Haijalishi Mtu wa Dini au Mpagani, Mtu asiye mwaminifu Hana mwisho mzuri ktk kila jambo

Kuna bosi mmoja amewahi kufukuzwa kazi na kuacha mshahara wa mamillioni kwa kosa la kutokuwa mwaminifu na ghalama ya kosa lililopelekea kufukuzwa ni chini ya millioni.
Mkuu watu wanakera saana. Mara nyingi huwa najisemea laiti binadamu wangekuwa kama nilivyo mimi aseeh dunia ingekuwa safe saana.

Huyo jamaa alikuwa na familia kabisa. Mnafanya kazi unampa usd 1000 ambayo ni pesa ndogo hata ukimtapeli mtu hununui kitu cha maana. Akahamisha familia alipokuwa anapanga akaondoka.
 
Kuna jukumu utakuwa unalikwepa mkuu kwa kuamua kujichimbia kwenye wizi wa kodi za wananchi masikini kama mbadala.
hawa wananchi usipo waibia badae wañakunanga na kuona huna maana, hata kizazi chako kitakuja laumu ulipata nafasi ukashindwa iba ili na wao wapate raha (rejea baba wa taifa).

jamii nayo inawapa credit wezi na kuona ni watu wenye heshima bila kujali kama wamewaibia ama laah

pesa ya kuwaibia wananchi kupitia serikali haina lawana ya moja kwa moja wala manung'uniko ya mtu kukufanya ukose furaha.
 
kila mtu akiishi huo mtazamo wako kuanzia sasa, nchi itafirisika na kufungwa rasmi leo jioni
 
Kuna baadhi ya vitu vinapita katikati ya Dini na upagani na vinamilikiwa pande zote.

Mwizi au fisadi hata awe na mamillioni mangapi maisha yake yanautofauti mkubwa na mtu mwaminifu anaejitambua hata kama anaishi chini ya dola moja.

Watu waongowaongo mara nyingi wanaishi maisha ya kutangatanga na hata akifanikiwa hafurahii maisha katika ukamilifu wake.

Matapeli mara nyingi hata kama akitapeli Trillion wanaishia kuishi maisha ya kungaunga na wasiwasi.

Watu wasio waaminifu kwenye mahusiano wengi wanaishi maisha yaliyo chini ya kiwango. Anakuwa na Furaha za Muda mfupi na maisha yanazungukwa na matatizo mengi yakujiongezea.

Watu wasio waaminifu kwenye Ajira zao, Shuguli zao za kila siku hara kama wakifanikiwa kupitia kutegea,Kudokoa uwezo wa kutunza hayo mafanikio na kuyafurahia mara nyingi ni wa chini. Furaha aliyonayo iko hatarini kukata muda wowote akibainika,

Uaminifu Uaminifu Uaminifu
Yaani this is the best thread ever. I belive wengi wataisoma na kuizingatia. Wengi tumeathirika kwa kutokuzingatia uliyoandika ndio maana malalamiko meeengi! Turudi tulikotoka kuzingatia maadali kwani yana long term impact!
 
Uko sahihi kabisa lakini siyo kwa mtu mweusi na serikali za afrika, maana wengi wameumia sana mwisho wa siku kwa kuwa waaminifu.
 
naamini wengi wapo kwenye mtizamo huu, ndo maana maendeleo hakuna Tanzani-africa

usipo iba jamii pia inakucheka
Na mtu athubutu kabisa kuandika! Hawajui kuwa uaminifu ni mtaji mkubwa sana kuliko kitu chochte. Nijitolee mfano mimi mwenyewe jana tu nimepeleka Cheque na supporting Documents kwa bosi.( sis ni signatories wawili) ana-skim na kusign zilikuwa nyingi na alikuwa anaenda kikaoni. you know what he said? Credibility ni muhimu sana katika maisha na inarahisisha maisha isingekuwa hivyo ningekuambia uziache urudi baadae. Na si kuwa hakusoma alisoma zote lakini kwa haraka na hakuwa na shaka! Mwisho wa mwezi napata mshahara wangu na kupata mahitaji yangu ya uwezo wangu maisha yanaenda nikihitaji extra cash nifanye kazi ya ziada kwa muda wa ziada maisha yanaendelea. Sasa ujanja ujanja hauna mwisho mzuri maana sasa mfano nikifukuzwa kazi nakaa mwaka au na zaidi natafuta kazi si bora nipate kidogo kidogo lakini ni sustainable? Just thinking aloud!
 
Yaani this is the best thread ever. I belive wengi wataisoma na kuizingatia. Wengi tumeathirika kwa kutokuzingatia uliyoandika ndio maana malalamiko meeengi! Turudi tulikotoka kuzingatia maadali kwani yana long term impact!
Ujue Mwana uko sahihi kabisa lakiniMfumo wa nchi ni shida sana sana maana serikali yenyewe haiaminiki!!! kwa wezentu wa mbele Uaminifu ni number one priority!!!!
 
Hii ni kweli kabisa ila wasiyo waaminifu wengi kwenye utafutaji ndiyo wenye mapesa mengi..na waliyo waaminifu wa kweli ni masikini na wenye hofu ya kesho itakuaje juu ya mahitaji.
Hatari sana
 
Ujue Mwana uko sahihi kabisa lakiniMfumo wa nchi ni shida sana sana maana serikali yenyewe haiaminiki!!! kwa wezentu wa mbele Uaminifu ni number one priority!!!!
Eti eeh! Basi sawa wachache tunaoamini na uliotufaidisha tutazidi toa elimu lakini! Ila system nzima inabidi ifumuliwe as ilifika wakati ( mfano mdodgo bandarini) wewe unaesema bei halali ili ulipie ushuru kihalali walafi wa TRA wanakupandishia. Yule ambaye sio muadilifu anakadiriwa bei kuduchu. Jamani tubadilike kuna faida yake. Basi kama si si kufaidika hapa basi hata mbele ya Mungu basi.
 
Kuna baadhi ya vitu vinapita katikati ya Dini na upagani na vinamilikiwa pande zote.

Mwizi au fisadi hata awe na mamillioni mangapi maisha yake yanautofauti mkubwa na mtu mwaminifu anaejitambua hata kama anaishi chini ya dola moja.

Watu waongowaongo mara nyingi wanaishi maisha ya kutangatanga na hata akifanikiwa hafurahii maisha katika ukamilifu wake.

Matapeli mara nyingi hata kama akitapeli Trillion wanaishia kuishi maisha ya kungaunga na wasiwasi.

Watu wasio waaminifu kwenye mahusiano wengi wanaishi maisha yaliyo chini ya kiwango. Anakuwa na Furaha za Muda mfupi na maisha yanazungukwa na matatizo mengi yakujiongezea.

Watu wasio waaminifu kwenye Ajira zao, Shuguli zao za kila siku hara kama wakifanikiwa kupitia kutegea,Kudokoa uwezo wa kutunza hayo mafanikio na kuyafurahia mara nyingi ni wa chini. Furaha aliyonayo iko hatarini kukata muda wowote akibainika,

Uaminifu Uaminifu Uaminifu
Umeongea siri kubwa mno hapa ndio maana wazungu wanatusua tu kwa sababu hii
 
Acheni imani potofu na huo ndio mwanzo wa ushirikina. Nawajua matajiri wengi wenye uhakika wa maisha na si waaminifu na hasa katika ndoa zao, na wapo waaminifu sana katika ndoa nk lakini wanaishi jehenum. Maisha hayanaga formula
 
Uaminfu sio wala haujawahi kufananishwa na imani potofu na ni kinyume cha ushirikina.
mkuu hiyo ni kanuni na unapata uhalali wa kuwasemea hao matajiri wako kama uko nao 24hrs, siku saba za juma.
Huyo masikini anaeishi jehanam, ukweli ni kwamba masikini wengi sio waaminifu pia kwny mambo mengine. Na jehanam unayopitia kama gharama ya uaminifu ni BORA zaidi Ya jehanam Unayopitia kama gharama ya kutokua mwaminifu
 
Back
Top Bottom