Haiwezekani kumrudisha Kiboko ya Wachawi nchini Tanzania na kumfungulia mashitaka?

Kosa sio sadaka kosa laweza kuwa,
1. Wizi wa kuaminika
2. Kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu
3. Kudhihaki dini
4. Utakatishaji fedha
5. ...
Wataendeleza watu wa NPS.

Watu wametulia ukute hakuna hata jalada la uchunguzi 😂😂 wakiulizwa watasema hakuna aliyekuja kulalamika.
Mkuu,amedhalilisha nini?Mlalamikaji ni nani?Itakuwa ni JINAI au ni MADAI?
 
Mimi naona watz ndiyo wajinga.Hivi utakubalije kutoa milioni Moja au laki Tano ili uombewe na mchungaji?Huo ni ujinga.kwa Nini usimuombe Mungu wewe mwenyewe?
 
Mkuu,amedhalilisha nini?Mlalamikaji ni nani?Itakuwa ni JINAI au ni MADAI?
sio lazima siku zote kesi ianzishwe na mlalamikaji. jinai inaweza inaanzisha na hawa wafuatao, jua hilo kuanzia leo;

1. mlalamikaji
2. Polisi wenyewe wamehisi kuna jinai wanafungua jalada la uchunguzi, watachunguza wakithibitisha wanakupeleka kwa dpp akushitaki.

3. DPP mwenyewe chini ya mamlaka ya sheria ya mashtaka, akiona kuna harufu ya jinai fulani, na polisi hawajaanzisha uchunguzi, amepewa mamlaka kuwapa maelekezo wapeleleze kitu hicho na wamletee majibu kwenye jalada. watakachofanya polisi ni kufungua jalada la uchunguzi kuchunguza alichoelekeza DPP, kama uchunguzi utakuwa positive, mtu anapelekwa mahakamani,kama uchunguzi hautakuwa positive basi jambo limeishia hapo.

wengi chuoni wanafundishwa kuwa hakuna kesi inafunguliwa bila complainant, ni kwasababu waalimu wengi wa chuo wanajua theories hawajui practice. na wanafunzi wanawalisha hicho hicho walicho nacho. and they don't update themselves na sheria mpya au zile zilizopo.
 
Back
Top Bottom