Hamad Rashid aomba huruma ya Rais kuwa makamu

Watu wanasikia kichefuchefu wakiona kifungu hiki, kila anayekuja anakataka pale anapoona panamfurahisha yeye lakini ukweli kifungu kinasomeka hivi;

39(i)(ii)
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10%) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais,
au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

Ndio maana Hamad Rashid anachosema, makamu wa rais toka upinzani kwa uchaguzi huu hakuna, bali nusuru ni nafasi mbili za uwakilishi wa baraza katika nafasi kumi za rais za upendeleo sababu kikatiba ni lazima watoke upinzani.

Hakuna mgombea wa uraisi badala ya Shein aliyepata zaidi ya 10%
Na hakuna chama zaidi ya CCM kilichopata viti zaidi ya 10%
kwa maana hiyo no makamu wa raisi
 
Wahenga walisema" lishalovuusha si dau"na ukimfadhili punda shukran yake mateke" ndugu Ndugu hamad rashid CCM hawawezi kukulipa fadhila.

Hamad akisikika kuhojiwa na kituo kimoja cha radio "cocnut FM" ambapo alidai kua pamoja na kutofikia alau asilimia 10 ama imani katika nafasi 10 za Rais basi atatumia busara yake ili kuteua wawakilishi wa vyama vilisho shiriki uchaguzi .Bwana Hamad amedai wamekisaidia na kuunga mkono juhudi za serikali kufanikisha uchaguz .Kwa mana nyengine bw.Hamad anataka kulipwa fadhila.Bwana Hamad pia amedai bila ya upinzani hakuna serikali ya National Unity ambapo itakua kuna mgogoro wa kikatiba.

Napenda kumuelewesha kua Hata Rais akifanya uteuzi wa chama cha Hamad kwa viti vyote 10 katiba hairuhusu kumpa nafasi ya makamo wa kwanza wa Rasi .Labda CCM watumie nguvu kama walivyozoea .
Chengine CCM hii serikali ya umoja wa kitaifa hawaikubali na hawamkubali muasisi wake Dr karume.

Kwanini nafasi za uteuzi haziwezi kuhalalisha makamo wa Rais na kuzima ndoto za Bwana Hamad Rashid???
Katiba ya zanzibar 1984 toleo 2010

38(3)(ii)
"Endapo rais atakua hana mpinzani basi nafasi ya makamo wa kwanza wa rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya majimbo katika baraza la wawakilishi"

Kwa muktadha huo wingi wa viti vya majimbo mana yake si wabunge wakuteuliwa .Ni lazima iwe na majimbo ya kuchaguliwa na wananchi
Huyu naye!! Si wampe anachoomba tu.
 
unajua bhana , maandiko matakatifu yameweka wazi sana kuhusu ukubwa wa laana ya usaliti , huyu hamad rashid atapatwa na balaa kubwa sana .
 
Afadhar umemwambia maana mimi hawa vijana wa form four huwa wananikera sana wanapotumia x badala ya s. Sijui ushamba wa wapi huu. Na watu wazima wameanza kuiga
Mkuu point nzur saaana ila sasa hizi X usizitumie tena zinakushushia heshima
 
Mkuu naomba ulete tafsiri halisi ya hichi 39(i)(ii)
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika
matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini
ya asilimia kumi (10%) ya kura zote za Uchaguzi wa
Rais, au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani,
basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote
cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika
Baraza la Wawakilishi.

HR hakupata asilimia 10% mustakbali wake upoje?
Sasa hakuna chama pinzan kilopata 10% wala kilopata jimbo la uwakilishi hapo pakoje
 
Watu wanasikia kichefuchefu wakiona kifungu hiki, kila anayekuja anakataka pale anapoona panamfurahisha yeye lakini ukweli kifungu kinasomeka hivi;

39(i)(ii)
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10%) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais,
au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

Ndio maana Hamad Rashid anachosema, makamu wa rais toka upinzani kwa uchaguzi huu hakuna, bali nusuru ni nafasi mbili za uwakilishi wa baraza katika nafasi kumi za rais za upendeleo sababu kikatiba ni lazima watoke upinzani.
Nafac mbili za uwakilishi za upendeleo co za majimbo
 
T
Kwa maelezo hayo basi ni dhahiri chama cha UPDP ndicho kitakachotoa makamu wa kwanza na sio chama cha ADC cha Ahmad Rashid kwàni chama cha UPDP kimepata mwakilishi mmoja wa kuchaguliwa anaitwa Assad Ahmad hivyo kinakidhi kigezo hicho cha kisheria
Tume ilishatoa ufafanuzi kua mcmamizi wa kituo aalijaza form kimakosa kw hiyo mshindi ni wa ccm
 
Hamad Rashid, Shibuda, Mzee Cheyo, na mzee Mrema wa TLP hao wote wana njaa kama fisi aliyetoka kujifungua, lazima wale watoto wao kukidhi njaa zao
 
Baada ya kushiriki uchaguz wa maigizo akitegemea kupata japo ile 10% ya kura za urais .
akaambulia patupu ila akashika nafas ya pili lakn isiyokidhi wiwango vya makamu wa kwanza wa raisi visiwan humo . Jana alimwandia barua rais Sheni kuulizia vip ndugu yangu mbona hunipi hicho cheo?? Si nimeshika nafasi ya pili?? Sijapata majibu aliyopewa na Sheni je kapewa huo uongozi au katoswa mazima??
Leo ndio mwisho kikatiba naweza kuwa binafsi sijajua nan makamu wa kwanza nchini humo anaweza kuwa yeye au mwingine.

Wenye taarifa walete hapa mm nilikua nazo za kuomba tu kupewa upendeleo!
 
Nasikia harufu ya uongo kwenye uzi huu
 
HRM atapewa uwaziri, takwa la asilimia 10 ili mtu ateuliwe makomo wa 1 wa rais ni takwa la kikatiba, this time ZNZ haitakuwa na makamo wa 1. Ila kwenye uteuzi wa mawaziri Shein anaweza kumteua yoytote hivyo HRM atapata.
Pasco
 
Back
Top Bottom