Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,639
- 47,454
Hodi hodi wanajukwaa leo nimewatembelea ktk jukwaa lenu.Kwavile jukwaa ni la burudani l,na mm nimeamua kuleta burudan ya aina hii.Naomba mnipokee.
Kisu Chenye Mpini Mwekundu -1
RIWAYA: KISU CHENYE MPINI MWEKUNDU
MTUNZI: Ahmed Mussa Mniachi
SEHEMU YA KWANZA
kipupwe kiliufanya mji wa Dar es salaam uchangamke zaidi.
Hali hii iliwakera wauza soda na maji baridi. Waliofurahia ni wenye Vilabu vya pombe na nyumba za kulala wageni ambazo si rasmi maarufu kama Gesti bubu.
Hali ya hewa ilikuwa ni baridi ya wastani ambayo iliwavutia wengi.
Hali hii ya baridi iliwafanya wanywaji wengi kuongeza kipimo cha ulevi.
Miongoni mwa mitaa maarufu ambayo ilifurika watu katika-kipindi hiki ni Buguruni.
Karibu kabisa na soko kubwa la Buguruni kuna baa maarufu inayoitwa Sewa.Umaarufu wa baa hiyo unatokana na biashara maarufu ya mwili ambayo hufanywa na makahaba ambao hujulikana zaidi kama dada poa.Kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu wa rika tofauti isipokuwa watoto.
Wachache walifika hapo ili kupata kinywaji tu.
Wengine walifika hapo kupata huduma za makahaba ambao hulifanya eneo hilo kuwa maarufu na lenye mvuto wa kipekee ukilinganisha na maeneo mengine ya Buguruni.
Eneo hili lina makahaba wengi ambao hujiuza kwa bei nafuu.
Wapo watu wenye ndoa zao ambao ni wateja wazuri wa biashara hii ya ukahaba, hivyo kulifanya eneo hili kuwa na msisimko mkubwa.
Ni eneo la ajabu kwa sababu wateja wake wengi ni wale ambao hulilaani na kuliona halifai mchana, wanapokuwa kwenye vijiwe vya kahawa au wanapochangia hoja zinazoibuka kwenye daladala lakini kumbe ni wateja wazuri linapoingia giza.
Watu wengi walikuwa wamekaa kwenye Baa hii wakiwa na malengo yanayofanana, kama si kujiuza basi ni kununua.
Wanaume wengi walikuwa wamekaa kwenye viti huku wakichagua huyu na yule katika namna ambayo usingeweza kugundua. .....Jinsi walivyowaita wanawake wale ilikuwa ni sanaa nyingine aina yake.
Wapo waliomwita waliyemtaka kwa ishara ya kukonyeza, wapo waliojifanya kwenda nje kisha kumgusa waliyemhitaji kwa namna ambayo hakuna ambaye angeweza kugundua zaidi ya yule aliyeguswa, pia walikuwepo wale ambao waliweza kuwakabili wale makahaba katika staili ambayo wengi iliwashinda, hawa ni wale ambao kama aibu inatokana na mishipa fulani wao ilikuwa imekatwa au haipo kabisa pia kuna ambao waliwasubiri eneo ambalo walihisi mwanga wa taa usingewaadhiri, hawa walivizia maeneo yenye giza kabla ya kuanza chombezo zao.
Walitumia njia ya kuongea nao moja kwa moja huku wakiomba wapunguziwe bei tena kwa sauti ambayo hata mtu aliyeko pembeni angeisikia.
Hili ndio tatizo lenu, kikifika kipindi cha baridi au mvua basi mnatupandishia bei. Alilalamika mmoja wa watu hao baada ya kuona bei imeongezeka kidogo muda huu wa baridi.
Ghafla, akaingia mwanamke ambaye kwa dakika kadhaa aliteka hisia za wengi. Alikuwa ni mwanamke mrefu mwenye sura nzuri ambayo ilipambwa vema na wanja na vipodozi vingine.
Alivaa gauni fupi la kijani ambalo liliruhusu nusu ya mapaja yake kuwa nje. Alikuwa na miguu iliyojaa vizuri na kuwafanya wanaume kadhaa wameze mate kama mtu anayeona ndimu ikiliwa mbele yake.
Rangi yake ilikuwa ni maji ya kunde ingawa sehemu ya mapaja ilikuwa nyeupe kadri ulivyokuwa unaelekea kule lilikoishia gauni. Viatu vyake vyeusi vya mchuchumio viliendana vema na gauni lile ambalo nafasi iliyotakiwa kuwa na mikono mirefu au mifupi ilikuwa imepita mikanda ambayo ililishikilia vema gauni lile. Sehemu ya kifuani iliruhusu robo ya matiti ambayo yalijaa vema kuwa nje.
Ili mradi kila mwanaume mle ndani alichagua sehemu iliyomvutia na kukazia macho.
Wapo waliokodolea macho kifua, wapo waliovutiwa na miguu, wapo..wapo walikuwepo tu, kwani wanakosa?
Alitembea taratibu huku akisindikizwa na macho ya wanaume wenye uchu wa fisi. Kwa mshangao wa wengi akachagua meza iliyokuwa tupu.
Kwa mtu aliyemtazama vema mwanamke huyu angegundua dosari moja tu.
Hakuwa na furaha.
Alionekana kutatizwa na jambo, jambo hilo lilimfanya awe na mawazo mengi kiasi cha kutotamani mteja kwa siku hiyo.
Akiwa na uzoefu wa miaka saba kwenye kazi ya ukahaba kwa mara ya kwanza alijikuta akikataa wateja jambo ambalo liliwavutia zaidi wateja na kuwafanya wapandishe dau.
Haikuwa rahisi kumnasa kwa siku hiyo. Mmoja wa machangudoa wenzake ambaye kiumri alionekana kuwa ni mdogo kwake hakuivumilia hali hiyo, akaingiwa na mashaka.
Huyu alionyesha kuwa na ukaribu zaidi ya ule wa kuwa wote nimakahaba.
Vipi dada Vero unaumwa leo? Aliuliza yule binti.
Hapana mdogo wangu nimechoka, nimechoka kujiuza. Aliongea waziwazi na kumfanya yule msichana abaki mdomo wazi kana kwamba ni kitu cha mwisho ambacho alitegemea kukisikia.
Akamtazama Vero usoni, akapatwa na mshangao baada ya kuona Vero akitiririkwa na machozi.
Una nini dada Vero? Aliendelea kuuliza yule msichana ambaye kiumri alikuwa kati ya miaka kumi na nne na kumi na saba. Badala ya kujibu Vero akaendelea kutiririkwa na machozi.
Hali hiyo ikamfanya yule muulizaji kutokwa na machozi pia .
Akajikuta akilia bila kujua kinachomliza dada yake.Hali ile ya huzuni kwa makahaba wale ikazusha maswali mle baa. Kwa kuogopa kuendelea kuvuta zaidi hisia za watu. Veronika akaondoka huku akisindikizwa na msaidizi wake katika kilio.Dada unalia nini. Aliendelea kuuliza yule binti.
Usilie Sara mdogo wangu hiki ni kilio changu we nisindikize tu.
Hapana dada, kilio chako ni changu sijisikii raha kuendelea na biashara wakati wewe unalia, wewe ndio mlezi wangu dada, wewe ndio kipenzi changu, wewe ni baba wewe ni mama siwezi dada bila wewe siwezi chochote, kumbuka nilipokuwa .. Hakumaliza chochote alichotaka kuongea kikakatishwa na kilio walichoangua wote wawili.
Safari yao ikawafikisha nyuma ya baa ya Kimboka maeneo ya Buguruni sheli. Wakafika kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa inauzwa pombe za kienyeji. Mama mmoja mnene ambaye alikuwa muuzaji akaja kuwalaki.
Walikuwa tayari wameshafuta machozi na kujitahidi kadri ya uwezo wao kuficha ile hali ya kilio.
Vipi wanangu mbona mmerudi mapema leo? Aliuliza yule mama huku akifunga vizuri kifuani kanga ambayo ilianza kulegea.
Tumechoka mama tumeona leo tupumzike mapema Alijibu Vero huku akiingia ndani akifuatiwa na mdogo wake ambaye alikuwa amejawa na maswali juu ya kipi kilichokuwa kinamliza dada yake. Hakuwahi kuingia ndani. Mama Pili , yule mama mnene muuza pombe akaenda kumzuia mlangoni huku akikaza vizuri kanga yake ambayo ilikuwa inakaribia kufunguka.
Hivi nyinyi watoto mna wazimu eeh. Eti tumechoka. huku akibana pua yake.Mnafikiri kama si hiyo kazi mtaweza kuchangia vipi gharama za hapa ndani?
Mama siku moja tu.
Siku moja tu. Nisikilize we mwana tena nisikilize vizuri. Nasema lazima urudi bila mchango huwezi kulala hapa. Aliendelea kufoka Mama Pili huku akifunika vizuri sehemu ya kanga ambayo ilikuwa inakaribia kuyaacha maziwa yake makubwa nje.
Sawa mama kama siwezi kulala mimi naondoka.
Ondoka. Tena ondoka na hii takataka yako Huku akimnyooshea Sara kidole.
Tuondoke mdogo wangu.
Tunaenda wapi dada?
Kusikojulikana.
Kwanini tusimuombe msamaha yule mama tukaendelea kukaa pale.
Hapana mdogo wangu yule Mama si mtu mzuri yaani miili yetu ndio kitega uchumi chake, haiwezekani. Aliongea huku akiendelea kutokwa na machozi.
Mama Pili alikuwa ameshika moja ya nguzo za nyumba yake huku akiwaangalia ndugu wale ambao waliokuwa wanatokomea gizani. Hakuamini kama wangeondoka kweli. Wangeenda wapi nao ni mateka wake? Hili ndilo alilolijua siku zote lakini leo mambo yalikuwa tofauti. Alisubiri dakika kadhaa kuona kama wangerudi kumuomba radhi na kumnyenyekea kama alivyozoea lakini haikuwa.
* * * *
Saa 11.00 waliamshwa na sauti za kipaza sauti iliyokuwa inasikika kutoka msikiti wa jirani na pale walipolala.
Waliamka kwenye baraza ya nyumba ile iliyoko Tabata Matumbi ili wasije wakakutwa na wenye nyumba.
Baridi ilikuwa kali ikawatesa.
Mbu walikuwa wachache kutokana na baridi lakini nao walijitahidi kuongeza mateso kwa ndugu hawa wawili.
* * * *
Ko.ko.ko.ko .. Saa 2.16 viatu vya Veronika, vilikuwa vinashirikiana na sakafu ya korido ya kituo cha afya cha Tabata shule kutoa mlio usio rasmi. Nyuma alikuwa anafuatwa kwa karibu na mdogo wake Sara , mpaka muda huo alikuwa hajafahamu kilichomleta dada yake pale kituo cha Afya.Kadri walivyokuwa wanaelekea upande fulani ndivyo alivyozidi kuhisi sababu ya dada yake kuja huku.Kupima, si uzito kipimo ambacho wakazi wengi wa Jiji la Dar es salaam hukipenda huku wakijidanganya kuwa ndio kithibitisho cha ubora wa afya zao. Ingekuwa uzito wangepima hata Buguruni. Kilikuwa ni kipimo ambacho mabrazameni na masistaduu wengi hawataki hata kukisikia, wanandoa nao hususani wanaume hukiogopa na badala yake husubiria majibu kutoka kwa wake zao pale wanapokuwa waja wazito. Ukimwi. Hakuamini kama dada yake yuko kwenye foleni kwa ajili hiyo.
Biashara yenyewe ya kujiuza kwa nini aje kupima? alishindana mwenyewe na mawazo yake.Wakati akiwa kwenye mawazo hayo ghafla. Vero akamgeukia, akaanza kumnongoneza sikioni. Ingekuwa foleni ya kawaida watu wangetega masikio ili kujua Vero na mdogo wake wananongona nini, Lakini hapa yaliwashinda. Foleni ya kupima, hususani kwa mtu anayepima mara ya kwanza si mchezo. Kila mmoja alikuwa kwenye hali nzito ambayo aliijua mwenyewe tu kwenye nafsi yake. Hakuna aliyekuwa na muda wa umbeya hapo.
Sikiliza mdogo wangu, nimekuja kupima nataka kujua afya yangu, kama unataka twende tuingie pamoja, sikulazimishi ni hiyari yako.
Ukawa ni wakati mwingine wa Sara kushindana na nafsi yake.
Niende nisiende?. Lilikuwa ni swali gumu lililopita kwenye nafsi yake. Ingawa alikuwa na umri mdogo wa miaka kumi na minne lakini alifahamu vema matatizo yanayotokana na maambukizi ya virusi hivyo hatari.
Ah. kwa nini niogope? Kama kufa mbona kuna wengi wanaokufa kwa magonjwa tofauti.? Lazima nipime. Akakata shauri.Niko tayari dada. alinongona baada ya kukubaliana na nafsi yake kuwa kuna umuhimu wa kupima, akaungana na dada yake kwenda kuchukua kadi kwa ajili ya vipimo.Hatimaye zamu ikafika.
Namba kumi na tatu aingie, kumi na nne ajiandae. Ilikuwa ni sauti ya muuguzi ambaye alikuwa na vikadi maalumu vya foleni kwa waliokuja kupima.
Vero aliitazama tena kadi yake akahakikisha kuwa ilikuwa namba kumi na tatu namba kumi na nne ilikuwa ni ya mdogo wake sara.
Twende. Alimuhimiza kwa sauti ndogo.
Ni zamu yako.
Twende tu.Wakaingia kwa pamoja. Kilikuwa ni chumba cha wastani ambacho kilikuwa na meza moja ndogo ambayo nyuma yake kulikuwa na kiti cha daktari na kitanda cha kulaza wagonjwa wakati wa vipimo.
Pia kapu dogo la plastiki ambalo lilikuwa limehanikizwa kwa mabomba ya sindano, mikasi, nyembe na vifaa kadhaa vya tiba.Meza ile ilikuwa imefunikwa kwa kitambaa cha kijani huku juu yake kukiwa na kifaa cha kupimia joto, mapigo ya moyo na vingine vingi.
Jina.
Naitwa Veronika Beda.
Umri.
miaka ishirini na moja.
Una mume?
Sina.
Huyu ni nani?
Ni mdogo wangu tumekuja kupima sote anaitwa Sara Beda.
Pamoja au kila mmoja atachukua majibu peke yake?
Pamoja. alijibu Vero huku akihisi kubanwa na pumzi kwa woga.
Karibuni sana kwenye huduma zetu rafiki za upimaji kwa hiyari.
Ahsante Wakajibu kwa pamoja.
Kwanza nikupongeze kwa uamuzi wa busara ulioufanya au mlioufanya. Watu wengi wanashindwa kufahamu umuhimu wa huduma zetu rafiki ambazo zinakufanya hata ukikutwa na maambukizi kuishi kwa uhuru na matumaini.
Akatulia kidogo na kumeza mate huku akiingiza mkono kwenye kiboksi kidogo ambacho kilikuwa na baadhi ya vifaa.Kazi ikaanza.
* * * *
NAAM!! Riwaya yetu imeanzia hapa .. nini kitajiri
Itaendelea