DOKEZO KERO Halmashauri ya Buchosa toeni mikopo kwa Vikundi vilivyojisajili, mbona mmeishia kutoa kwa Viongozi wenu tu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna tatizo kwa Vikundi katika Halmashauri ya Buchosa vina malalamiko kuhusu ile mikopo ya Asilimia 10 kwa vijana, kuna vikundi vimeomba mkopo tangu Julai 2024, hela zilitoka na zikaenda kwa Viongozi wa juu wa Halmashauri lakini upande wa pili wameshindwa kutoa mikopo hiyo kwa vikundi husika.

Inasikitisha na inauma kuona hela nyingi za mikopo zikienda kwenye mifuko ya Viongozi hao licha ya wananchi kutumia gharama kubwa kusajili vikundi ili kupata mikopo.
 
Back
Top Bottom