Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,665
- 8,805
Mwandishi wa EFM, Gerald Hando ameshangazwa na majibu ya sukari yaliyotolewa na Prof. Janabi yaliyoungwa mkono na mkuu wa mkoa wa Dar.
Hando amesema ni mtazamo finyu kuwaza sukari ni chai pekee ilhali sukari inayotumika kwenye chai ni vijiko viwili. Hando amesema sehemu kubwa ya vitafunwa vinavyotumika nchini vinatumia sukari.
Hando amedai wafanyabiashara wanaotengeneza vitafunwa wamechanganyikiwa na wanajiuliza wakiongeza bei itakuwaje kwa biashara zao.
"Janabi anataka kutudanganya kama mtaalam tena anafanya kosa kubwa la kitaalam, mwanadamu hawezi bila sukari kwasababu ndio chanzo kikuu cha nishati katika mwili, sukari ni zaidi ya maisha ya mwanadamu. Ukitaka kuona nchi inatepeta, kata sukari.
Mkuu wa Mkoa atuambie kwanini sukari haipatikani, watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie sukari. Mvua zinanyesha na zinaendelea, sugar iko wapi?"
Hando amesema Janabi sio wa kutoa majibu ya sukari nchini, akae Moi apambane na Muhimbili yake. Amedai na mkuu wa mkoa kuunga mkono hapohapo ni dharau mbaya kwa watanzania.
Soma=> Profesa Janabi: Bei ya sukari imepanda juu, take advantage
Pia, soma=> Chalamila: Dkt. Janabi alisema sukari ni hatari kwa afya, tumieni fursa ya upungufu huu kuachana nayo msipate magonjwa mbeleni