Haki za Msingi za Wanawake na Haki zisizo za Wanawake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,095
62,787
HAKI ZA MSINGI ZA MWANAMKE NA HAKI ZISIZO ZA WANAWAKE

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwa mujibu wa mtazamo wangu na ambao ninajiamini; ni hakika, Hapa sitauma Una maneno, sitaficha chochote, nitataja Kwa haki kabisa.

Zifuatazo ndizo Haki za msingi za wanawake;

1. Haki ya Kuishi
Kama binadamu wengine na viumbe wengine mwanamke anayohaki ya kuishi.
Hii ndio haki namba moja kabisa ya mwanamke na mwadamu yeyote Yule.

2. Haki ya KUPENDWA
Mwanamke anahaki ya kupendwa kivyovyote vile, na hapa nazungumzia kuthaminiwa, kujaliwa, kutunzwa, kupendelewa, kupewa kipaombele n.k.

Hiyo namba mbili ambayo wanawake wapaswa. Mwanamke awapo Kwa wazazi wake lazima mzazi ampende mtoto wa kike na kumpendelea zaidi kuliko wa kiume hiyo ni Haki ya Mwanamke. Upendeleo ninaoutaja hapa ni ule wa kumlinda, kumfurahisha binti wa kike, kumjali, na kumuandaa kuwa Mama Bora.

Akishaolewa, Mwanamke sharti apendwe, kanuni muhimu na yalazima ni kumpenda Mke wako. Kumthamini Kwa kila haki zake azitakazo ikiwemo kutunzwa, kulindwa na kupewa kipaombele.

KUPENDWA ni Haki ya msingi kabisa ambayo mwanamke anayohaki kuidai, na anastahili kupewa Kwa vile ni Haki yake.

3. KULINDWA
Mwanamke anayohaki ya KULINDWA, ulinzi wa mwanamke lazima uwe mkubwa zaidi kuliko ulinzi wa mwanaume, hiyo ni Haki Yao.

Iwe yupo Kwa wazazi au Kwa mume wake. Mwanamke anayohaki ya KULINDWA Kwa sababu zifuatazo;

I) wathamani Mwanamke ni kiumbe cha thamani Sana kuliko kiumbe chochote Duniani.
Wanawake ni mapambo ya Dunia, ni zaidi ya Vito vya thamani, kulindwa ni Haki Yao.

Ii) Rahisi kulaghaiwa/kuibwa/kubadilika
Mwanamke kiasili ni kiumbe asiye na muono wa mbali, asiyeyatafakari mambo ya miaka kumi ijayo, unajua ni Kwa nini?
Jibu ni kuwa, mwanamke sio kwamba Hana uwezo wa kuona mbali, Hasha! Isipokuwa kiasili akili zao hazitaki kuulizwa/hawapendi kuumiza ubongo katika kufikiria mambo magumu. Kuona mbali inapaswa uumize ubongo. Ndio maana ni rahisi kudanganywa, kupotoshwa, kuamini Kwa upesi pasipo kufikiria. Hii ni moja ya sababu ya Kwa nini mwanamke analindwa kuliko mwanaume.
Ndio maana kuna baadhi ya taasisi nyeti mfanyakazi wa jinsia ya kike haruhusiwi kuolewa na mtu wa nje ya taasisi au fani hiyo.

iii) Mwanamke ni kiwanda
Mwanamke analindwa Kwa sababu yeye ni kiwanda cha kuongeza watu Duniani, ni sehemu ya Mradi muhimu wa uumbaji katika Dunia.
Mwanamke analindwa hasa mwanamke aliyetunzwa akawa na sifa za mwanamke haswa, kusudi apate mwanaume Bora Kwa maslahi mapana ya jamii na taifa.
Mwanamke ni kiwanda cha kuzalisha malezi, ndio maana anapaswa kulindwa na kupewa ulinzi mkali ili asijezalisha Matoto ya hovyo Kwa kushindwa kuyalea.

Siku zote malezi yanatoka Kwa Mama dunia ingalipo.
Ndio maana Sheria nyingi zinaonekana kumgusa zaidi mwanamke kuliko mwanaume ambazo kizazi cha sasa Kwa upuuzi wao wanasema ni sheria kandamizi.
Lengo la sheria hizo ni kulinda kiwanda kinachozalisha watu Duniani,

Mwanamke asipolindwa basi ujue jamii haipo salama, Matoto na kizazi hiko lazima kiwe hatarini.
Jamii zenye sheria Kali Kwa wanawake zimeendelea kudumu katika maadili Mema na tabia njema. Zipo salama kabisa.

IV) Maumbile Yake
Maumbile ya mwanamke yanavutia na mazuri, Hilo ni Jambo la Kwanza, lapili; Maumbile ya mwanamke ni rahisi kuharibika. Mara nyingi vitu vizuri huharibika haraka hasahasa visipopewa ulinzi wa kutosha.

Mtoto wa kike lazima awekewe sheria Kali kulinda maumbile yake yasiharibike Kwa haraka. Mtoto wa kike asipopewa ulinzi Imara akaachwa akue Kama bidhaa isiyo ya thamani hujikuta akiharibika kimaumbile mapema hata kabla hajafikisha miaka 20.

Unakuta binti mdogo miaka 20 haijui lakini keshachakaa, ziwa limeshalala na halitamaniki tena,
Hii ni Kwa sababu hakulindwa vizuri, jamii yake haimthamini na imeshindwa kulinda haki zake.
Hata hivyo nafahamu kuwa wapo mabinti ambapo Genetic zao za kurithi huwapelekea kuchoka mapema. Lakini hawa ni wachache.

Uzuri na mvuto wa mwanamke wakati mwingine hupelekea akapata madhara ya kubakwa ndio maana lazima alindwe, na moja ya namna ya kumlinda ni kumuwekea sheria Kali ikiwemo muda wa kuwa nje ya nyumba isizidi saa kumi na mbili jioni, kutoka atoke Kwa taarifa ikiwezekana apewe mtu wa kumsindikiza, mavazi yake sharti yazingatiwe na yadhibitiwe, mahali anapoenda sharti kuwe na maadili.

Hiyo nikiwa Mwanamke awaye yeyote awe mkubwa au mdogo,
Akiwa chini ya wazazi au chini ya Mume wake lazima alindwe.

Kama hatapewa haki ya Ulinzi nini kitatokea;
1. Atazalishwa kabla ya ndoa, atakuwa single Mother
2. Atapelekea mtoto kukosa malezi ya Wazazi wawili Kwa uzembe.
3. Kama atakuwa ameolewa basi atapewa talaaka na ndoa kuvunjika kisa Usaliti wa mapenzi.
4. Atakuwa single mama na ataleta usumbufu usio WA lazima kutaka kugawana mali.
5. Anaweza kuleta mtoto haramu kwenye ndoa halali.

Mwanamke ulinzi ni Haki yake hilo ndilo anapaswa alipiganie. Sio apiganie haki za kuachana sijui talaka, wakati talaka Kwa sehemu kubwa ni matokeo ya kukosa haki ya KULINDWA na KUPENDWA

4. KUELIMISHWA
Mwanamke anayohaki ya kupewa elimu ili imsaidie katika Mazingira anayoishi. Elimu hiyo aitumie Kama Mwanamke kuisaidia familia yake.
Elimu za msingi anazopaswa kupewa Mwanamke;

I) Elimu ya Dini
Hii atafundishwa kumjua Mungu ili aweze kujitambua.
Mwanamke asiye na elimu ya Mungu kamwe hawezi kujitambua, hii ipo pia hata Kwa wanaume. Mtu hawezi kujitambua Kama Hana elimu ya MUNGU.
Ukiona mtu anajitambua basi lazima awe anaelimu ya MUNGU.
Elimu ya Mungu ndio inamfanya binadamu awe mtu, elimu ya Mungu ndio utu wa Binadamu.

Ni wajibu wa mzazi kumpa elimu ya Mungu mtoto wa kike ili ajitambue, Ajue nafasi ya Mungu, mzazi, Mume wake mtarajiwa, na jamii/watu wengine.

Mwanamke asipopewa elimu ya Mungu, sio ajabu ukamkuta anatembea uchi huko mitaani, unakuta mwanamke anatembea uchi utadhani Mbwa, tena Bora mbwa Anamkia huwaga wanaziba nyuchi zao.

Au unakuta mwanamke anabadilisha Wanaume pasipo kujua yeye ni wathamani kuliko anavyojichukulia. Kitu cha thamani hakiwi cha wengi, kinakuwa cha mtu mmoja, hiyo yote ni matokeo ya kukosa haki ya elimu hasa ya Dini.

Mwanamke akishaolewa, mume wake ndio anaowajibu wa kumuelimisha kuhusu Mungu.
Mwanamke nataka kukuambia unayohaki ya kudai kufundishwa elimu ya Dini na Mumeo.
Kama mumeo hajui elimu ya Mungu basi huyo hakufai, mwanaume asiyejua elimu ya Mungu atakufanya udharaulike upende usipende. Pengine nikaonekana naongea mambo yasiyo na macho lakini wenye akili wanaweza kunielewa.

ii) Elimu ya Duniani
Elimu ya Duniani zipo nyingi kidogo, mwanamke anayohaki ya kupewa elimu ya Dunia ambayo haitaathiri uanamke wake, na hapa nazungumzia thamani yake Ile Ile aliyoimbwa nayo.
Mwanamke afundishwe Usafi wake, Usafi wa Mazingira, Upishi, urembo, mapozi na miteho ya kumfurahisha mume wake,

Mwanamke afundishwe bajeti, na kuweka Akiba kwani zipo siku mume wake atakosa au inaweza kutokea dharura.

Mwanamke Kama upo uwezo apelekwe akasome taaluma Kama ualimu, udaktari, uhasibu, injinia Kwa sharti la kutoathiri wajibu wake wa malezi Kwa watoto atakaowazaa.
Ikiwa kazi itaathiri malezi ya watoto wake ni Bora aibadili kazi hiyo.

Kwani kusudi la mwanamke sio kufanya kazi, yaani huo sio wajibu wake, huo ni wajibu wa mwanaume.

Narudia ili nieleweke; Ikiwa kazi aifanyayo mwanamke itaathiri malezi Kwa watoto wake basi Hana budi kuiacha kazi hiyo.

Athari hizo ni Kama kukosa muda wa kukaa na watoto na kuwafundisha tabia na maadili Mema, na kuiandaa Familia iwe tayari Baba akirudi nyumbani.

Angalau Kwa siku Mama awe na muda wa masaa yasiyopungua matano ya kukaa na Familia. Tafsiri yake ni ipi, Kama anafanya kazi basi kazi hiyo iwe kuanzia asubuhi mpaka saa kumi jioni ili awe nyumbani.

Mwanamke afundishwe kufanya maamuzi magumu Kama Mwanaume, ili siku mumewe asipokuwa awe na uwezo wa kuiendesha Familia katika njia nzuri.

Mwanamke apewe elimu ya kujitegemea ili Ile haki yake ya kuwa Msaidizi Kwa Mumewe iweze kutenda kazi vyema. Asiwetegemezi labda Katika mazingira maalumu Kama kuumwa au kuwa mlemavu.

5. HAKI YA KUTUNZWA
Mwanamke anayohaki ya KUTUNZWA Kama ishara ya kuthaminiwa, kupendwa na kujaliwa.
Kutunzwa Kwa chakula, mavazi, urembo, malazi n.k.
Mwanamke kabla hajaolewa anayohaki ya KUTUNZWA na wazazi wake.
Na atakaoolewa Mumewe ndiye mwenye haki hiyo.
Sio haki wala ruhusa kumtunza mwanamke ambaye hujamuoa, kufanya hivyo huleta madhara zaidi katika jamii.

Madhara ya mwanamke kutunzwa na Mwanaume ambaye hajamuoa;
1. Kuchelewa Kwa ndoa kufungwa au kutokuolewa kabisa.
2. Uzinzi na zinaa
3. Magonjwa ya zinaa
4. Mimba zisizotarajiwa
5 single Mothers kuongezeka
6. Kutapeliana.
Unaweza kumhudumia mwanamke ambaye hujamuoa ukitazamia utamuoa kumbe yeye yupo na wewe Kwa sababu ya Huduma zako. Mwisho unakuja kugundua hakupendi unapata madhara ya kihisia, kiakili na kimwili au hata kudhuru watu.
Pia Mwanamke unaweza kuwa unampenda anayekuhudumia ukitazamia atakuoa kumbe mwenzako kukuhudumia kwake sio shida Kwa sababu anakipato kizuri. Mwisho unaachwa unapata madhara au kuleta madhara.

6. Haki ya Kuabudu
Mwanamke anayohaki ya Kuabudu kulingana na wazazi wake wanachoamini,
Lakini akishaolewa anayohaki ya Kuabudu kulingana na Imani ya mume wake.
Ni Haki ya Mwanamke kumfuata mwanaume na wala sio kinyume chake.

Wanawake mnapaswa mjue kuwa haki zako zinatoka Kwa Mzazi au Kwa mume kutegemeana na Ulipo. Ukiwa Kwa Mzazi haki zako zinatoka Kwa Mzazi, na ukiwa Kwa mume haki zako zinatoka Kwa Mume.

Kama Mwanamke unaamini katika Ukristo basi olewa kwenye Ukristo, na Kama unaamini kwenye uislam basi olewa kwenye uislam.

Sio uwe unaamini kwenye Ukristo alafu utake kuolewa na Muislam ili uje umpelekee shida kijana wa watu, hakuna kutetea haki zako za Kuabudu Kwa Wakristo wakati wewe ni Muislam,au kutetea haki zako za uislam Kwa Wakristo hapo huna haki isipokuwa unaleta ushenzi na ushetani tuu.

Kama unataka uwe Mkristo maisha yako yote, basi tafuta Mkristo mwenzako ambaye naye anataka kuwa Mkristo maisha yake yote. Halikadhalika na Kwa dini zingine.

Ikitokea mmoja wenu amebadili Imani katikati, labda ni mwanaume ndio kabadili, basi mwanamke unayohaki ya kupinga msimamo wake kukubadilisha ikiwa utaona hutaki.
Ulishabadili mara ya Kwanza huna haja ya kubadili tena.

Kingine, Kama Mwanaume mpaka anakuoa hajakua Imani atakayozikwa nayo yaani atakayoiamini mpaka kufa basi jua hukupata mwanaume Sahihi.
Mwanaume sahihi ni Yule kabla hajakuoa ameshaamini katika Mungu Fulani kuwa atamuamini huyo mpaka kifo.

Ikiwa ameweza kumbadilisha Mungu aliyekuwa akimuamini kabla hajakupata, kisha akakupata na kukuoa, basi kaa ukijua kuwa IPO siku anaweza kupata mwanamke mwingine akaubadili moyo wake.
Nguvu ya Mapenzi na Imani mara nyingi vinalingana.

7. MWANAMKE ANAYOHAKI YA KUOLEWA
Hii ni moja ya Haki kubwa Sana Kwa mwanamke.
Haki hii humfaharisha mwanamke na kumpa utukufu.
Haki hii imegawanyika katika visehemu ambavyo ni vimichakato Kama ifuatavyo;
I) Mwanamke anahaki ya kutongozwa.
Iwe yupo Kwa wazazi au hata Kwa mume wake.
Ni Haki ya Mwanamke kutongozwa kwani ni ishara kuwa bado anavutia, mi mzuri na bado niwathamani.
Mwanamke asipotongozwa sio ishara nzuri, na akijigeuza kutongoza hapo atakuwa anajishushia thamani yake.

ii) mwanamke ni Haki yake kuchumbiwa wa kufuata itifaki.
Baada ya kutongozwa na wengi anayohaki kuchagua, akishamchagua kinachofuata mi taratibu za posa na mahari.
Mwanamke ni Haki yake kupewa mahari.

iii) Ni Haki ya Mwanamke Kuolewa.
Baada ya kuchumbiwa anayohaki ya kuolewa ili apate Haki zingine Kama kutunzwa na mumewe, kuzaa, kuridhishwa kimwili/kingono N.k.

Kuolewa Kwa mwanamke ni moja ya Haki yake ya msingi sana.
Hii itamfanya uzuri wake kuthibitika, uzuri wa tabia, elimu aliyopewa na wazazi wake ya kuchagua mwenza Bora maisha yake, na uzuri wa kuijenga jamii.

MWANAMKE anayohaki kuona aolewe mmoja au awe na Mke mwenza kulingana na sababu kuu tatu;
1. Kama ataona yeye ni mgonjwa na anashindwa kumhudumia mumewe.
2. Kama mumewe atakuwa na nguvu za Libido za kuhitaji kila siku na yeye Hana uwezo wa kumudu kila siku, anaumia na hakuna uwiano wa kihisia baina yake na mumewe.
Anaweza kumwambia mumewe aongeze mwanamke ili wasaidizane. Hiyo ni Haki yake.

3. Kama atatamani mumewe awe na watoto wa idadi au Aina Fulani alafu yeye Hana uwezo huo.
4. Kama uchumi unaruhusu mumewe kuoa wake wawili na kutunzwa wote wawili pasipo shida

8. URITHI

Mwanamke anayohaki ya kurithi Mali za mumewe ikiwa ameolewa Kwa ndoa Rasmi iwe ya kimila, Kidini au kiserikali au namna yoyote Ile ambayo itazuka huko mbeleni ambayo sasa haipo Ila ilimradi iwe Rasmi inayotambulika.

Mwanamke anayohaki ya kurithi Mali walizochuma pamoja na wasizochuma pamoja endapo mumewe atafariki ikiwa tuu alizaa mtoto na hataolewa na Mwanaume mwingine nje ya ukoo wa mumewe.

Ikiwa atataka kuolewa na Mwanaume mwingine nje ya ukoo wa mwanaume basi mi Haki yake kugawiwa nusu Kwa nusu Mali zote walizochuma na mumewe Enzi wakiwa wote. Na zile ambazo hawajachuma wote sio haki yake kwani atakuwa sio tena mke wa huyo aliyefariki. Bali atakuwa mke WA huyo mwanaume mpya aliyempata.

Mwanamke anayohaki ya kurithi Mali za Mwanaye ambaye hajaoa/hajaolewa.
Pia anayohaki ya kurithi Mali za mtoto wake aliyeoa/aliyeolewa ikiwa mwanaye aliandika wosia na pia ikiwa Mkwe wake atataka kuoa/kuolewa na mtu mwingine.
Hivyo atarithi Mali zile ambazo mwanaye alizichuma mwenyewe kabla hajaoa/hajaolewa.

9. KUZIKWA
Mwanamke anayohaki ya KUZIKWA kulingana na alipokuwepo.
Kama aliolewa Kwa ndoa halali basi mi Haki yake KUZIKWA kulingana na Mila za mume wake. Na ikiwa hakuolewa Kwa ndoa Rasmi basi atazikwa kulingana na Mila za wazazi wake.
Na ikiwa Hana wazazi (katika Mazingira maalumu) na hakuolewa basi atazikwa vile alivyotaka au kulingana na kanisa/msikiti aliokuwa anaaabudia.

Atazikwa Kwa upande wa mume ikiwa aliolewa, na Kama hakuolewa atazikwa Kwa wazazi wake.
Na ikiwa katika Mazingira maalumu basi atazikwa na serikali au mahali anapoabudia.

10. KULEA WATOTO NA KUWAMILIKI
Mwanamke anayohaki ya Kulea watoto wake aliowazaa vile atakavyo pasipo kuvunja thamani yake Kama Mwanamke.
Mwanamke Kwa vile moja ya majukumu yake makuu ya kuwapo Duniani ni Kulea anayohaki ya kukataa mtoto wake asiishi katika Mazingira Fulani yasiyoridhisha.

Ikiwa mwanamke ataachana na mume wake na wana-mtoto basi Mwanamke anayohaki ya kuishi na mtoto kwenye kumi la Kwanza la umri wa mtoto, yaani miaka 0-10. Kisha Baba Kama atamuhitaji huyo mtoto basi atapewa kwani ni Haki yake.
Naye atamlea katika Kumi la pili la umri wa mtoto yaani kuanzia miaka 11- 20
Baada ya hapo mtoto atakuwa ni mtu mwenye kujitambua, ataamua aishi Kwa Baba au Kwa Mama au akajitegemee na maisha yake.

Ikiwa Baba alimtelekezea Mama mtoto, Mama akalea mtoto Kwa kumi la Kwanza na kumi la pili, Basi mtoto huyo atakuwa ni Mali ya Mama,

Ikiwa Mama atafanya Kwa hila kumnyang'anya Baba mtoto Kwa sababu labda anauwezo wa kumlea mtoto mwenyewe, na wakati huo Baba alikuwa anahitaji kumlea mtoto basi Mwanamke hatakuwa na haki ya kummilili huyo mtoto.

Ninaposema kumiliki nazungumzia Mamlaka ya kumuamulia mtoto kuanzia majina yake atakayoitwa akiwa Duniani, wakati WA harusi sherehe ifanywe Chini ya usimamizi WA upande Fulani (mwanamke au mwanaume kutegemeana ana mmiliki wa mtoto), Maziiko, kwamba mtoto Kama ikitokea amekufa azikwe upande upo.

Wakati mwingine tutaandika Haki zisizo za Wanawake ambazo siku hizi wanazigombania. Naona andiko limekuwa refu alafu kuna watu wangu WAVIVU kusoma wasije nitupia maneno.

Ni Yule;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Na unazidi kujikandamiza ngoja uone matokeo yake baada ya miaka 30 mbele najua utafika mana bado umri wako mdogo 27+30=
 
Back
Top Bottom