JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,868
- 6,807
GOLUGWA: HATUJAWAHI KUSEMA TUNATAKA KUPINDUA SERIKALI
Naibu Katibu Mkuu Bara – CHADEMA), Amani Golugwa akizungumza na Wanahabari leo, Aprili 11, 2025 katika Makao Makuu ya Chama Mikocheni, amesema Chama chake hakijawahi kutoa tishio la kutaka kuipindua Serikali wala kutishia maisha ya Rais.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehoji ukimya wa Mamlaka za Serikali kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya #CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla aliyedai CHADEMA inachangisha fedha kwenda kununua Virusi vya Ebola na Mpox.
Hoja hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Bara – CHADEMA, Amani Golugwa, Aprili 11, 2025 alipozungumza na Wanahabari, akizitaka mamlaka kuchukua hatua kwa kuwa kauli hiyo inaichafua Nchi katika sekta mbalimbali.
Naibu Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuelewa lugha za Kisiasa zinazotuka kwa kuw anyingine hazimaanishi vile inavyotamkwa, amesema hayo leo Aprili 11, 2025 alipozungumza na Wanahabari