Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 256
- 458
Hali ya Soko la Ndizi Mabibo ni mbaya mamlaka ziwajibike kwa kufumbia macho kero ya Wananchi.
Hali Soko la Mabibo maarufu kama soko la ndizi inasikitisha hasa kipindi hiki ambacho mvua inaendelea kunyesha kwa mfululizo, karibia kila kona kwenye soko hilo ni tope tope, katika hali ya kushangaza kuna bidhaa zanapangwa chini kwenye matope ambayo yamechanganyika na taka nyingine zinazotokana na shughuli zinazoendelea sokoni hapo.
Hali hii ikiendelea hivi kuna hatari kubwa ya watu kupata magonjwa ya mlipuko ingali yanaweza kuzuilika kama wahusika na mamlaka zitawajibika ipasavyo kuchukua hatua dharura pamoja hatua za muda mrefu kuliweka soko hilo kwenye mazingira rafiki.
Sio mara ya kwanza hapa jukwaani kuletwa andiko la aina hii, lakini nashangaa kama mamlaka zimeshindwa kuweka hata miundombinu ya dharura kuwezesha shughuli nyingine kuendelea huku mipango ya muda mrefu ikiendelea.
Kwa sasa ukienda sokoni hapo unachotangulia kuchukua ni kukodi buti za kuvaa kinyume na hivyo jiandae kukabiliana na tope, unaweza kujiuliza soko hili kama linatengeza mapato, kwanini mamlaka kwa siku zote haziwajibiki ipasavyo kuweka miundombinu rafiki ya soko hili, au tunangojea magonjwa ya mlipuko yatokee kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo ndio tushikane uchawi.
Najiuliza wahusika wameshindwa hata kumwaga vifusi hata kwenye maeneo korofi mfano kwenye njia (mlango) za kuingilia sokoni hususani upande unaouza ndizi na matunda, wahusika wanaosimamia maeneo hayo wanatakiwa kuwajibika kuna mambo mengine yangesaidia kuondoa kero kama mamlaka za chini ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilipo soko hilo kuwajibika.
Pia soma:
- DOKEZO - Serikali ina mpango gani na Afya za Wananchi wanaotumia Soko la Mabibo? Watu wanalishwa uchafu pale
- Wafanyabiashara Soko la Ndizi Mabibo: Rais Samia tunaomba tusaidie tupate hati ili soko lijengwe
- Dar: RC Chalamila amevunja Uongozi wa Soko la Mabibo na kukabidhi kwa Manispaa ya Ubungo
- Dar: Milioni 600 zatengwa kukarabati soko la Mabibo