Haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika mfumo wa kidemokrasia ndani ya CCM

Jul 6, 2024
96
70
Kuchagua na Kuchaguliwa

Ni haki ya kikatiba ya CCM.

Kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kiuraia ya kila Mtanzania mwenye utimamu wa akili, ambayo haiwezi kutungiwa sheria wala kanuni ili kuvizwa.

Nilisikika ndotoni nikimwaga upupu wa neno baada ya kuvuta bangi huko ndotoni, ingawa haiui kama vile sigara zinavyoua na kuikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo la 2005, ukurasa wa 21, ibara ya 14.

Na maelezo haya ya mauaji ni kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na mshauri wa Mheshimiwa Rais aitwaye Professor Janabi, akidai kuwa sigara huwaua watu takriban milioni nane kwa mwaka.

Nikaanza:

Tusome kitabu kilichotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Agosti 2020, kiitwacho Mwelekeo wa Sera za Chama Cha Mapinduzi katika Kipindi cha Mwaka 2020-2030, ukurasa wa 190, ibara ya 143:

Kinatueleza:
"Huwezi kuwa mwana wa nchi ukiwa huna uchungu wa nchi yako.
Ni wajibu wako kuitetea na kuipigania nchi yako.
Huo ndiyo utu na huo ndiyo uzalendo."


— Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

Mwisho wa kunukuu.

Tusome Katiba ya CCM 1977, toleo la 2022, ukurasa wa 10-11, ibara ya 15 yote, pamoja na ibara ya 05(02)(04)(08)(09)(11)(16) kwa msisitizo.

Ukurasa wa 152 wote kwa umuhimu wake

Kipekee, ukurasa wa 05, ibara ya 05 A(04), ikisomwa kwa pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977:

  • Ukurasa wa 60-61, ibara ya 64(5).
  • Ukurasa wa 20-21, ibara ya 12(1)(2), ibara ya 13(1)(4)(5), ibara ya 26(1)(2), ibara ya 09(a, b, f, h).
Hii ni kwa madhumuni ya kulinda Katiba ya CCM 1977, toleo la 2022, ukurasa wa 09-10, ibara ya 14(03), ili itiiwe na kuheshimiwa sambamba na Kitabu cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu, ukurasa wa 125-126, kwa msisitizo wa Katiba ya CCM, ibara ya 05(04).

Ilani ya CCM 2020, ibara ya 110(c).

Tukisoma Katiba ya CCM 1977, toleo la 2022, ukurasa wa 153, kifungu cha 08, kinatupa idhini ya kwenda kusoma Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM na Jumuiya Zake, toleo la 2022, ukurasa wa 02, ibara ya 04, inatueleza:

"Kufuata na kutii Katiba ya CCM na Kanuni zake ni wajibu wa kila mwanachama wa CCM."

Mwisho wa kunukuu.

Ilani ya CCM, ukurasa wa 01, ibara ya 04, na ukurasa wa 161-168, pamoja na ukurasa wa 08, ibara ya 10 na 11, inatusisitiza kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kufuata sheria na kuzitekeleza kwa vitendo.

Mheshimiwa Salum Ally Hapi,
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,

Akiwa Shinyanga, nakumbuka tarehe 23/01/2025, alisema:

"Wala usije ukajidanganya kwamba wewe utakiuka kanuni za chama chetu na maadili ya chama chetu ukawa salama."

Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Toleo la 2005), Ibara ya 60-61, Ibara ya 64(5), Ibara ya 12(1)(2), Ibara ya 13(1)(4)(5), Ibara ya 26(1)(2), na Ibara ya 09(a, b, f, h), tunapaswa kulinda Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 1977, toleo la 2022 (Uk. 09-10, Ibara ya 14(03)).

Katika Ilani ya CCM ya mwaka 2020, Ibara ya 110(c) inasisitiza juu ya kufuata sheria na kuzitekeleza kwa vitendo, badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

Mheshimiwa Salum Ally Hapi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, alipokuwa Shinyanga tarehe 23/01/2025, alisema:

"Wala usije ukajidanganya kwamba wewe utakiuka kanuni za chama chetu na maadili ya chama chetu ukawa salama."
Kitabu cha Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM na Jumuiya zake (Toleo la 2022, Uk. 24-25, Ibara ya 05(a)) kinaeleza kuwa kosa la kikao katika masuala ya maadili linaweza kuwa katika sura mbili:

  1. Sura ya kutenda
  2. Sura ya kuto tenda
Kikao kinachokataa misingi ya imani ya CCM, kuongeza uasi ndani ya chama, au kugomea michango halali ya wanachama kinakuwa na kosa la uasi na kinastahili adhabu kulingana na kosa husika.

Katiba ya CCM (Uk. 01, Ibara ya 04(01)(02)) inasisitiza imani ya chama kwamba:

  • Binadamu wote ni sawa.
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977, Toleo la 2005, Uk. 20, Ibara ya 12(1)(2)) inasema:
"Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake."

Sheria ya mwaka 1984 namba 15, Ibara ya 06, inahimiza usawa wa binadamu.

Kitabu cha Sera za Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha mwaka 2020-2030 (Uk. 74-75, Ibara ya 52(c), Uk. 76-77, Ibara ya 53(b), Uk. 197, Ibara ya 147, Uk. 118, Ibara ya 100) kinasisitiza kuwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa haipaswi kuwekewa vizuizi kwa njia ya kanuni zisizo halali.

Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM na Jumuiya zake (Toleo la 2022, Uk. 34) zinaeleza kuwa chama kinapaswa kuendeshwa kwa misingi ya demokrasia katika kila ngazi. Mwanachama wa CCM anapaswa kuachwa ajaze fomu ya kuomba uongozi, na hatma yake iamuliwe na wanachama walio wengi, si vikao kumkata kabla ya kufikia wananchi.

Mwanachama anayependa kuomba uongozi na asipopewa fursa ya kujaza fomu ni ukiukwaji wa kanuni za chama (Toleo la 2022, Uk. 20, Ibara ya 04(a)(b), Uk. 17, Ibara ya 05(1)(2)).

Kitabu cha Awamu ya Tatu ya Mradi wa Kukiimarisha Chama (Uk. 07) na Ujamaa: Essays on Socialism cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Uk. 13-15) vinahimiza tafakuri juu ya haki za kila mwanachama.


Katiba ya CCM (1977, Toleo la 2022, Ibara ya 14(03), Uk. 09) inasema kuwa mwanachama ana haki ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi wake kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, na Taratibu za CCM.

Mwongozo wa CCM wa 1981 (Uk. 138-139, Ibara ya 159, Uk. 104, Ibara ya 110) unasisitiza nidhamu ya kweli ndani ya CCM na nchi kwa kuhakikisha kila mwanachama na kila Mtanzania anatii Katiba, Kanuni, Miongozo, na Taratibu za kimfumo, huku upendeleo na vitendo vya ubaguzi vikikataliwa.

Kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM na Jumuiya zake (Toleo la 2022, Uk. 34), demokrasia inapaswa kuwa msingi wa nidhamu ndani ya chama.

Katiba ya CCM (Uk. 153, Kifungu cha 14) inatupa uhalali wa kusoma Kanuni za Tume ya Uthibiti na Nidhamu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Uk. 11, Ibara ya 13B), inayosema:

"Nidhamu ni amri, ama ya kujiamrisha mwenyewe kwa kuelewa na kukubali maana na umuhimu wa hilo unalolitenda, ama ya kuelekezwa na wengine iwapo wewe ni mzito wa kufanya hivyo mwenyewe."


Maneno ya Waasisi na Viongozi wa Chama

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema:

"Madhali wewe ni raia wa Tanzania, huna kichaa, hauko gerezani, na umetimiza umri wa miaka 18, basi una haki ya kupiga na kupigiwa kura. Haki hii haiwezi kufutwa na mtu yeyote."

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tarehe 18/01/2025, alisema:
"Naomba nimpe nafasi Comrade Kinana, naye ana neno la kutuambia. Karibu sana."

Mheshimiwa Abdulrahman Omar Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, akiwa Serengeti, Mara, tarehe 14/04/2024, alisema:

"Chama chetu kinaendeshwa kwa utaratibu. Tuna Katiba, Kanuni za Uchaguzi, Kanuni za Uteuzi wa Vyombo vya Dola, na Kanuni za Maadili. Kila kitu kimeandaliwa. Ukiona mtu anafanya mambo visivyo, ujue hayo ni yake."

Dkt. Samia Suluhu Hassan pia aliongeza:
"Comrade Kinana ni mmoja wa makada watiifu wa CCM na mwenye uzalendo usiotiliwa shaka kwa nchi yake."

Kutunga kanuni zinazoviza haki za wananchi ni kwenda kinyume na Katiba ya CCM, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Tukiheshimu maandiko ya CCM, tutakuwa tumetenda haki kwa mujibu wa Katiba na Sheria. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977, Toleo la 2005, Ibara ya 64(5)) inasema:

"Katiba hii itakuwa na nguvu ya kisheria katika Jamhuri nzima ya Muungano. Endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti ya Katiba hii, basi Katiba ndiyo itakayoshika nguvu, na sheria hiyo nyingine itakuwa batili."

Kwa msingi huo, kidumu Chama Cha Mapinduzi!
 
Back
Top Bottom