Hadi Juni 2024, zimeripotiwa taarifa za watu zaidi ya 50 waliotekwa na kupotezwa kabisa

Sawa lakini usifanye ushindani kama huwezi kushinda
Dunia bado inakumbuka ujasiri wa mtu mmoja aliyeokoa maisha ya mamilioni ya Wachina kwa kusimama mbele ya matenki ya kivita huko China wakati wa mapinduzi kuzuia yasisonge mbele.

The Chinese man who stood in frony of Army Tanks!.png

Alikuwa tayari kutoa uhai wake kutetea wananchi wenzake waliokuwa wanauawa kama panzi!​
 
"Uchambuzi huu Kwa hisani ya Boniyai"

Mwaka huu 2024 pekee yake binafsi nime’ ripoti taarifa za watu zaidi ya 50 waliotekwa na kupotezwa kabisa.

Hawa ni baadhi tu ya watu waliopotea kwa kutekwa na kisha taarifa zao kutopatikana mahala popote ikiwemo vituo vya Polisi na Hospitali katika vyumba vya kuhifadhia maiti.

1. Herman William
2. David Gasper Lema
3. Ridhiwani Hemed Msangi
4. ⁠Hamza Said
5. ⁠Paul Jerome Kisoka
6. ⁠Gidion Michael Mwihumbo
7. Kelvin Sebastian Mkabai
8. Benson Erasto Arbogast Ishungisa
9. Casian Mazambo
10. Charles Aden Mwampyate na wengine zaidi ya 40

Tofauti na tulivyozoea kuona matukio ya Jinai mengine ambapo mtu akiuwawa au Kutekwa baada ya muda ndugu na jamaa zake wanaweza kuokota mwili au mabaki ya mwili baada ya kuuwawa.

Miaka ya hivi karibuni imekuwa ni tofauti kidogo, ndugu au Jamaa yako akitekwa akapotea na kuuwawa

Basi uwezekano wa kupata taarifa juu ya kifo cha ndugu yenu ni mdogo sana

Na uwezekano hata wa kupatikana kwa mwili au mabaki ya mwili umekuwa ni mgumu sana.

Bila shaka wauaji wameacha ile mbinu ya zamani ya kuua na kupeleka maiti vyumba vya kuhifadhia maiti

Kuua na kuteleleza mwili barabarani, kuua na kutupa mwili ukiwa katika mifuko ya sandarusi au viroba.Kuua na Kutupa mwili katika bahari au mito

Kwa tukio hili la Edger Edson Mwakabela (Sativa) limetufundisha kuwa watekaji na wauwaji wana mbinu mpya ambayo inapoteza ushahidi kwa 100%.

Mbinu hii ni ya kupeleka watu matika mbuga za wanyama au hifadhi za taifa zenye wanyama wakali, ili baada ya kukuua mwili wako utafunwe na wanyama wa porini.

Edger Edson Mwakabela (SATIVA ) anasema watesi wake walio mteka siku ya tarehe 23 June 2024 walimchukua Dar es saalam kisha kumpaki katika karakana za Kituo cha polisi Oysterbay, Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni na baadae kuanza kuelekea naye mkoani Arusha.

Kwanini Arusha? Kwa akili za haraka utagundua walielekea mkoa wenye Mbuga nyingi za Jirani za Wanyama wakali wenye uwezo wa kula mwili na mifupa yake kama Serengeti, Ngorongoro,Manyara na Tarangire.

Lakini huenda kwa sababu ya msimu wa watalii na ubize wa wageni katika mbuga hizi,Wauwaji wa Edger Edson Mwakabela waliamua kuchagua eneo lingine mbali kabisa baada yabkuona mbuga za Arusha hazina utulivu nyakati hizi

Wakaanza safari ya masaa 15 yenye umbali wa Kilomita 1091 ya kutoka Arusha kuelekea huko hifadhi ya ya Taifa ya Katavi wilaya ya Mlele

Sababu ni moja tu.Walifuata Fisi wenye madoa madoa (Spotted hyena) ambao wanasifa ya kunusa mzoga kuutafuna wote hadi mifupa ikaisha

Hifadhi ya Taifa ya Katavi ina ukubwa wa kilomita za mraba 4,471 (maili za mraba 1,727) ipo Kusini Magharibi mwa Tanzania,kaskazini mwa ziwa Tanganyika, Kilomita 40 kutoka Mji wa mpanda.

"an estimated 4,000 elephants might converge on the area,together with several herds of 1,000-plus buffalo, while an abundance of giraffe, zebra,impala and reedbuck provide easy pickings for the numerous lion prides and spotted hyena clans."

Spotted hyena ndiyo siri ya wauaji ya Edger Edson Mwakabela kutembea umbali wa Kilomita 1,091 kutafuta hifadhi ya Taifa ya Katavi wanakopatika Fisi wa aina hiyo.

Walikuwa wana uhakika wa kuua na kupoteza ushahidi kwa haraka sana, ndani ya masaa 12 tu pasingebaki mabaki ya mwili.

Na ili wasibahatishe kazi yao wakahakikisha wanatekeleza mauaji pembeni ya Mto Ikuu unaosifika kwa Mamba wakali sana pamoja viboko wengi.

Kwa mujibu wa wenyeji wanaoishi pembezoni mwa msitu wa hifadhi wa Katavi wanashangaa imekuwaje mtu huyo ameweza kupatikana akiwa hai bila kutafunwa na fisi au Mamba

Wenyeji wanasema Jamaa ana bahati sana,aende akatoe sadaka,ule msitu nusu saa tu ni nyingi sana sana kuishi,wanyama wanakutafuna

Sasa nimejiridhisha kwa mbinu hii miili ya watu waliopotea kwa miaka ya hivi karibuni tusiwe na matumaini ya kuja kupatikana.

Au kupata ushahidi wa mabaki yao, kama wauaji wanatumia mbinu ya Kuua ndani ya hifadhi na kutelekeza mwili wako ili utafunwe na wanyama.

View attachment 3028293View attachment 3028294View attachment 3028295
Kila ubaya utalipwa
 
Lakini hata Mungu aliwasahaulisha tu kwenye lile Pori mbele ya Inyonga lina Fisi wengi kuliko Katavi proper.

Hiyo njia nimepita sana.
Nadhani utakuwa unamaanisha Hifadhi ya ipembampazi labda, iliyoungana na Wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora na imeingia kidogo upande wa katabi?
 
Kama ni kweli kuwa watu wanatelekezwa kwenye mbunga basi tatizo Ili litaleta madhara makubwa sana awa wanyama wataanza kuizoea nyama ya binadamu na itakuwa tatizo kubwa sana
 
MaCCM ni mauaji makubwa. Hizi mbinuza kiboya ndiyo yanatumia miaka nenda rudi kuua raia wasiokuwa na hatia na kupoteza ushahidi wote. MiCCM ni misenge sana
 
Muwe mnawaambia hao wasishindane na wenye Nguvu kama hawawezi kujitetea.

Hapo ashukuru karma imemstahi na kupotea mazima.

Mwisho hivi Huwa anajuaje kwmaba nimepelekwa.pale,mda Fulani ikawa hivi na vile afu nikapigwa na hiki,nini kinamjulisha yote hayo kwenye mazingira ya kutekwa?

Pole yake.
We mtu mbona una roho mbaya sana?
 
Kuna namna ya kudeal na haya mambo ya mifumo ya kidunia .... Vijana tuna jiamini sana na kusahau penye maslahi ya watu uhai hua ni chembe ya haradani.... Hii ni principal sehemu zote zenye maslahi ukicheza kidogo umepotea...

Sio Kila vita ni ya kupigana na usipigane kama humjui adui Yako vizuri, ukiwajua watanzania hasa WA mitandaoni sidhani kama unaweza kupigana vita Kwa kuwategemea utashindwa tu.

Mtasema sana ila wahusika washafikisha ujumbe Kwa wote waliokua Arusha na Katavi....

Dunia ya Leo inahitaji uelewa mapana sana ukijipambanua tu kama adui wa mifumo UTATUMIKA kupima nguvu ya mifumo ikoje. Na hapa jua UTAUMIZWA tu hata kama mchakato WA kukutumia ulikua unaendelea na haujatimia

Kabla ya kuingia pima kina Cha maji kwanza na ukianza kupokea simu za deals mbalimbali Kwa sababu unamovement flani inayo husisha kuliumiza kundi flani jua umeshajaa kwenye MIFUMO ya wenye uwezo zaidi Yako.

Wakuelewa na aelewe.
 
Unatekwa, unapigwa, unaminywa kolozidad, yote hayo kwa faida ya nani?

Ukisema, eti, unapigania haki za Watanzania, hapana. Mimi na familia yangu hatujakutuma ukatupiganie.
 
Dunia bado inakumbuka ujasiri wa mtu mmoja aliyeokoa maisha ya mamilioni ya Wachina kwa kusimama mbele ya matenki ya kivita huko China wakati wa mapinduzi kuzuia yasisonge mbele.

View attachment 3028369
Alikuwa tayari kutoa uhai wake kutetea wananchi wenzake waliokuwa wanauawa kama panzi!​
Wapi huko maana kama ni pale Tiananen Square Serikali ilizima maandamano Kwa vikosi vya Jeshi
 
Kuna namna ya kudeal na haya mambo ya mifumo ya kidunia .... Vijana tuna jiamini sana na kusahau penye maslahi ya watu uhai hua ni chembe ya haradani.... Hii ni principal sehemu zote zenye maslahi ukicheza kidogo umepotea...

Sio Kila vita ni ya kupigana na usipigane kama humjui adui Yako vizuri, ukiwajua watanzania hasa WA mitandaoni sidhani kama unaweza kupigana vita Kwa kuwategemea utashindwa tu.

Mtasema sana ila wahusika washafikisha ujumbe Kwa wote waliokua Arusha na Katavi....

Dunia ya Leo inahitaji uelewa mapana sana ukijipambanua tu kama adui wa mifumo UTATUMIKA kupima nguvu ya mifumo ikoje. Na hapa jua UTAUMIZWA tu hata kama mchakato WA kukutumia ulikua unaendelea na haujatimia

Kabla ya kuingia pima kina Cha maji kwanza na ukianza kupokea simu za deals mbalimbali Kwa sababu unamovement flani inayo husisha kuliumiza kundi flani jua umeshajaa kwenye MIFUMO ya wenye uwezo zaidi Yako.

Wakuelewa na aelewe.
Umefafanua vyema. Vijana wakubali tu kuna wababe ambao ukigusa maslahi yao hawana huruma. Pia hawa wanaharakati na viongozi wa upinzani zile ndo kazi zao ila na wao nyuma ya pazia wanakula na hao hao wanaowapinga. Vijana wanajazana ujinga Twitter na matokeo yake baadhi huumia. Hakuna mtoto wa kiongozi mkubwa wa upinzani utamkuta mahakamani kijinga au kwenye mabalaa yoyote kwasababu wazazi wao wanawazuia wasijiingize kwenye kazi zao.
 
Inamaana hapo Dar es salaam hakuna mahala kuna chatu? Walishindwa kumtupa deep sea hapo na kumonitor survival yake in 30mins tu.

Nahisi Arusha na Katavi bado kulikuwa na project inayoendelea, kuna walichokuwa wanatafuta.
Uhai wa binadamu usidhani ni kama wa mnyama? Unakumbuka dokta ulimboka alivyopona kuuawawa.
 
Back
Top Bottom