Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza

Kwa kauli hiyo hana tofauti na mtu ambaye atamwambia mwenye njaa, "haya na ukashibe". Ni sawa na kusema, "acheni madawa ya kulevya. Yana madhara"
Una maana gani?

Kwamba watu wana uraibu wa kuzaa na hawawezi kuacha kuzaa?
 
Kwamba viongozi hawana dhamira ya dhati ktk kauli zao
Viongozi mnawapa umuhimu uliopita kiasi nyie wenyewe wananchi.

Kwanza viongozi ni kioo cha jamii tu, ukisema viongozi hawana dhamira dhati katika kauli zao, hiyo dhana inaakisi ukweli kwamba jamii nzima ya Tanzania haina dhamira dhati katika kauli zake.

Kwa hiyo, ukiwanyooshea kidole viongozi, angalia jamii ambayo hao viongozi wametoka ikoje?

Sasa wewe unamlea mtoto kwa kumfundisha uongo, akija mtu fulani nyumbani kwako unamwambia mwanao kuwa "mwambie mgeni baba hayupo" , wakati upo nyumbani. Mtoto analelewa kwa kujua kudanganyadanganya ni kitu cha kawaida.

Mtoto analelewa kwa kupigwapigwa bila kufundishwa hoja, kupigwa kwa style ya "mwenye nguvu mpishe".

Mtoto huyu akipenyapenya na kuungaunga mpaka kuwa kiongozi siku moja, utategemea awe mkweli? Utategemea awe si mtu wa kuwapigapiga wenzake tu bila kujali hoja?

Tuna tatizo kubwa kuliko uongozi.

Tuna tatizo la jamii nzima. Uongozi ni sehemu ndogo tu ya jamii.

Uongozi mara nyingine ni matokeo ya matatizo ya jamii, si sababu ya matatizo ya jamii.
 
Wewe akili yako imeishia wapi? Unaongea as if unaishi dunia fulani uko peke yako. Unafikirj ukiweza wewe kulipia gharama za matibabu kila mtu anaweza. Yaani kama yule alieshangaa watu kuandamana kisa bei ya mkate kuoanda na kuuliza kwanini wasinunue keki.
Hela anatoa wapi huyo wakati anaishi kwa dada yake.

Kani bore kidogo nimtukane
 
Mdogo wangu wa kike alijifungua mtoto njiti mpaka dogo anatoka hakuna sehemu ambayo hakukopa gharama zilikuwa juu plus alichelewa kuzaa 38+ years.

So this issue ni very serious nikajiuliza inakuwaje gharama ziligonga 8m+ inakuwaje mtoto wa mkulima ambae kupata 50k kama saving ni mtihani atafanya nini akikutana na mtihani kama huu?

Na tukumbuke hakuna aliyejua kuwa atajigungua mtoto njiti same to kuzaa kwa operation.

Alafu anatokea mtu mmoja anaongea nonses kwenye mada za kujadili kama hizi
 
yaani hospitali za serikali zote ni kama zina laana, yaani wanatoza hadi gharama ya kumuona daktari, eti gharama ya kufungua faili sijui daftari...yaani badala iwe bure sababu ni hospitali za serikali kulinda raia wake..wenyewe wapo busy kukandamiza wananchi wao wenyewe...yaani serikali yetu jamani kama hatuna viongozi wa kutetea wananchi wake. Hadi la hospitali limewashinda..yaani kulinda afya ya wananchi wake wanashindwa...kuweka bure kufungua faili, kumuona daktari iwe bure...matibabu tu ndio yagharamiwe na dawa...wao wameshindwa...wamejificha kwenye kimvuli cha kulazimisha watu wakate bima,....so stupid!!. Pole sana Tanzania nchi yangu
 
Viongozi mnawapa umuhimu uliopita kiasi nyie wenyewe wananchi.

Kwanza viongozi ni kioo cha jamii tu, ukisema viongozi hawana dhamira dhati katika kauli zao, hiyo dhana inaakisi ukweli kwamba jamii nzima ya Tanzania haina dhamira dhati katika kauli zake.

Kwa hiyo, ukiwanyooshea kidole viongozi, angalia jamii ambayo hao viongozi wametoka ikoje?

Sasa wewe unamlea mtoto kwa kumfundisha uongo, akija mtu fulani nyumbani kwako unamwambia mwanao kuwa "mwambie mgeni baba hayupo" , wakati upo nyumbani. Mtoto analelewa kwa kujua kudanganyadanganya ni kitu cha kawaida.

Mtoto analelewa kwa kupigwapigwa bila kufundishwa hoja, kupigwa kwa style ya "mwenye nguvu mpishe".

Mtoto huyu akipenyapenya na kuungaunga mpaka kuwa kiongozi siku moja, utategemea awe mkweli? Utategemea awe si mtu wa kuwapigapiga wenzake tu bila kujali hoja?

Tuna tatizo kubwa kuliko uongozi.

Tuna tatizo la jamii nzima. Uongozi ni sehemu ndogo tu ya jamii.

Uongozi mara nyingine ni matokeo ya matatizo ya jamii, si sababu ya matatizo ya jamii.
Viongozi wanatudanganya tuko wengi wakati nchi ina mapori makubwa kama nchi yenyewe. Wanaogopa kutawanya maendeleo watu wakaishi nje ya miji. Wanachoona sawa ni kusikiliza na kjtekeleza sera za wazungu
 
Wewe guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo, huwezi kunielewa.

Sishangai kwamba hunielewi, nitashangaa ikitokea ukanielewa.

Na hapa nakupeleka ignore list sitaona tena unachoandika kuanxia hapa.

Na nitaandika popote ninapotaka hunifanyi kitu.

Eeeeeh
Si kwa njia umetumia.. Hayo yote ni wewe. Ufungue uzi wako uandike hayo yanakukuna hata ukitaka kupitisha ujumbe. Sio lazima kuchangia kila uzi. Yuu geti zat?
 
Maisha ya sasa ni ya gharama.

Kama huwezi kumgharamia mtoto, kwa nini unamzaa?
Sasakuna anayewaza kama atazaa mtoto njiti
Au unakuwa na fikra finyu kwa kuwa umejipata
Hali ya kuzaa mtoto NJITI ni kama accident hakuna anayetegemea hilo.
Kuna mambo mengine kama huna la kuchangia unakaa kimya hii inakufanya uendelee kuonekana mwenye HEKIMA
 
Viongozi wanatudanganya tuko wengi wakati nchi ina mapori makubwa kama nchi yenyewe. Wanaogopa kutawanya maendeleo watu wakaishi nje ya miji. Wanachoona sawa ni kusikiliza na kjtekeleza sera za wazungu
Kuwa wengi si suala la ardhi tu.

Samia kasema nchi kubwa lakini hatuhimili ongezeko la watu.

Kwa sababu wachache tumeshindwa kuwapanga watumie resourcws vizuri, wengi tutaweza vipi?

Japan ni ndogo kuliko Tanzania lakini wanaweza kuhimili watu zaidi ya milioni 100.

Hawatumii kuni kupika hao.

Wewe ukiwa na watu milioni 100 Tanzania leo wanaotumia kuni utafanya nchi iwe jangwa.

Utaona hapo si suala la ardhi tu, kuna suala la teknolojia pia.
 
Sasakuna anayewaza kama atazaa mtoto njiti
Au unakuwa na fikra finyu kwa kuwa umejipata
Hali ya kuzaa mtoto NJITI ni kama accident hakuna anayetegemea hilo.
Kuna mambo mengine kama huna la kuchangia unakaa kimya hii inakufanya uendelee kuonekana mwenye HEKIMA
Mkuu huyo jamaa kapuyanga vibaya sana anatoa hoja dhaifu utafikiri mtoto wa chekechea, matarajio ya kila mtu ni uzazi salama Mama mjamzito afike miezi tisa ajifungue kawaida ambazo gharama zake ni rahisi, hii case inayozungumzwa ni nje ya matarajio na gharama zingekuwa ndogo hakuna ambaye angelalamika sasa kumlipisha mtu more than 4m kwa usawa huu nani atamudu katika hali ambayo watu wanashindwa kulipa gharama za mochwari.

Serikali yenyewe imeona shida kwenye dialysis mpk wanaangalia namna ya kupunguza gharama halafu huyu gharama za kuokoa watoto anasema watu sijui wazae kwa mpango sijui population kubwa mara hawalipi kodi hayo yanahusiana na nini mbona hazungumzii matumizi mabaya ya serikali pia juzi tu tumesikia makumbusho ya marais yanajengwa kwa 34B hizi hela zingeelekezwa huko gharama zingeshuka kiasi gani, vipi sheria ya kuwalipa wenza wa viongozi huko ni hela kiasi gani zinaenda na zingeelekezwa kwenye hii issue gharama zingeshuka kiasi gani. Kapuyanga sana
 
..wamejificha kwenye kimvuli cha kulazimisha watu wakate bima
Hapa ndipo kuna pointi ukiiweka kiuchanya.

Ngoja nianze kwanza kwa kuwapa pole wote wanaokumbana na shida hiyo ya ghafla. Mungu awasaidie na kuwatia nguvu.

Unaonaje suala la, badala ya kuwalazimisha wananchi wote wakate bima. Basi kuwe hata na bima ya makundi maalumu mfano. BIMA YA UZAZI tu wakate wote wenye mpango wa kujifungua miezi mitano ijayo?

Tuliona jinsi bima ya watoto ilivyofanikiwa, labda watanzania tunataka bima hizo. Watu wasaidiwe kupitia bima serikali ijitahidi kuongezea ruzuku huko lakini sio kiholela?

Kivyovyote vile ni lazima tuchangie gharama ya kuwasaidia watoto njiti. Muhusika na jamii (serikali na ndugu) ili kuwe na uwajibikaji pande zote. RESPONSIBILITY. Hili halikwepeki.
Aione pia cocochanel 3 Angels message jerryempire na wengineo. Poleni sana tutafute sasa njia inayoweza kuwa suluhisho linalowezekanika.

Katika hili itabidi tutumie akili ya Kiranga yeye (strategy yake) analimudu vizuri kwa sababu kiimani anakubali dunia ipo hivyo ni fujo, lolote laweza kutokea (chaos) na ameonelea ni muhimu KILA MMOJA kuweka mipango yake kwa namna hiyo. Ni wazo zuri sana hili katika kukabili majanga. Kuhamishia gharama serikalini kwanza kimsingi ni kurudisha gharama kwa wananchi wenyewe maana serikali ni watu.

Ni lazima tunyumbulike, tuishi kama vile tunapanga kila kitu (we make things happen)..... na wakati huohuo mahala fulani tujipange kama vile mambo yanalipuka tu (shit happens).

Ninapotetea kujipanga simaanishi kila mmoja aweke milioni kumi (10M+) kwa ajili ya uzazi tu!!. Lakini mipango ipo mingi tu, mfano hilo la kutumia bima kuwalipa wao kuibeba hiyo hatari. Naamini gharama ya kulipa mtu binafsi haiwezi fika milioni hizo. Huu mpango utawasaidia watu wenye nia moja WAZAZI
 
Nawe naye, umemsoma mwanzoni huyo alivyo andika hata kama nini maisha ya watoto kuandika hayo yote. Mbona wewe umeandika kueleweka tunaelekea wapi.. Mnafikiri kila mtu ni kama mnavyotaka. Hata aandike nini kukandia big No No No na mtu kafungua uzi kuweka hoja yake. Badsla ya kuelimisha anaanza kwa kukandia na sijui kaeleza nini baada na maurefu yake. Kachemsha Kachemsha tu.. Mwenye pesa huyo.
 
Huyo likimkuta ndo ataelewa watu huwa wanapitia hali gani labda asiwe na uzazi
 
Back
Top Bottom