#COVID19 Hadi 07/10/2021 wananchi wa Marekani waliochanja ni 65%. Lakini maambukizi mapya ni 102,000 na vifo kwa jana ni 1,709!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,882
18,437
Hapo ndkpo mjue hii chanjo ya corona haisaidii kitu. Marekani ni moja ya mataifa ya kibeberu yaliyofanikiwa kuchanja zaidi ya asilimia 60 ya watu wake. Kiwango hicho kinadharia kinapaswa kuikinga jamii na maambukizi mapya kwa kuleta kitu kiitaacho "herd immunity", Lakini kwa corona hakuna cha herd immunity wala baba yake na herd immunity!

Pamoja na Marekani kufikia kiwango kinachotegemewa kupata kinga kwa kundi zima la raia wao, lakini bado corona imeambukiza watu 102,090, na imeua watu 1,709 kwa jana peke yake!

Huu ni ushahidi tosha kuwa chanjo haizuii maambukizi mapya wala haizuii vifo!! Hizi ni taarifa za wazi ambazo kila mmoja anaweza kuziona akitaka!! Kinachoshangaza ni watu kuamua kujitoa ufahamu na kuwadanganya watu kuwa chanjo itawalinda na corona!! Hao wanaoambukizwa kila siku wengi wao wana chanjo mbili.

Je, wewe unayeng'ang'nia watu wachanje kachanjo kamoja katika jamii ambayo waliochanjwa hawafiki hata asilimia 1% utakuwa umesaidia nini% Kama asilimia 65% imeshindwa kuwakinga waliochanjwa je asilimia 1% kwa hapa.

Tanzania itaweza kuwakinga? (mpaka majuzi, watu waliokuwa wamechanjwa Tanzania walikuwa asili ia 0.5%).

Kila mmoja ni shahidi kuwa Tanzania ambao hatujapata chanjo tuko salama kuliko Marekani walikochanjwa wengi! Huu ni ushahidi wa wazi unaoonesha kuwa mbinu tuliyotumia watanzania ya ku tanguliza Mungu katika vita hii ya corona, inafanya kazi vizuri na kwa uhakika kulika mbinu ya kutanguliza "sayansi" na kumpa Mungu nafasi ya pili.

Mawakala wa mabeberu wanaitafuta corona kwa tochi hapa Tanzania hadi wanalazimika kutoa data za uongo ili tu kuwafurahisha mabeberu ili waachie "mkopo". Kwa kweli watanzania tutakuwa watu wa ajabu sana kama tusipoweza kuona uponyaji huu mkubwa sana kwa Taifa letu!
 
Acha porojo, takwimu za Amerika umepata wapi, japo wao takwimu zao zipo wazi, tuletee na takwimu za kwenu. Tujue unasena ukweli au ni ugwaji tu, je unajua idadi ya waamerika au kupotosha tu kwakuwa unaogopa sindano.
Ingia kwenye worldometer ujionee mwenyewe!! Hata takwimu za Tanzania utaziona hapo !
 
Acha porojo, takwimu za Amerika umepata wapi, japo wao takwimu zao zipo wazi, tuletee na takwimu za kwenu. Tujue unasena ukweli au ni ugwaji tu, je unajua idadi ya waamerika au kupotosha tu kwakuwa unaogopa sindano.
Worldometers.info/coronavirus/
 
Mungu aliamua kuiponya Tanzania kwa ajili yake mwenyewe.

Mungu ataendelea kuwafedhehesha wanaotaka chanjo na barakoa zibebe utukufu,kuwa zimepunguza maambukizi.

Ndiyo maana watu wamegoma kuchanjwa na kuvaa barakoa ili Mungu abaki kujulikana ndiye anailinda nchi.
 
Hapo ndkpo mjue hii chanjo ya corona haisaidii kitu.
Umesomea kitu gani mkuu?

Ingawa hata sijasoma hayo uliyoandika huko chini, lakini kichwa cha mada yako na hitimisho hilo hapo limenifanya nikuone kuwa hujui kitu chochote juu ya maswala haya.

Lakini siyo hivyo tu, hata kama wewe ni mpiga 'propaganda' tu, inaonekana wazi kwamba hata kazi hiyo huna uwezo nayo.

Sasa basi, kama umepewa kazi ya kueneza ujinga, huyo aliyekupa kazi hiyo inawezekana hana anachojuwa, kwa sababu angejuwa asingeajili mtu kama wewe!.

Mnaigeuza JF kuwa sehemu ya kusambaza ujinga!
 
Jamaa kaelezea maoni yake, sio lazima iwe ni ajira. Wewe njoo na unachokifaham kumpinga, acha kumshambulia yeye binafsi? Unamfaham na unauhakika hii ni ajira anafanya, lete hoja mkuu.
 
Shule za chini ya minazi hizi!!

Hata kama kweli, 102,000 kati ya watu milioni 333 ni asilimia ngapi?! Ni 0.03%. Kimahesabu hiyo ni zero. Na katika hao walikufa utakuta wengi ni hawa wabishi wa chanjo.

Halafu sijui wapi walisema ukichanjwa hupati kabisa maambukizi?!
 
Jamaa kaelezea maoni yake, sio lazima iwe ni ajira. Wewe njoo na unachokifaham kumpinga, acha kumshambulia yeye binafsi? Unamfaham na unauhakika hii ni ajira anafanya, lete hoja mkuu.
Wewe hapa umeleta hoja gani?

Nitaletaje hoja kwenye jambo ambalo halina hoja?

Ninakukumbuka sana wewe, nilijaribu kukufundisha juu ya jambo hili hili, lakini naona ujinga bado upo palepale!
 
Unaongea kishabiki na hata haujui unalo ongea. Mimi naisha hapa Marekani si kweli unayosema. Marekani ina watu zaidi ya 329.5 M na 35% ni watu 115M ambao hawajachanja. Hospital wagojwa asilimia 95% ni watu ambao awajachanja. Chanjo zinafanya kazi vizuri sana tatizo ni kwa wale wasiochanja.

Lakini kuna watu wachache wamechanja wanapata corona "break through" lakini hawalazwi au kuzidiwa. Na kinga ziko wazi zinazuia 70%-95% hivyo uwezekano wa kuambuliza upo na hii ni kwa kinga zote.
 
Wewe hapa umeleta hoja gani?

Nitaletaje hoja kwenye jambo ambalo halina hoja?

Ninakukumbuka sana wewe, nilijaribu kukufundisha juu ya jambo hili hili, lakini naona ujinga bado upo palepale!
Oh! Nilisahau huu msemo, nisamehe mkuu

"Never argue with a fool, they will drag you down to their level, then beat you with experience"
 
Umesomea kitu gani mkuu?
Ingawa hata sijasoma hayo uliyoandika huko chini, lakini kichwa cha mada yako na hitimisho hilo hapo limenifanya nikuone kuwa hujui kitu chochote juu ya maswala haya.

Lakini siyo hivyo tu, hata kama wewe ni mpiga 'propaganda' tu, inaonekana wazi kwamba hata kazi hiyo huna uwezo nayo.

Sasa basi, kama umepewa kazi ya kueneza ujinga, huyo aliyekupa kazi hiyo inawezekana hana anachojuwa, kwa sababu angejuwa asingeajili mtu kama wewe!.

Mnaigeuza JF kuwa sehemu ya kusambaza ujinga!

There are +140k new cases of Covid a day in the USA right now 3.5-4x the average this time last year..

Tell me what changed?!
 
Unaongea kishabiki na hata haujui unalo ongea. Mimi naisha hapa Marekani si kweli unayosema. Marekani ina watu zaidi ya 329.5 M na 35% ni watu 115M ambao hawajachanja. Hospital wagojwa asilimia 95% ni watu ambao awajachanja. Chanjo zinafanya kazi vizuri sana tatizo ni kwa wale wasiochanja. Lakini kuna watu wachache wamechanja wanapata corona "break through" lakini hawalazwi au kuzidiwa. Na kinga ziko wazi zinazuia 70%-95% hivyo uwezekano wa kuambuliza upo na hii ni kwa kinga zote.
Mkuu Tanzania yetu hii imejaaa vilaza sana, alivyoandika mwenyewe kajiona bonge la mjanja pale.Hesabu Mdogo tu imemtoa kapa.Alivyoona maambukizi mapya 102,000 akasahau kutuletea hiyo 35% wasiochanjwa wapo wangapi kwenye hayo maambukizi.Ndio wanasiasa wanawaweza watanzania kwa kuwaambia uongo kisa wananchi wanapenda kudanganywa.
 
There are +140k new cases of Covid a day in the USA right now 3.5-4x the average this time last year..

Tell me what changed?!
And how many cases are there in Tanzania, do you know?

Well, simply the fact that they (Americans) know how many new cases, (140k), as you say, don't you acknowledge that fact as making a difference from last year? (in fact your numbers are bogus to start with)!
 
Back
Top Bottom