Gerald Hando: Watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie. Asema majibu ya Janabi na Chalamila ni dharau kwa watanzania

Prof Janabi ameongea ukweli mchungu ambao waTanzania wengi hawataki kuusikia......ukitaka kuwateka waTanzania ongea kile wanachopenda kusikia......na ndio maana wajinga wajinga wanathaminiwa na wenye weledi wanatolewa akili........

Janabi hakuzungumza kama mwanasiasa ameongea kutokana na nafasi yake....kwa jinsi anavyoyaona mambo......

Mtu mlevi na mwenye maisha ya hovyo kama Hando hawezi kuelewa kauli za Prof Janabi.......Bali watu waliothirika na vyakula hivyo ndio mashahidi wa hayo......

Alichokiongea Janabi ni kikubwa Sana kwenye akili za mlevi kama Hando........
Janabi yupo sahihi ila kauli ya mkuu wa mkoa sio kabisa ameongea kisiasa,na kauli ya Hando yupo sahihi kabisa kama kiongozi atupatie sababu za msingi kwanin hamna sukari,sukari ina matumizi mengi
 
Japo mnamsifia huyo mtangazaji ila anaongea vitu asivyovijua

Swala la sukari kuwa na madhara hafahamu??

Sukari unayotakiwa mwilini ni sukari hii iliyoadimika ??

Ikiwa mgonjwa wa kisukari abatakiwa asile hadi wali au ugali, itakuwa sukari ya viwandani?

Anavyosikia mwili unahitaji sukari anadhani sukari ya Mtibwa sugar
Nikuulize kwanza,umesikiliza kauli ya mkuu wa mkoa vizuri?na je umesikiliza kauli ya Janabi vizur na mwisho wa siku umekielewa alichokisema Jerald Hando?
 
Kumshambulia Prof. Janabi ni kukosa utimamu mzuri, yule ni mtaalam wa masuala ya Afya ni lazima atoe tahadhari lakini neno lake sio sheria kikubwa likitokea yeye atakua pale Muhimbili kukutibia huku ukilalamika gharama ni kubwa.
 
Usifikiri kila mtu ni punguani.
Kwa taarifa yako yeye ndio kakosa utimamu.....wacha apewe makavu...
 
Prof Janabi ameongea ukweli mchungu ambao waTanzania wengi hawataki kuusikia......ukitaka kuwateka waTanzania ongea kile wanachopenda kusikia......na ndio maana wajinga wajinga wanathaminiwa na wenye weledi wanatolewa akili........

Janabi hakuzungumza kama mwanasiasa ameongea kutokana na nafasi yake....kwa jinsi anavyoyaona mambo......

Mtu mlevi na mwenye maisha ya hovyo kama Hando hawezi kuelewa kauli za Prof Janabi.......Bali watu waliothirika na vyakula hivyo ndio mashahidi wa hayo......

Alichokiongea Janabi ni kikubwa Sana kwenye akili za mlevi kama Hando........
Kwahiyo utaniambia janabi hatumii sukari ?
 
CCM WAWEWESEKA MBEYA

Wameita Bajaji Wapuuuzwa
Wameita Bodaboda wamepuuzwa
Wameita Wamachinga wamepuuzwa
Wameita wafanyabiashara wamepuuzwa
Wameitaa Mama kishe wamepuuzwa
Wameita waandishi wa habari wamepuuzwa

Maandamano ndiyo HABARI YA MBEYA.

Mwisho Wakamtuma Naibu waziri Mkuu Dotto awe anakatisha ktka maandamano ya CHADEMA

Mara aende ,Mara arudi

Wamekutana na midfielder mkata umeme Tundu Lissu,Kawazuia Kupita Kudadekiiiiiiii.

Mkinuna tunapost tena,Shauri zenu
 
Muhimbili National Hospital, MNH (Muhimbili)

Muhimbili Orthopaedic Institute, MOI (MOI)
Zote ni Muhimbili.
Hata Mloganzila inajulikana kama Muhimbili.

MUHAS
MOI
MNH
Muhimbili - Mloganzila.

Ukienda kupata huduma ya CT Scan Muhimbili NH, kama kuna foleni utapelekwa MOI, na MOI ni hivyo hivyo.
 
Janabi anamatatizo ya akili. Afya ya akili. Ila anaendekezwa sababi ya wadhifa wake. Uwa anaongea vitu vingi ambavyo practically havimake sense.
 
Mimi siwezi kula chakula ambacho hakina chumvi, lazima nitatapika!!
Mimi mtu haniambii chochote kuhusu chumvi.

Siwaamini hawa wanaosema tusile chumvi eti ina madhara,ni uongo mtupu,chumvi muhimu sana katika mwili.
 
Zote ni Muhimbili.
Hata Mloganzila inajulikana kama Muhimbili.

MUHAS
MOI
MNH
Muhimbili - Mloganzila.

Ukienda kupata huduma ya CT Scan Muhimbili NH, kama kuna foleni utapelekwa MOI, na MOI ni hivyo hivyo.

Japo unajaribu kulazimisha lakini bado umezidi kuzitofautisha.

1. Umeitaja Muhimbili(MNH)

2. Umeitaja Mloganzila(Tawi la MNH)

3. Umeitaja MOI (Muhimbili Orthopaedic Institute).

Kawaida mtu akikuambia kalazwa Muhimbili amemanisha MNH.

Ukiambiwa yupo MOI (Mifupa)

Aa ukiambiwa yupo Mloganzila unajua kabisa alipo.

MUHAS ni Chuo Kikuu
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mwandishi wa EFM, Gerald Hando ameshangazwa na majibu ya sukari yaliyotolewa na Prof. Janabi yaliyoungwa mkono na mkuu wa mkoa wa Dar.

Hando amesema ni mtazamo finyu kuwaza sukari ni chai pekee ilhali sukari inayotumika kwenye chai ni vijiko viwili. Hando amesema sehemu kubwa ya vitafunwa vinavyotumika nchini vinatumia sukari.

Hando amedai wafanyabiashara wanaotengeneza vitafunwa wamechanganyikiwa na wanajiuliza wakiongeza bei itakuwaje kwa biashara zao.

"Janabi anataka kutudanganya kama mtaalam tena anafanya kosa kubwa la kitaalam, mwanadamu hawezi bila sukari kwasababu ndio chanzo kikuu cha nishati katika mwili, sukari ni zaidi ya maisha ya mwanadamu. Ukitaka kuona nchi inatepeta, kata sukari.

Mkuu wa Mkoa atuambie kwanini sukari haipatikani, watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie sukari. Mvua zinanyesha na zinaendelea, sugar iko wapi?"

Hando amesema Janabi sio wa kutoa majibu ya sukari nchini, akae Moi apambane na Muhimbili yake. Amedai na mkuu wa mkoa kuunga mkono hapohapo ni dharau mbaya kwa watanzania.

Soma=> Profesa Janabi: Bei ya sukari imepanda juu, take advantage

Pia, soma=> Chalamila: Dkt. Janabi alisema sukari ni hatari kwa afya, tumieni fursa ya upungufu huu kuachana nayo msipate magonjwa mbeleni
Mkuu wa Mkoa anakuja na hoja pia kuwa Umeme ni mwingi kasoro ni miundombinu tu...

Mteule wa Rais anayewakikisha mamlaka ya uteuzi ndo anakuja na akiki hizi.....
 
Back
Top Bottom