Godbless Lema: Waislamu teteeni mtu kwa sababu ya haki, msitetee mtu kwa sababu ya dini

Lema#MkutanoOkoaBandariZetuTemeke
Ndo nini maana yake kuandika Katika Kila Mwisho wa Aya,Huna tofauti Na Mtoto wa Primary Aliyepewa Simu juzi wao ndio huandika "from James mnyamwezi" mwisho wa sms
 
Wafuasi wa MUDY ni wepesi Sana kudanganyika nakumbuka kipindi kile cha Mzee msoga aliwadanganya atawapa mahakama ya kadhi na wafuasi wote wa MUDY walimpa Kura lkn mwisho wa picha waliishia kupewa kesi za ugaidi
Uhalisia Unajulikana wakristo ndo watu wepesi kufanganyika Kila Siku akina Mwamposa,Mitume wapya na Yesu wa tongareni wanaibuka Na wanapata Wafuasi wengi.
Ilikiwa Rahisi pia kwa paulo Kuwadanganya
 
Wewe unasema hakuna muisilam anaekula kitomoto Kwa data zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuseme wapo wanaokula, palikua nahaja gani ya Lema kuyaongea hayo, yanamantiki ipi katika hotuba yake?. Naje Huoni kuiongozi kusema hayo nisawa nakukashifu waislamu?. Je neno wajinga nyinyi katika hotuba yake Lina mantiki ipi?. Angesema waislamu wasimtetee Samia Kwa sababu ya dini yake nawala wakristo wasimpinge sababu ya dini yake lngekua la Muhimu zaidi.
 
"Tutakwenda kuvunja mipaka ya udini, tutakwenda kuweka haki, usawa na uzalendo mbele ,hii ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu Tanzania" - Nukuu.Hii ni kauli thabiti na ya kizalendo haswa. Kongole nyingi mno ziende kwa kamanda Lema. Nchi hii kwa sasa inamuhitaji mno mtu wa kariba yake kwa ajili ya ulinzi wa rasilimali za taifa letu.
Majizi ya bandarini mnateteana.
 
Lema ameusema ukweli mtupu. Hapo mwishoni tu pa kusema kuna waislam wanakula naye kiti moto na kunywa naye bia, japo ni kweli, lakini hakukuwa na haja ya kuyasema hayo. Ni sawa useme kuwa kuna walokole wanazini, hawamjui Mungu yeyote! Kutenda yaliyokatazwa na vitabu vitakatifu ni dhambi, lakini haimaanishi anayetenda dhambi hamjui Mungu yeyote. Kwa nini watu wanatubu? Ni kwa sababu wanakuwa wametenda dhambi. Na hawawezi kutubu kama hawajui kuna Mungu.

Ni kweli wapo waislam wengi wanaokunywa pombe na kula kiti moto, ndiyo maana wakati wa mfungo wa ramadhani unasikia wenye mabaa wakisema kuwa mauzo yamepungua kwa sababu ya mwezi wa ramadhani, lakini hiyo haimaanishi hawamjui Mungu.
Kweli kabisa kiongozi
 
"Tulimpinga Hayati Rais Magufuli kwa miaka mitano hawakusema kwa sababu ni mkristo,Leo tunampinga Rais Samia wanasema kwa sababu ni Muislam,wajinga nyinyi" Godbless Lema#MkutanoOkoaBandariYetuTemeke.

"Mashehe wengi waliwekwa jela wakati wa Utawala wa Rais Kikwete hawakusema kwa sababu ni muislam,kama Mashehe hao wangewekwa ndani wakati Rais akiwa ni mkristo,nchi hii ingewaka moto,hii ni akili mbovu sana" Godbless Lema#MkutanoOkoaBandariYetuTemeke.

"Leo niwaambie CCM ndio Chama kitakachowaingiza Watanzania kwenye udini kwa sababu akili ya kutawala imefika mwisho kwenye Chama chao" Gobless Lema#MkutanoOkoaBandatiYetuTemeke.

"Chadema tutakwenda kuvunja mipaka ya udini,tutakwenda kuweka haki,usawa na Uzalendo mbele,hii ni kwa maslahi ya nchi yetu Tanzania" Godbless Lema#MkutanoOkoaBandariZetuTemeke.

"Wameingia mkataba wa kijinga kwenye bandari yetu ambayo inategemewa na Zambia,Malawi, Zimbabwe,Congo,Rwanda,Burundi na Uganda" Godbless Lema#MkutanoOkoaBandariZetuTemeke.

"Ndugu zangu Waislamu,teteeni mtu kwa sababu ya haki,msitetee mtu kwa sababu ya dini, Waislamu wengine nakula nao kiti moto na nakunywa nao bia hawamjui Mungu yoyote" Godbless Lema#MkutanoOkoaBandariZetuTemeke.
Lema alaaniwe mbinguni na ardhini. Ametukana sana waislamu. Hakika CHADEMA ni parokia ya mtakatifu Mtei na mwenyeheri Mbowe.
 
Back
Top Bottom