JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,661
- 6,395
Licha ya Mamlaka za Kiserikali pamoja na Wadau kueleza mipango mikakati na kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza vifo vya Mama na Mtoto hasa vinavyotokana na Watoto Njiti (Watoto waliozaliwa kabla ya muda) lakini hali inaonekana kuwa sio shwari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ambapo kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wazazi ambao wamejifungua Watoto Njiti kutozwa gharama kubwa hali ambayo inatufanya wengine kulazimika kuweka bondi ya mali zetu au kukopa ili kupata fedha za kulipia kupata watoto.
Baadhi ya sisi wazazi ambao tumekumbana na changamoto hiyo kwa kukaa Hospitalini kwa muda wa wiki moja hadi mbili tumekuwa tukitakiwa kulipa kati ya Shilingi Milioni 2 hadi 6.
Hali hii inasababisha baadhi ya Wazazi hasa wenye hali duni Kiuchumi kulazimika kuweka bondi ya mali au vitu vya thamani kwa lengo la kupata fedha ili matibabu yakiisha tuweze kuruhusiwa hospitalini.
Hali hii imeongeza maumivu kwa baadhi ya wazazi huku wengine wakifikia hatua ya kutaka kutelekeza Watoto hao hospitalini kutokana na gharama kuwa kubwa.
Matukio mawili ya hivi karibuni, wapo wazazi waliambiwa kama wanataka kuchukua Watoto wao watoe Shilingi Milioni 5 lakini baada ya Wazazi hao kudai kuwa hizo ni pesa nyingi kwao ndipo waliambiwa watoe Shilingi Milioni 3, kinyume na hivyo wakaambiwa hawezi kupewa Watoto, hali ambayo imewalazimu nao kuuza na kuweka bondi baadhi ya mali ili kupata fedha hiyo.
Nimelazimika kuandika hapa baada ya kuona wenzangu yamewakuta wakiwa hawana uwezo wa kulipia gharama hizo.
Nitoe wito kwa Wizara ya Afya pamoja na mamlaka nyingine za Kiserikali kufuatilia kwa ukaribu suala hili kwa sababu limekuwa kilio kwa wengi.
Kulingana na hali ya maisha gharama hizo ni kubwa, sio rahisi Wananchi hasa wenye kipato duni kuzimudu hali ambayo binafsi nahofia kuna wakati baadhi ya wazazi wanaweza kushindwa kuzimudu na uenda wakati mwingine ikawa inapelekea changamoto ya kutohudumiwa ipasavyo kwa wakati na kusababisha vifo kwa watoto njiti jambo ambalo tungeweza kuliepuka kwa kuweka gharama au utaratibu rafiki kwa wahusika.
Kama endapo huduma za kuwahudumia Watoto Njiti ni ghali sana basi mamlaka ziongeze uwekezaji katika eneo hilo kwa lengo la kusaidia wazazi wanaojifungua watoto njiti ili kuepuka makali ya gharama ambayo yanafanya baadhi wafikie hatua ya kuuza mali ambazo pengine zingewasaidia katika kugharamikia matunzo ya watoto hao.
Nilipouliza wanadai Mashine zinazotumiwa na Watoto hao wanaozaliwa kwamba zipo chache na zina gharama kubwa katika uendeshaji wake, kama ni hivyo, basi naomba Serikali iingilie kati kujua namna ya kutusaidia Wananchi wake wenye kipato cha kawaida.
Pia soma
~ Watoto njiti zaidi ya laki mbili Nchini huzaliwa kwa mwaka
~ Serikali na Mkakati wa Kupunguza Vifo Vya Watoto Njiti Nchini