The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 365
- 713
Wanafunzi hasa chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM mpaka sasa hawajapata stahiki ya fedha za kujikimu ijulikanayo kama "boom" mpaka sasa ilihali hali fedha hizo zilitakiwa kulipwa tangu tarehe 23 mwezi mei.
Ukipitia account za SIPA za wanafunzi zinaongesha fedha ziliwekwa tangu mei 13 lakini mpaka sasa wanafunzi waliopata stahiki zao ni waliosajiliwa kwa mfumo wa Didis na wanaotumia account za benki za NMB pekee.
Wanafunzi wanaotumia benki ya CRDB mpaka sasa hawajapata fedha zao na hakuna dalili ya kupata fedha hizo licha ya taarifa kwa umma iliyotolewa na bodi ya mikopo kuwa wanafunzi watapata fedha zao kuanzi jumatatu ya wiki hii.
Changamoto hiyo imepelekea wanafunzi kukosa utulivu katika masomo yao kwa sababu ya kukosa mahitaji ya msingi kutokana na fedha zao ambazo ni haki yao ya msingi.
Kucheleweshwa kwa fedha hizo za kujikimu kwa wanafunzi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mamlaka husika zinapaswa kuwajibika kwa kulipa fidia kwa muda ambao fedha hizo zimecheleweshwa kwani huwasababishia wanafunzi kukopa fedha zinazolipwa kwa riba hivyo kusababisha msongo wa mawazo mkubwa.