Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,245
1642571100215.png

Ni mwendo ule ule, umafia wa kimya kimya, kwa Voda na Tigo wameanza kutesti mitambo kwa kkupunguza GB za vifurushi vya mwezi.

Kuanzia sasa tutegemee lolote, hii ni trailer tu, bado muvi kamili ya machinjo yatayofanyika kimya kimya gizani usiku wa manane, nadhani tunaweza kuamka asubuhi mabadiliko kadha na kadha yakiwa yamefanyika kwenye vifurushi vingine.

Screenshot_20220118_231344.jpg
 
Ujinga wa wabongo ni kwamba watalalama weee lakini baada ya wiki washazoea

Na ndio spirit wanayotumia wamiliki wa mitandao kupandisha gharama za vifurushi

Imefika hatua kukikucha tu lazima ucheki menu kama ulichokinunua jana ndo hicho hicho kipo na leo, maana vifurushi vinapanda kama dollar
 
Wakuu,

Jana nimeishiwa bando niko Halotel, kawaida naweka elf 3 kwa wiki mwanzoni nilikuwa napata GB 3 na point, majuzi ikawa kwa elfu3 ile ile napata GB 2, jana nimeweka elfu 3 ile ile nimepata GB 1.6.

Nataka kuhama Halotel wapi kuna nafuu?

Hapa sijagusia bidhaa mbalimbali zinazopanda bei kila siku.
 
Back
Top Bottom