DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,131
- 24,680
"Uchambuzi huu Kwa hisani ya Boniyai"
Mwaka huu 2024 pekee yake binafsi nime’ ripoti taarifa za watu zaidi ya 50 waliotekwa na kupotezwa kabisa.
Hawa ni baadhi tu ya watu waliopotea kwa kutekwa na kisha taarifa zao kutopatikana mahala popote ikiwemo vituo vya Polisi na Hospitali katika vyumba vya kuhifadhia maiti.
1. Herman William
2. David Gasper Lema
3. Ridhiwani Hemed Msangi
4. Hamza Said
5. Paul Jerome Kisoka
6. Gidion Michael Mwihumbo
7. Kelvin Sebastian Mkabai
8. Benson Erasto Arbogast Ishungisa
9. Casian Mazambo
10. Charles Aden Mwampyate na wengine zaidi ya 40
Tofauti na tulivyozoea kuona matukio ya Jinai mengine ambapo mtu akiuwawa au Kutekwa baada ya muda ndugu na jamaa zake wanaweza kuokota mwili au mabaki ya mwili baada ya kuuwawa.
Miaka ya hivi karibuni imekuwa ni tofauti kidogo, ndugu au Jamaa yako akitekwa akapotea na kuuwawa
Basi uwezekano wa kupata taarifa juu ya kifo cha ndugu yenu ni mdogo sana
Na uwezekano hata wa kupatikana kwa mwili au mabaki ya mwili umekuwa ni mgumu sana.
Bila shaka wauaji wameacha ile mbinu ya zamani ya kuua na kupeleka maiti vyumba vya kuhifadhia maiti
Kuua na kuteleleza mwili barabarani, kuua na kutupa mwili ukiwa katika mifuko ya sandarusi au viroba.Kuua na Kutupa mwili katika bahari au mito
Kwa tukio hili la Edger Edson Mwakabela (Sativa) limetufundisha kuwa watekaji na wauwaji wana mbinu mpya ambayo inapoteza ushahidi kwa 100%.
Mbinu hii ni ya kupeleka watu matika mbuga za wanyama au hifadhi za taifa zenye wanyama wakali, ili baada ya kukuua mwili wako utafunwe na wanyama wa porini.
Edger Edson Mwakabela (SATIVA ) anasema watesi wake walio mteka siku ya tarehe 23 June 2024 walimchukua Dar es saalam kisha kumpaki katika karakana za Kituo cha polisi Oysterbay, Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni na baadae kuanza kuelekea naye mkoani Arusha.
Kwanini Arusha? Kwa akili za haraka utagundua walielekea mkoa wenye Mbuga nyingi za Jirani za Wanyama wakali wenye uwezo wa kula mwili na mifupa yake kama Serengeti, Ngorongoro,Manyara na Tarangire.
Lakini huenda kwa sababu ya msimu wa watalii na ubize wa wageni katika mbuga hizi,Wauwaji wa Edger Edson Mwakabela waliamua kuchagua eneo lingine mbali kabisa baada yabkuona mbuga za Arusha hazina utulivu nyakati hizi
Wakaanza safari ya masaa 15 yenye umbali wa Kilomita 1091 ya kutoka Arusha kuelekea huko hifadhi ya ya Taifa ya Katavi wilaya ya Mlele
Sababu ni moja tu.Walifuata Fisi wenye madoa madoa (Spotted hyena) ambao wanasifa ya kunusa mzoga kuutafuna wote hadi mifupa ikaisha
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ina ukubwa wa kilomita za mraba 4,471 (maili za mraba 1,727) ipo Kusini Magharibi mwa Tanzania,kaskazini mwa ziwa Tanganyika, Kilomita 40 kutoka Mji wa mpanda.
"an estimated 4,000 elephants might converge on the area,together with several herds of 1,000-plus buffalo, while an abundance of giraffe, zebra,impala and reedbuck provide easy pickings for the numerous lion prides and spotted hyena clans."
Spotted hyena ndiyo siri ya wauaji ya Edger Edson Mwakabela kutembea umbali wa Kilomita 1,091 kutafuta hifadhi ya Taifa ya Katavi wanakopatika Fisi wa aina hiyo.
Walikuwa wana uhakika wa kuua na kupoteza ushahidi kwa haraka sana, ndani ya masaa 12 tu pasingebaki mabaki ya mwili.
Na ili wasibahatishe kazi yao wakahakikisha wanatekeleza mauaji pembeni ya Mto Ikuu unaosifika kwa Mamba wakali sana pamoja viboko wengi.
Kwa mujibu wa wenyeji wanaoishi pembezoni mwa msitu wa hifadhi wa Katavi wanashangaa imekuwaje mtu huyo ameweza kupatikana akiwa hai bila kutafunwa na fisi au Mamba
Wenyeji wanasema Jamaa ana bahati sana,aende akatoe sadaka,ule msitu nusu saa tu ni nyingi sana sana kuishi,wanyama wanakutafuna
Sasa nimejiridhisha kwa mbinu hii miili ya watu waliopotea kwa miaka ya hivi karibuni tusiwe na matumaini ya kuja kupatikana.
Au kupata ushahidi wa mabaki yao, kama wauaji wanatumia mbinu ya Kuua ndani ya hifadhi na kutelekeza mwili wako ili utafunwe na wanyama.