yake....pia shemeji ndo anachochea ili apate kuzitumia pesa hizo
sasa kumbe sio zako ni za baba wa dada ako kwanini uling'ang'ania?!
 
Habari ya kazi wakuu!,

Mimi ni kijana wa miaka 31 na nimehitimu degree ya uhasibu mwaka 2011. Mwaka huo huo nlipata kazi kwenye kampuni binafsi na maisha yakawa yanaenda vema tu mpaka mwaka 2014 mwezi wa 3 ndipo maisha yakabadilika nakuwa hayaeleweke.

Ni kwamba mwaka 2012 niliingia katika ugomvi na dada angu wa baba na mama mmoja tukazozana juu ya mali za urithi wa wazazi wetu. Dada alinipigia simu na kuahidi kuwa atanikomesha na shemeji yani mume wa dada akasisitiza lazima niwajue (ieleweke shemeji ni nmganga wa kienyeji) basi siku chache nikafukuzwa kazi bila sababu za msingi,nikapata kazi tena lkn nikafukuzwa pia na matatizo yakawa yanaendelea yani watu wananichukia bila sababu mara ugomvi na mke wangu hauishi tena usio na kichwa wala miguu,ndoto za ajabu ajabu hasa kuota napigana na watu nisiowajua au nawajua,kila nachofanya hakifanikiwi hata kama nitakuwa makini sana,hivi sasa sina muelekeo wa maisha na kila kitu hovyo kabisa...

Je, naweza nisaidiwa vipi kujiondoa ktk janga hili?,kuna uwezekano kweli mtu akavuruga mipango yako kimazingara?
Okoka tu!!! Kinachokusumbua ni hofu na wao wanatumia hofu yako.
 
Amini kwa Allah hakuna litakalo kupata bila yeye kutaka hata kama ni uchawi yeye ataweza kukuondolea kwa kuombewa na mungu atakusaidia bali hujasema ukweli wote Nawewe ulikwenda kwa mganga gani kujihami baada ya vitusho hivyo
 
Maombi kwa jina LA Yesu hayashindwi chochote.amini,soma neno,omba..nakuhakikishia baraka zako zinazoitea zitakurudia kwa jina LA Yesu.
 
Wapo kaka, ila wengi matapeli, be careful , mi namjua mpemba mmoja ni komesha,but wewe mkristo,na yeye ana solve matatizo kupitia Qur'an,, ,yupo sehemu moja inaitwa kunduchi pwani,,,,

wataalamu wa kwenda kwenye tunguri....asilimia 90 wanaokwenda kwa babu wanawake
 
Matatizo ni sehemu ya maisha ya Mwanadamu, ukiweza kuyakwepa tumia nguvu zako zote, hakukuwa na sababu ya kugombea urithi ilhali ulishapata elimu iliyokuwezesha kupata kazi ya kumudu familia yako. Mzazi anaposomesha mtoto ni ili akihitimu ajimudu ktk maisha yake sio kuja kulipa fadhila au kusubiria urithi. Fanya maombi/nenda ktk mambi maalumu vunja nguvu za giza utarudi ktk hali yako, Dua kama ni Muislam.
 
mmmh mkuu hakuna siku nliyogombea urithi soma vizur
 
Sikia omba kukutan na sister wako au mtafute kwa njia ya amani.
Takana nae amani, ondoa vinyongo vyote.

Hata kama hatokusikiza na kukubali ila tamka kuwa upo oky na umesamehe yote na omba msamaha kama umekosea mahali.

Baada ya hapo, anza kupiga goti mbele za Mungu muombe aingie kwenye maisha yako , kuna faida nyingi sana ukiwa mtu wa kumshirikisha Mungu kwenye maisha yako.

Mwanzoni hauta pata mtiririko mzuri na kwa urahisi but hakuna ku stop endelea. Kabidhi kazi za mikono yako, maisha yako yote pamoja na afya kwa Mungu. Mkeo pia amshirikishe haya, hakuna ambalo ni gumu kwa Mungu hakuna . Yeah unaweza ona kuwa hujui uombeje na kwa namna gani Mungu analijua hilo na ndio anasema kwenye maandiko yake kuwa sisi hatujui kuomba kama ipasavyo ila Roho Mtakatifu hutusaidia.

God only God can help you mwanadamu atatumika kama njia ya upatanisho tu.
Nimependa hapo pa kumwomba msamaha, mkuu Kajole fanya hivyo, usijali kama atakusamehe au atakutukana! ....cha muhimu ni kinywa chako kuomba msamaha.
 
"Hakika shetani hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanaomtegemea Mola wao" (Quran 16:99)
"Wala mchawi hafaulu popote afikapo" (Quran 20:69)
"Msiogope, Bila shaka MIMI ni pamoja nanyi; nasikia na naona" (Quran 20:46)
"Mwenyezi MUNGU ni mlinzi wa wale walioamini, Huwatoa katika giza na kuwaingiza kwenye Nuru" (Quran 2:257)

Ndugu yangu mtegemee Mwenyezi MUNGU tu; Muamini Yeye tu, utauona Mkono wa Mwenyezi MUNGU katika maisha yako. Mimi nimeuona mkono wake nawewe utauona. Soma Zaburi 23 na Quran 2:255 utapata nguvu mpya ya kuzidi kumtegemea Mwenyezi MUNGU.
 
"Hakika shetani hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanaomtegemea Mola wao" (Quran 16:99)
"Wala mchawi hafaulu popote afikapo" (Quran 20:69)
"Msiogope, Bila shaka MIMI ni pamoja nanyi; nasikia na naona" (Quran 20:46)
"Mwenyezi MUNGU ni mlinzi wa wale walioamini, Huwatoa katika giza na kuwaingiza kwenye Nuru" (Quran 2:257)

Ndugu yangu mtegemee Mwenyezi MUNGU tu; Muamini Yeye tu, utauona Mkono wa Mwenyezi MUNGU katika maisha yako. Mimi nimeuona mkono wake nawewe utauona. Soma Zaburi 23 utapata nguvu mpya ya kuzidi kumtegemea Mwenyezi MUNGU.
aameni
 
Habari ya kazi wakuu!,

Mimi ni kijana wa miaka 31 na nimehitimu degree ya uhasibu mwaka 2011. Mwaka huo huo nlipata kazi kwenye kampuni binafsi na maisha yakawa yanaenda vema tu mpaka mwaka 2014 mwezi wa 3 ndipo maisha yakabadilika nakuwa hayaeleweke.

Ni kwamba mwaka 2012 niliingia katika ugomvi na dada angu wa baba na mama mmoja tukazozana juu ya mali za urithi wa wazazi wetu. Dada alinipigia simu na kuahidi kuwa atanikomesha na shemeji yani mume wa dada akasisitiza lazima niwajue (ieleweke shemeji ni nmganga wa kienyeji) basi siku chache nikafukuzwa kazi bila sababu za msingi,nikapata kazi tena lkn nikafukuzwa pia na matatizo yakawa yanaendelea yani watu wananichukia bila sababu mara ugomvi na mke wangu hauishi tena usio na kichwa wala miguu,ndoto za ajabu ajabu hasa kuota napigana na watu nisiowajua au nawajua,kila nachofanya hakifanikiwi hata kama nitakuwa makini sana,hivi sasa sina muelekeo wa maisha na kila kitu hovyo kabisa...

Je, naweza nisaidiwa vipi kujiondoa ktk janga hili?,kuna uwezekano kweli mtu akavuruga mipango yako kimazingara?
Jibu pekee la kushinda giza ni kuitafuta nuru. Tafuta kumjua Mungu na uweza wake wenye nguvu kuliko hizo nguvu za giza anazotumia Dada yako na mumewe.

Sikushauri na wewe utumie giza yaani nguvu za kichawi kushindana nao maana utakuwa umefungua mlango mwingine wa matatizo zaidi na kuyamilikisha maisha yako na familia yako kwa shetani.

Tafuta mtu yoyote anayemjua Mungu vizuri, mshirikishe tatizo hili na mwingie kwenye maombi. Itapendeza sana kama hujaokoka ukampa Yesu maisha yako kwani hii inakupa "full access" ya kuliamrisha jeshi la Malaika kupambana na hizo nguvu za kichawi /kiganga.

Kila la kheri.
 
Kama unahitaji maombi nifate inbox.
Maombi si jibu ndugu yangu, Jibu sahihi ni yeye kumtegemea Mwenyezi MUNGU kwa asilimia mia moja, Na huwezi kumtegemea Yeye kama humuamini; Kwa hivyo, Ufunguo Mkuu ni Imani, Kumuamini Mwenyezi MUNGU ndio Ufunguo Mkuu kabla hata ya kumtegemea. Baada ya kumuamini ndio amuombe Mwenyezi MUNGU moja kwa moja, hakika Mwenyezi MUNGU anasikia na anaona, sio lazima fulani akamuombee, huko ni kumtegemea muombezi baadala ya Mwenyezi MUNGU. Akiwa na wasiwasi usiku wa manane pia akupigie wewe simu ili umuombee? Mfundishe namna ya kumtegemea Mwenyezi MUNGU na jinsi gani yeye mwenyewe aombe msaada kwa mwenyezi MUNGU kwa kutumia neno lake, Hakika Mwenyezi MUNGU ni mwaminifu wa neno lake na wala yeye havunji miadi.

Neno linasema
"Na waja wangu watakapo kuuliza khabari Zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie Mimi, nawaniamini Mimi, iliwapatekuongoka” (Quran 2: 186).
"Na Anayemcha Mwenyezi MUNGU Humtengenezea njia ya kutokea” (Quran 65: 2). Na anayemtegemea Mwenyezi MUNGU Yeye humtosha” (Quran 65: 3).“Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu” (Quran 2: 45). Aya hizi ni za Quran, kama huiamini, soma Biblia, kuna aya nyingi sana zinadhihirisha nguvu za Mwenyezi MUNGU, ni wewe tu kuamini na kuanza kutumia. Soma zaburi 23 na Quran 2:255 utapata faraja hata kama mashetani wenye pembe ndefu wamekuzunguka. Ili roho wa MUNGU na awe ndani yako muda wote sharti zake zipo kwenye (Zaburi 1:1-3), hizo ni universal principles, si dini, bali ni neno la Mwenyezi MUNGU.

Off-course kuna mambo mengi kabla hata ya kufanya hayo, anatakiwa afanye toba huku akisamehe wote waliomkosea ili naye apate kusamehewa. Aisiwe vuguvugu vinginevyo shetani atamshinda, Achague kuwa wamoto au wabaridi. Vita ya kiroho ni kama vita ya kawaida ya kimwili, kama huna silaha, utashindwa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom