Uchaguzi 2020 Hafla ya kuapishwa Dkt. John Magufuli kuendelea na Awamu ya Pili ya Urais wa JMT uwanja wa Jamhuri, Dodoma 05 Oct 2020

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
593
1,712
Leo November 5, 2020 anaapishwa Dkt. John Magufuli kumalizia Muhula wake wa mwisho kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika October 28 mwaka huu. Wageni kadhaa wameshafika akiwemo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Kuwa nami kukujuza yanayojiri.

======

09: 44, Dkt. Magufuli anaingia uwanja wa Jamhuri Dodoma. Waliohudhuria uwanjani wamesimama na kupeperusha bendera za Taifa na Dkt John Pombe Magufuli anazunguka uwanja kabla ya kwenda jukwaani.

09: 49, Dkt. Magufuli anapokea salamu ya heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama na wimbo wa taifa unaimbwa.

09:53, Wimbo wa taifa umemalizika kuimbwa na sasa Gwaride linakwenda kukaa katika umbo la Alfa kwa ajili ya kukaguliwa hii inaonesha kwamba mamlaka ya awali yamekwisha.

09:59, Rais amemaliza kukagua Gwaride na ameagwa na bendera yake(bendera ya rais) inashushwa ili kuyavua madaraka yake ya urais wa awamu ya tano kipindi cha kwanza. Bendera sasa inashushwa rasmi polepole na mamlaka yake yanakuwa yameondoka na anabaki kuwa rais mteule anaesubiri kuapishwa.

10:05, Anaelekea jukwaani kwa ajili ya kusubiri taratibu za kuapishwa ili kuchukua mamlaka mapya ya urais baada ya yale ya kwanza kumalizika.

10:07, Rais Mteule anasogea kwenye meza ya kiapo, sasa Rais mteule anaapa. Rais mtele amemaliza kula kiapo na anatia saini kwenye hati ya kiapo. Amekabidhiwa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na sasa makamu wake anakwenda kula kiapo, na kwa sasa ameketi kwenye kiti cha jaji.

10:12, Makamu wa Rais mteule anaapa, Mama Samia Suluhu Hassan amemaliza kula kiapo na sasa anaweka saini kwenye hati ya kiapo na kisha jaji anaweka saini kuwa yeye ndie aliemuapisha.

10:15, Rais anakabidhiwa ngao na mkuki. Na sasa tukio linalofuata ni dua na sala , na viongozi wa dini wako tayari kuanza zoezi hilo.

10:32, Maanadamo rasmi kuelekea jukwaa kuu maandamo haya yatawahusu wote isipokuwa raais baada ya kukamilika kwa dua na sala, na maandamo hayo yanafuata utaratibu maalum. Rais kwa sasa hatakwenda jukwaani mpaka bendera ya rais ipandishwe na ndio zoezi linalosubiri sasa.

10:40, Wimbo wa taifa unaimbwa na bendera ya rais inapandishwa na Dkt John Pombe Magufuli rasmi sasa ni rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa awamu ya pili. Wananchi wanapunga mikono juu kuonesha kushangilia zoezi hilo.

10: 47, Sasa gwaride linakwenda kuweka umbo la Alfa kuonesha mamlaka mapya ya Rais yanakwenda kuanza. na sasa Amiri jeshi mkuu, Rais John Pombe Magufuli anakwenda kukagua gwaride hilo likiwa katika umbo la Alfa. Sasa rais anapanda jukwaa kuu baada ya kumaliza kukagua gwaride na anasalimiana na baadhi ya viongoi wakiwemo kutoka nje ya nchi. Wimbo wataifa unaimbwa. Gwaride maalum linapita mbele ya Rais.

11:25, Rais na makam wake wanapongezwa kwa makofi na kisha utambulisho wa viongozi mbalimbali waliohudhuria kuapishwa kwa rais Dkt. Magufli unafanyika . Wimbo maalum wa kumpongeza rais na makamu wake unaimbwa, pia utafatiwa na burudani nyingine mbalimbali.

11:56, Hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ameanza kwa kutoa salam kwa viongozi mbalimbali akiwemo waziri Mkuu mstaafu, Majaliwa kasimu Majaliwa na wengine wengi wakiwemo viongozi wa dini siasa na wana nchi kwa ujumla.

Siku kama ya leo Nov. 5, 2015 niliapishwa kuwa Rais na siku kama ya leo Nov. 5, 2020 nimeapishwa tena kuwa rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzaniakwa miaka mingine 5 namshukuru sana Mungu. Lakini tofauti na kipindikilichopita niliapishwa katika uwanja wa taifa Dar es Salaam, na kwa mara ya pili naapishwa katika JIji hili zuri la Dodoma. Aidha, nafurahi kuwa rais wa kwanza kuapishwa katika Jiji hili kwa mara ya kwanza.

Napenda niseme kuwa ushindi huu nilioupata sio wa wana CCM peke yao bali ni ushindi wa watanzania wote na nitumie fursa hii kuipongeza sana tume ya taifa ya uchaguzi kwa kusimamia vizuri zoezoi la uchaguzi na pia vyombo vya ulinzi na usalama kwa kusimamia vyema zoezi hili la uchaguzi hongereni sana. Pia kuwashukuru viongozi wa dini kwa kutuogoza vizuri kwa maadili mazuri.

Napenda kuwashukuru watanzania kwa kuonesha utulivu mkubwa katika kipindi chote cha uchaguzi na Kama mjuavyo uchaguzi umekuwa ni chanzo cha uvunjifu wa amani kwa nchi nyingi lakini Mungu ametuvusha salama Tanzania tumevuka mtihani huu salama na dunia imeshuhudia kuwa sisi watanzania ni watu wa amani na tumekomaa kidemokrasia. Na hii ni ishara nyingine kuwa Mungu analipenda Taifa letu tangu tumepata uhuru 1961 tumepita kwenye matatizo mengi lakini kipindi chote Mungu amekuwa akituvusha salama nyie wenyewe ni masha hidi katuvusha salama kwenye janga la korona ambalo mpaka sasa ni tishio kwa dunia.

Napenda kuwashukuru nchi mbalimbali waliokuja kushiriki nasi katika zoezi hili na waliotutumia salamu na uwepo wenu ni ishara ya kuwepo kwa mahusiano mazuri kati yetu na nyie.

Ndugu watanzani amliopo hapa na wale mnaonisikiliza, uchaguzi sasa umekwisha jukumu lililo mbele yetu ni ujenzi wataifa na kuleta maendeleo kwa taifa letu , na kiapo nilichoapa hapa na alichoapa makamu wangu nasema tutahakikisha na kukienzi kwa nguvu zote na bila kujali dini kabila wala rangi nitashirikiana nanyi nyote katika kuhahakisha yale yote tulioyaahidi tunayatekeleza ikiwa ni apamoja na kuendelea kulinda amani na umoja wa nchi pamoja na mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Bado nayakumbuka yote niliyoahidi kupitia ilani ya CCM na nitatekeleza yote bila kujali itikati

Kuendeleza jitihada za kujikomboa na kutekeleza miradi tulioanzisha na kuanzisha mingine mipya kukuza uchumi kushughulikia changamto za ajira hasa kwa vijana na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwa pamoja na kudhibiti wizi na mambo mbalimbali.

Siwezi nikahitimisha hotuba yangu bila kukishukuru chama changu cha CCM na wote walioshiriki wakiwemo wasanii aidha nawashukuru pia wagombea urais wenzangu pamoja na makomo wao.

Asanteni sana wana habari kwa kazi kubwa mliofanya na pia nawapongeza sana wabunge waliochaguliwa na wengi wanatoka katika chama changu cha CCM, na mwisho nawapongeza wananchi wote waliojitokeza kwa wingi.

Sherehe imefana watu wamejaa uwanja na nje ya uwanja na hii inanipa changamoto kwamba serikali inayokuja ianze kwa kujenga uwanja mkubwa hapa Dodoma ili wakati mwingine watu wa Dodoma mkae wote.

Nampongeza Mheshimiwa Mwinyi kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi na pia nawapongeza watanzania wote na hii inadhihirisha kuwa hapa Dodoma ndio makao makuu ya Dodoma na napenda kuwahahakikishia wana Dodoma kuwa yale yote tuliyoahidi tutayetekeleza ikiwamo barabara ya mzunguko kwa kuwa msongamano umeanza kuonekana.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Dunia yetu.
0.jpg
1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
 
Hii nchi yetu ya ajabu sana, na wote tuliomo tunatakiwa kuwekwa makumbusho vizazi vijavyo waje kutushangaa; hawa wanafurahia ushindi feki, na wale wengine wanaogopa kudai haki zao uchaguzi urudiwe kwasababu haukuwa huru na haki.

Sijui tumelogwa?!
 
Hii nchi yetu ya ajabu sana, na wote tuliomo tunatakiwa kuwekwa makumbusho vizazi vijavyo waje kutushangaa; hawa wanafurahia ushindi feki, na wale wengine wanaogopa kudai haki zao uchaguzi urudiwe kwasababu haukuwa huru na haki.

Sijui tumelogwa?!
Kuna 'Hawa' na "Wale"

Wewe uko wapi!?
 
Biblia inakataza kuapa; Mathayo 5:34, lakini jamaa anaapa kwa kuishika hiyo hiyo Biblia!
 
Back
Top Bottom