HansPoppe : Safari hii hatutaki wachezaji wa kuokota kijiweni kama Kiiza

Mkuu, maisha ya kambini yana mambo mengi ya siri. Huku nje mnaweza kumuona mtu amapiga mabao lakini akiwa kambini anashawishi migomo. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa soka ya mataifa ya Africa, basi utakumbuka kuwa Samuep Eto'o, E R
basi tuupewakati wakati wake
 
Football ni team work ndo inayofanya timu ipate matokeo tofauti na tennis.

Sasa huyo striker anayewahakikishia kutupia goli kila mechi ni wa kufikirika tu sababu hata kwa wenye soka lao,hakuna striker wa aina hiyo.

BTW:Huko aliko sasa ana-record hiyo? Wapi?

Halafu haya mambo ya kuficha ficha majina yamepitwa wakati.
 
Huyo Zakaria ni bure kabisa, eti ndiyo anayefanya usajili!!!!

Hebu hawa viongozi wajisumbue angalau kidogo tu kujifunza wenzao wa ulaya wanafanyaje na wanaendeshaje vilabu.

Sijawahi sikia kauli ya kijinga kama hii kwa hao wenzetu wa ulaya.

Mtu anapoitumikia timu no matter what mchango wake lazima uheshimiwe tu, eti Kiiza walimtoa kijiweni?????
Yaleyale ya Amis Tambwe, huku kukurupuka na kutafuta sifa sijui kunawasaidia nini..!!!!
 
Huyo ndo fundi/ mtaalamu wa Dar Young African mwaka huu hata shirikisho watachukua
 

Attachments

  • IMG-20160526-WA0001.jpg
    IMG-20160526-WA0001.jpg
    42.8 KB · Views: 31
Football ni team work ndo inayofanya timu ipate matokeo tofauti na tennis.

Sasa huyo striker anayewahakikishia kutupia goli kila mechi ni wa kufikirika tu sababu hata kwa wenye soka lao,hakuna striker wa aina hiyo.

BTW:Huko aliko sasa ana-record hiyo? Wapi?

Halafu haya mambo ya kuficha ficha majina yamepitwa wakati.
alinacha story
 
Huyo Zakaria ni bure kabisa, eti ndiyo anayefanya usajili!!!!

Hebu hawa viongozi wajisumbue angalau kidogo tu kujifunza wenzao wa ulaya wanafanyaje na wanaendeshaje vilabu.

Sijawahi sikia kauli ya kijinga kama hii kwa hao wenzetu wa ulaya.

Mtu anapoitumikia timu no matter what mchango wake lazima uheshimiwe tu, eti Kiiza walimtoa kijiweni?????
Yaleyale ya Amis Tambwe, huku kukurupuka na kutafuta sifa sijui kunawasaidia nini..!!!!
kweli nilikua namuheshimu sana unless kama waandishi wamemnukuu vibaya na hata TFF ikemee hili
 
Mkuu, maisha ya kambini yana mambo mengi ya siri. Huku nje mnaweza kumuona mtu amapiga mabao lakini akiwa kambini anashawishi migomo. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa soka ya mataifa ya Africa, basi utakumbuka kuwa Samuel Eto'o, Emmanuel Adebayor na Benni McCarthy kwa vipindi tofauti waliwahi kuachwa kuitwa kwenye vikosi vya mataifa yao kwa sababu za kuchochea migomo ya posho, lakini wote hao walikuwa wachezaji mahiri wanaopachika mabao. Sasa itakuwa Kiiza?
Acha hizo wewe, Kiiza ni mchezaji mzuri,kuhusu kusapoti mgomo viongozi ndio wanasababisha haya,unawacheleweshea mishahara yao unategea nini?Simba imejaa siasa na nakuambia tutaendelea kulia kwa uongozi huu.Wachezaji wa kigeni hawalipwi,unategemea nn kwa hawa wa nyumbani wasio na sauti?Unavunja timu kila msimu kujenga upya badala ya kuongeza nguvu penye mapungufu!!!Mimi ni mshabiki nguli wa Simba,Lakini kwa uongozi huu wa kisiasa na ubabaishaji,Simba ikishinda sawa ikifungwa pia sawa.Mana najua hatufiki popote.
 
I can imagine isingekua magoli ya kiiza sijui simba ingeishia nafasi ya ngapi, namuheshimu sana Hans ila kwa hali yoyote kama kiongozi ni muhimu kuwa makini na kauli.............hata aveva naye kumtumbua kessy haikua stahiki ilihali krossi nyingi za kessy zilizaa mabao and i can also imagne krosi za kesst Tambwe atafunga sana....time will tell....unajua hata Phiri ananukuliwa kusema Tambwe si straika wa aina yake..........
Mkuu Amavubi huwa unanifurahisha sana kwa ukweli wako. Hakika umekomaa kimichezo.

Kiiza siyo wa kubeza kama alivyofanya huyo Popo, natarajia hata wachezaji wa Simba waliopo wamtake amwombe radhi Kiiza. Bila Kiiza Simba ingekuwa pabaya zaidi ya hapo. Dogo alijitolea sana kwa ajili ya Simba lakini leo amelipwa kejeli.

Popo siyo mwanamichezo hata kidogo, yuko pale Simba kwa maslahi yake binafsi.
 
Huyo foward ataekuwa anatupia kila game anatoka dunia gani!!!! Basi kama kweli ana uwezo huo hata Ronaldo na Messi hawamfikii.
Unajua kaka hawa wazee ifikie hatua wakae pembeni wawaachie vijana wafanye kazi na cjii watajifunza ln? Wamekaa kiupigaji gaji eti straika wa kufunga kila mechi na waandish wetu walivomanjanja wanaandika habari zahivi. Hivyo unaweza kukuta amehakikishiwa 10% ndo maana mzee akKimbilia kwenye vyombo vya habari. Mambo ya usajili aachiwe kocha sasa huyu mzee ni kocha mambo mengine yanatia hasrA mpka basi naonatujiandae kushuka daraja tukiendekeza mazee mapiga dili ya namna hii
 
....nyie kandambili huku mnajidai mnajua saaana kuishauri Simba,mmeambiwa na kocha wenu Manji akiondoka,timu inakufa baada ya wiki!!....
endeleeni kujifanya masharobaro kwa nguo za kuazima!! iko siku...
 
....nyie kandambili huku mnajidai mnajua saaana kuishauri Simba,mmeambiwa na kocha wenu Manji akiondoka,timu inakufa baada ya wiki!!....
endeleeni kujifanya masharobaro kwa nguo za kuazima!! iko siku...
Mchango wa Manji pale Yanga si wa kubeza hata kidogo kama Popo alivyobeza mchango wa Kiiza huko vyura fc. Hata hivyo Manji ana umri mdogo, hata nusu ya umri wa Yanga hafikii. Kabla ya Manji Yanga ilikuwepo, wakati wake Yanga ipo na hata atakapoondoka Yanga itaendelea kuwepo.

Shukrani kwa Manji kwa mchango wake unaoonekana hata kwa vipofu lakini haimaanishi kuwa bila yeye Yanga itakufa, hayo maneno yalisemwa na kocha zaidi ya miaka 7 iliyopita (Tazama tarehe ya gazeti).
 
Kiiza kumbe alikua kijiweni?sasa walimsajiri wa nn mtu wa kijiweni?..ila wakijiweni kafunga goli 19,yule mgosi sijui wa wapi?kafunga goli 1 tu
 
nakumbuka Kitwanga alimuuliza swali mbunge (akiwa amelewa) 'unauliza nyumba ngapi kwani wewe una miaka mingapi? sasa Manji ana miaka mingapi na Yanga ina miaka mingapi hadi IFE LEO?
 
hivi kwa nini hawa viongozi hawajifunzi. walitakiwa waanze na kocha aje na mikakati yake na wachezaji wa aina gani anaowataka kutokana na mifumo yake. then wamtafutie msaidizi ambaye yupo kwenye ligi yetu zaidi ya miaka 3 ili amsaidie kupata majina ya aina ya wachezaji anaowahitaji kwa mifumo yake. kocha na msaidizi wapeleke majina kwenye kamati ya usajili ya aina ya wachezaji wanaowahitaji. lakini cha ajabu kamati ya usajili imeshaanza kusajili mwezi huu wa tano kocha ataletwa mwezi wa saba mwishoni na bado mwezi wa nane mwanzoni wataletwa wachezaji double dobule kwa majaribio maana bado kamati ya usajili itakuwa inaendelea na usajili (sijui huwa wanasajili nini kwa zaidi ya miezi 4)! hapo mwishoni ndio utaona wakina niang, papa ndaw wanapishana airport. mwisho wa siku kocha naye anachanganyikiwa anasajili galasa kama papa ndaw halafu analaumiwa wakati kamati ya usajili ndio inamchanganya pamoja na presha ya kuwahi dirisha la usajili kufungwa. kwa viongozi makini timu inajengwa kwa kuanzia na wachezaji waliopo sio kufukuza wachezaji zaidi ya 15 na kusajili zaidi ya 15 kila mwaka. ukiangalia wachezaji wote waliofukuzwa simba miaka miwili mitatu iliyopita wengi wao ndio wanang'ara kwenye ligi na ndio waliinyima simba ubingwa mwaka huu hili ni somo tosha kwa viongozi. kocha kwanza usajili wa wachezaji baadae vinginevyo mwaka mwingine wa kilio kwa sisi wapenzi wa simba.
 
..
Simba imejaa siasa ... Lakini kwa uongozi huu wa kisiasa na ubabaishaji,Simba ikishinda sawa ikifungwa pia sawa.Mana najua hatufiki popote.
Nini maana ya siasa? Siasa ni kitu kibaya? Kwangu mimi siasa ni utaratibu, na ningependa ikibidi timu zote ziongozwe kisiasa
 
Back
Top Bottom