Geronimo Pratt: Kiongozi wa Black Panther na Godfather wa Tupac aliyeishi Tanzania baada ya FBI kumbakikia kesi iliyomweka gerezani miaka miaka 27

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
618
1,803
PRATT.jpg

Elmer "Geronimo Ji-Jaga" Pratt

Kama ni mfuatiliaji wa muziki wa Tanzania, basi utakuwa unaikumbuka ngoma kali ya Nako2Nako inayoitwa We Ndiyo Mchizi Wangu Remix (2008) iliyowashirikisha marapa kibao kama vile Fid Q, Geez Mabovu, Babuu, Mwana FA, Temba, Mansu Li n.k

Ukiisikiliza vizuri ngoma ile kwenye ubeti wa Ibra Da Hustla utamsikia akighani maneno haya:

Big up kwa machizi wangu walioko behind (back)

Nje na ndani, bara na pwani, amani

Peace kwa jeshi yangu ya dimes na ngumi

Wanamapinduzi wote….bila kumsahau the one and only Geronimo Pratt

Remember when we sat, what we talked about ilikuwa fact

Na haitawahi kuwa televised, na remember that

We ndiyo mchizi wangu, god-father wangu kama Pac

(Nakuendelea…)

Naam! Nilitaka usome hilo jina “Geronimo Pratt”. Huenda si wengi walijua ndiyo jina lililotajwa hapo, lakini hata kama wanajua, basi si wote wanaomjua ni nani.

Sasa basi, Geronimo Pratt ni nani?
Geronimo Pratt alizaliwa Elmer Pratt, Septemba 13, 1947 huko Morgan City, Louisiana, Marekani.

Pratt alihudumu katika ziara mbili za kivita kama mwanajeshi katika Vita vya Vietnam, na kufikia cheo cha sajenti na kupata medali na tuzo kadhaa za utumishi jeshini.

Baada ya kufanya ziara zake mbili, Pratt alisoma sayansi ya siasa katika chuo cha UCLA na baadaye aliajiunga na Black Panthers. Baadaye alipanda kuwa Waziri wa Ulinzi wa kundi hilo.

Black Panther Party kwa ufupi
Black Panther Party ilianzishwa na Huey P. Newton na Bobby Seale huko Oakland, California mwaka wa 1966. Kundi hilo hapo awali lilijiita Black Panther Party for Self-Defense.

Kwanza lilianzisha doria katikaa vitongoji na kuwalinda wakazi (watu weusi) dhidi ya ukatili wa polisi. Hata hivyo, chama hicho baadaye kilibadilika na kuwa kikundi cha wanamapinduzi cha Ki-Marxist ambacho kilipigania haki za umiliki wa silaha kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika, ili kupambana na kutengwa na vikwazo vya Wamarekani weupe.

Katika kilele cha kundi hilo mwishoni mwa miaka ya 1960, lilikuwa na chapters katika majiji kadhaa makubwa ya Marekani na wanachama wapatao 2,000.

Black Panthers walikuwa sehemu ya vuguvugu kubwa la Black Power, ambalo lilisisitiza watu weusi kuona fahari ya rangi yao na kuungana ili kupata haki zao za kiraia.

Ingawa mamlaka ziliona Black Panthers kama genge, uongozi wao uliona kundi hilo kama chama ambacho lengo lake lilikuwa kupata Wamarekani Weusi wengi zaidi kuchaguliwa kwenye ofisi za kisiasa.

Hata hivyo Black Panther ilidhoofishwa na FBI kufikia miaka ya 1970.

Kesi iliyompeleka gerezani
Jioni moja mnamo Desemba 18, 1968 mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni mwalimu Caroline Olsen (27) na mumewe, Kenneth, walivamiwa na vijana wawili Weusi waliokuwa na bunduki, huko Santa Monica, California. Vijana hao walichukua dola 18 kutoka kwenye mkoba wa Bi. Olsen kisha kumpiga risasi Bw. Olsen mara tano na mkewe mara mbili. Bi. Olsen alikufa siku 11 baadaye. Pratt alikamatwa na kusingiziwa uhalifu huo.

Ushahidi dhidi ya Pratt ulijumuisha bastola iliyotumika kama silaha ya mauaji, gari aina ya Pontiac GTO lenye rangi nyekundu na nyeupe lililotumika kama gari la kutorokea eneo la tukio, na barua ya kurasa nane kutoka kwa mtu mmoja ambaye alidai Pratt alijigamba kwake kwamba alitekeleza mauaji hayo. Bw. Olsen, mume wa mwalimu aliyefariki naye alikuwa ni shahidi katika kesi hii na alimtambua Pratt kanma muuaji.

Pratt alipatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia mnamo Julai 28, 1972. Mwezi mmoja baadaye, alihukumiwa kifungo cha maisha.

Baada ya miongo miwili hati zilionyesha kwamba mtoa taarifa aliyesema kwamba Pratt alikiri kwake alikuwa amedanganya. Ushahidi mwingine wa muhimu ulioeleza ukweli wa alipokuwepo Pratt wakati mauaji hayo yakitekelezwa ulitoweka kwa njia ya ajabu kutoka kwa mafaili ya FBI. Yote haya yalifahamika baada ya miaka mingi ya Pratt kutumikia kifungo.

Kwa ufupi ni kwamba Pratt alikuwa ni target ya FBI kutokana na nafasi yake kwenye kundi la Black Panthers. Kwa hivyo, mpango wote huo wa kumsweka ndani ulisukwa na FBI.

Mkurugenzi wa FBI wakati huo, J. Edgar Hoover aliidhinisha operesheni ya COINTELPRO (COunterINtelligence PROgram) dhidi ya Black Panther Party, akiwaelekeza maajenti wa FBI kufichua, kuvuruga na kukashifu kundi hilo. Operesheni hiyo ilijihusisha na vitendo haramu kama vile kingilia mazungumzo ya simu, wizi wa hati, na kughushi nyaraka ili kuwadhalilisha walengwa.

Kutolewa gerezani na kuhamia Arusha, Tanzania
Juni 1997 Pratt alitoka gerezani na baadaye alipokea dola milioni 4.5 kama malipo ya kifungo asichostahili. Jiji la L.A. lililipa dola milioni 2.75 za suluhu hiyo huku Idara ya Haki ya Marekani ikilipa dola milioni 1.75 zilizosalia.

Pratt alihamia Kijiji cha Imbaseni, huko Arusha ambapo alijiunga na Pete O'Neal pamoja na mke wake Charlotte O’Neal (maarufu kama Mama C), ambao wao mpaka wakati huu bado wanaishi kijijini hapo. Pete na Charlotte walikuwa wanachama wa Black Panther pia.

Pratt alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo mnamo Juni 2, 2011 akiwa Arusha.

Uhusiano na Tupac Shakur
Kabla ya kufungwa kwake, Pratt alikuwa mtu wa karibu wa Afeni Shakur (Mama wa Tupac) aliyekuwa mwanachama wa New York Black Panther. Alikuwa godfather wa Tupac Shakur, ambaye alizaliwa mwaka wa 1971.

Katika nyimbo nyingi, Tupac amemtaja Pratt kishujaa na amekuwa akimuenzi kupitia mashairi yake.

Hapa chini ni baadhi tu ya nyimbo ambazo Pratt ametajwa na Tupac.

Katika wimbo Letter To The President, Tupac anasema: ”In case you don’t know, I let my pump go Get ride for Mutulu like I ride for Geronimo, Down to die, for everything I represent, Meant every word, in my letter to the President”

Katika wimbo Hold Ya Head, Tupac anasema: ”My homeboys in Clinton and Rikers Island

All the penitentiaries Mumia, Mutulu, Geronimo, Sekon

All the political prisoners, San Quentin (who can save you).. all the jailhouses

I’m alive”

Katika wimbo Ballad Of A Dead Soulja, Tupac anasema: ‘‘To Geronimo.. all the down ass riders

All the niggaz that put it down, all the soldiers”

Katika How Can We Be Free – Shairi aliloliandika Tupac, anasema: ”Can tell by the way you smile at me

then I remember George Jackson, Huey Newton and Geronimo 2 hell with Lady Liberty
 
View attachment 2096259
Elmer "Geronimo Ji-Jaga" Pratt

Kama ni mfuatiliaji wa muziki wa Tanzania, basi utakuwa unaikumbuka ngoma kali ya Nako2Nako inayoitwa We Ndiyo Mchizi Wangu Remix (2008) iliyowashirikisha marapa kibao kama vile Fid Q, Geez Mabovu, Babuu, Mwana FA, Temba, Mansu Li n.k

Ukiisikiliza vizuri ngoma ile kwenye ubeti wa Ibra Da Hustla utamsikia akighani maneno haya:

Big up kwa machizi wangu walioko behind (back)

Nje na ndani, bara na pwani, amani

Peace kwa jeshi yangu ya dimes na ngumi

Wanamapinduzi wote….bila kumsahau the one and only Geronimo Pratt

Remember when we sat, what we talked about ilikuwa fact

Na haitawahi kuwa televised, na remember that

We ndiyo mchizi wangu, god-father wangu kama Pac

(Nakuendelea…)

Naam! Nilitaka usome hilo jina “Geronimo Pratt”. Huenda si wengi walijua ndiyo jina lililotajwa hapo, lakini hata kama wanajua, basi si wote wanaomjua ni nani.

Sasa basi, Geronimo Pratt ni nani?
Geronimo Pratt alizaliwa Elmer Pratt, Septemba 13, 1947 huko Morgan City, Louisiana, Marekani.

Pratt alihudumu katika ziara mbili za kivita kama mwanajeshi katika Vita vya Vietnam, na kufikia cheo cha sajenti na kupata medali na tuzo kadhaa za utumishi jeshini.

Baada ya kufanya ziara zake mbili, Pratt alisoma sayansi ya siasa katika chuo cha UCLA na baadaye aliajiunga na Black Panthers. Baadaye alipanda kuwa Waziri wa Ulinzi wa kundi hilo.

Kesi iliyompeleka gerezani
Jioni moja mnamo Desemba 18, 1968 mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni mwalimu Caroline Olsen (27) na mumewe, Kenneth, walivamiwa na vijana wawili Weusi waliokuwa na bunduki, huko Santa Monica, California. Vijana hao walichukua dola 18 kutoka kwenye mkoba wa Bi. Olsen kisha kumpiga risasi Bw. Olsen mara tano na mkewe mara mbili. Bi. Olsen alikufa siku 11 baadaye. Pratt alikamatwa na kusingiziwa uhalifu huo.

Ushahidi dhidi ya Pratt ulijumuisha bastola iliyotumika kama silaha ya mauaji, gari aina ya Pontiac GTO lenye rangi nyekundu na nyeupe lililotumika kama gari la kutorokea eneo la tukio, na barua ya kurasa nane kutoka kwa mtu mmoja ambaye alidai Pratt alijigamba kwake kwamba alitekeleza mauaji hayo. Bw. Olsen, mume wa mwalimu aliyefariki naye alikuwa ni shahidi katika kesi hii na alimtambua Pratt kanma muuaji.

Pratt alipatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia mnamo Julai 28, 1972. Mwezi mmoja baadaye, alihukumiwa kifungo cha maisha.

Baada ya miongo miwili hati zilionyesha kwamba mtoa taarifa aliyesema kwamba Pratt alikiri kwake alikuwa amedanganya. Ushahidi mwingine wa muhimu ulioeleza ukweli wa alipokuwepo Pratt wakati mauaji hayo yakitekelezwa ulitoweka kwa njia ya ajabu kutoka kwa mafaili ya FBI. Yote haya yalifahamika baada ya miaka mingi ya Pratt kutumikia kifungo.

Kwa ufupi ni kwamba Pratt alikuwa ni target ya FBI kutokana na nafasi yake kwenye kundi la Black Panthers. Kwa hivyo, mpango wote huo wa kumsweka ndani ulisukwa na FBI.

Mkurugenzi wa FBI wakati huo, J. Edgar Hoover aliidhinisha operesheni ya COINTELPRO (COunterINtelligence PROgram) dhidi ya Black Panther Party, akiwaelekeza maajenti wa FBI kufichua, kuvuruga na kukashifu kundi hilo. Operesheni hiyo ilijihusisha na vitendo haramu kama vile kingilia mazungumzo ya simu, wizi wa hati, na kughushi nyaraka ili kuwadhalilisha walengwa.

Kutolewa gerezani na kuhamia Arusha, Tanzania
Juni 1997 Pratt alitoka gerezani na baadaye alipokea dola milioni 4.5 kama malipo ya kifungo asichostahili. Jiji la L.A. lililipa dola milioni 2.75 za suluhu hiyo huku Idara ya Haki ya Marekani ikilipa dola milioni 1.75 zilizosalia.

Pratt alihamia Kijiji cha Imbaseni, huko Arusha ambapo alijiunga na Pete O'Neal pamoja na mke wake Charlotte O’Neal (maarufu kama Mama C), ambao wao mpaka wakati huu bado wanaishi kijijini hapo. Pete na Charlotte walikuwa wanachama wa Black Panther pia.

Pratt alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo mnamo Juni 2, 2011 akiwa Arusha.

Uhusiano na Tupac Shakur
Kabla ya kufungwa kwake, Pratt alikuwa mtu wa karibu wa Afeni Shakur (Mama wa Tupac) aliyekuwa mwanachama wa New York Black Panther. Alikuwa godfather wa Tupac Shakur, ambaye alizaliwa mwaka wa 1971.

Katika nyimbo nyingi, Tupac amemtaja Pratt kishujaa na amekuwa akimuenzi kupitia mashairi yake.

Hapa chini ni baadhi tu ya nyimbo ambazo Pratt ametajwa na Tupac.

Katika wimbo Letter To The President, Tupac anasema: ”In case you don’t know, I let my pump go Get ride for Mutulu like I ride for Geronimo, Down to die, for everything I represent, Meant every word, in my letter to the President”

Katika wimbo Hold Ya Head, Tupac anasema: ”My homeboys in Clinton and Rikers Island

All the penitentiaries Mumia, Mutulu, Geronimo, Sekon

All the political prisoners, San Quentin (who can save you).. all the jailhouses

I’m alive”

Katika wimbo Ballad Of A Dead Soulja, Tupac anasema: ‘‘To Geronimo.. all the down ass riders

All the niggaz that put it down, all the soldiers”

Katika How Can We Be Free – Shairi aliloliandika Tupac, anasema: ”Can tell by the way you smile at me

then I remember George Jackson, Huey Newton and Geronimo 2 hell with Lady Liberty

Rafiki yangu Sana Huyu Mzee, mtu muungwana Sana Na mke wake! Shawatembelea back in 2010!
 
Good stories man
 
Back
Top Bottom