Poleni na majukumu wana-JamiiForum. Ni imani yangu wote mpo salama. Kama kuna anayepitia changamoto Mungu awe faraja kwako.
Nimekuwa mfatiliaji wa kipindi cha 'Ushauri wako' kinachorushwa saa 2-3 asubuhi siku ya Jumapili Radio Free Africa. Kwenye hiki kipindi huwa wanahojiwa wahitaji mbalimbali ila mara nyingi huwa ni wagonjwa wanaohitaji msaada wa matibabu. Kiukweli watu wanapitia magumu sana.
Nimegundua yafuatayo kwenye hiki kipindi cha ushauri wako:
Ushauri
Ni hayo tu muwe na Jumapili njema.
...............................................................................
Mariam Abdalah Ramadhani 0748576466/ 0657399861 amehojiwa leo kwenye kipindi cha ushauri wako RFA. Alifanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua mwaka 2015, baada ya miezi 3 kizazi kilioza kikatolewa. Baadae akapata uvimbe kwenye kibofu cha mkojo akafanyiwa upasuaji. Tatizo kwenye kibofu cha mkojo limerudi tena anapitia maumivu makali. Anahitaji msaada wako. Unaweza kuongea naye kupitia hizo namba hapo juu.

- Baadhi ya wanaume wanatelekeza familia(mke/watoto) zao wakati wa ugonjwa hasa magonjwa ya muda mrefu. Pia na wanawake wanafanya hivyo ingawa ni kwa uchache ukilinganisha na wanaume.
- Baadhi ya wanaume wanakimbia familia zao baada ya kupata watoto wenye ulemavu.
- Upendo umepungua kwenye baadhi ya familia zetu. Mfano kama baba ametangulia mbele za haki. Upande wa baba huwa hawana msaada kwa familia iliyoachwa na ndugu yao.
Ushauri
- Naomba wanajamii forum tuwe tabasamu na faraja kwa wahitaji katika magumu yao. Unaweza kuona umefanya kidogo lakini ni kikubwa kwa anayepokea.
- Wanaume jitahidini kuwajengea uwezo wake zenu katika misingi ya kusamamia familia.
- Wawezeshe wake zenu wajue kujitafutia ata husipokuwepo itakuwa rahisi kuendeleza vilivyobaki kama vipo au kutafuta kwa ajili ya familia.
- Tenga muda muda wakusikiliza vipindi kwa ajili ya wahitaji utapata kitu. Au kama huna muda wa kusiliza redio tembelea vituo vya watoto yatima utafarijika na utawiwa ndani ya moyo wako kufanya jambo kwa ajili yao.