Habari wakuu!? Naomba kujua matibabu ya Toki, uvimbe wenye maumivi juu ya paja unaotokea wakati fulani unapopata jeraha au maumivu mguuni.

Habari

Mfumo wa Kinga wa mwili unahusika na kupambana na vijidudu vya magonjwa kwa njia nyingi, mojawapo ni kuzuia visienee zaidi ya sehemu vilipoingilia. Kwa hiyo kuna matezi maalumu ambayo yanahusika na kuvikamata vijidudu vya magonjwa visipite zaidi ya eneo fulani na kuenea mwili mzima.

Unapoumia mguuni, vijidudu vinaingia hapo kwenye kidonda na vinaanza kuenea kwenda sehemu zingine za mwili, mfumo wa Kinga unavinasa kwenye matezi yaliyoko kwenye nyonga.

Matibabu sio kutibu tezi,Bali kutibu kidonda kwa dawa za kuua vijidudu. Ukienda hospitali utapewa dawa sahihi .
 
Back
Top Bottom