General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Mkuu Invisible natambua wewe ni mzalendo sana kushida hata mimi nakuomba kwa heshima zote kabisa huu uzi uuweke sticky pale juu.

Kuna mambo yanatia uchungu sana na pia tunajifunza mambo mengi kupitia uzi huu maana kuna vijana wamezaliwa kuanzia 1985 wanasikiaga tu Tanzania tulikuwa na viwanda wapate history kupitia hapa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hata mimi naambiwa kuna mpango wa kukifungua lakini kisiasa zaidi kwasababu hakuna sera ya kulinda viwanda vya ndani.Tayari soko la tairi limevamiwa na wafanyabiashara wengi wanaokwepa kodi.Nasisitiza bado uwekezaji mkubwa unatakiwa kufanywa ikiwemo ufungaji wa mitambo ya kisasa. Kurudisha magodown yaliuzwa bila kufuata taratibu eg Pugu road / Nyerere road limechukuliwa na Gachuma kinyemela bila board resolution etc........ Mambo mengi sana yanatakiwa kufanya si hizi siasa za kutaka sifa za reje reja.


G tyres kitafunguliwa later this year. Fununu
 
Yaani hiyo machine tools ndio inaniumiza roho sana maana tulipewa msaada kama sikosei na Wabulgaria. Walipoondoka tu na kukabidhi rasmi kwa watanzania waliowapa mafunzo sijui kilitokea nini kiwanda kwishney. Huwezi amini kilikuwa kinatengeneza mota, misumeno, misumari na vimashine vidogo vidogo kibao vyenye ubora wa hali ya juu achana na hizi feki zilizojaa kariakoo toka kule ambapo kila mtu anapafamu. Aiseewe achaa tu perma sharp, swala daa nashindwa kuendelea

Basi basi usilie bwana.., haya em futa hayo machozi.., siku si nyingi parapanda italia wala sio mbali.., we ngoja tu.., haya nyamaza..
 
Kwa swala la viwanda kufa ni shida kubwa sana sidhani kama tungekua na tatizo kubwa la ajira kama ilivyo sasa

Naomba kama inawezekana tuweke thread inayo onesha viwanda vilivyo fungwa
kwa makusudi na watawala wasio waaminifu kwa kila mkoa.

Mfano Kilimanjaro kuna Machine tools pale junction ya kwenda Machame na Kiwanda cha Magunia kule Kiboroloni.

Unaweza ukatoa machozi aisee
 
Direct employment 450 iliyopotea na bado wakatafuna u$ 10 million za NSSF hakuna aliyefungwa,aliyeshitakiwa ...........

Mkuu nakumbuka miaka ya 90 kuna gari aina ya Toyota dyna(chai maharage) nlikuwa nasembenza huyo mwenye gari alikuwa anafungaga hizo tairi zilikuwa imara sanaaa yaani balaaa.

Ni kweli general Tyre walikuwa wanatumia teknolojia ya kijerumani kutengeneza hzo tairi?
 
Kwa swala la viwanda kufa ni shida kubwa sana sidhani kama tungekua na tatizo kubwa la ajira kama ilivyo sasa

Naomba kama inawezekana tuweke thread inayo onesha viwanda vilivyo fungwa kwa makusudi na watawala wasio waaminifu kwa kila mkoa.

Mfano Kilimanjaro kuna Machine tools pale junction ya kwenda Machame na Kiwanda cha Magunia kule Kiboroloni.

Kulikuwa na Coffee Curing pale Moshi na Tanalec kule Arusha, hivi navyo vinajikongoja au vilishakufa?

Kibo Match pale Moshi kipo mochwari sasa hivi.
Breweries aahh inauma ...
***2015 operation Delete CCM*** basi
 
Halafu nisikie hili neno " ivi tumerogwa na nani?" Silipendi hili neno kwa kweli. Tunatafunwa hivi halafu tunakuja na sentensi kama hii
 
Ngongo

Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??
 
Last edited by a moderator:
Ngongo

Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??

Yani unaambiwaje Tanzania hamna tena kiwanda! Unachoongelea wewe kilishakufa muda sana!
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi sipost kitu au kuchangia threads especially zinazohusu mustakbari wa nchi yenu maana inakera na kutia hasira kiasi kwamba kila nikitaka kuchangia linalonijia ni tusi tu,yaani hawa wa...... kum....... aghrr
 
Kulikuwa na Coffee Curing pale Moshi na Tanalec kule Arusha, hivi navyo vinajikongoja au vilishakufa?

Kibo Match pale Moshi kipo mochwari sasa hivi.
Breweries aahh inauma ...
***2015 operation Delete CCM*** basi

Dah mkuu umenikumbusha mbali sana yaani nakumbuka nyumbani tumeshawahi kutumia jiko la Tanalec kumbe ilikuwa made in Tanzania?? inatia uchungu sana aisee!!
 
Acha kilitex mkuu kuna baby biscut kuna kiwanda cha kutengeneza sillingboard, camartec, tanzania litho, nmc kiwanda cha maziwa aisee jamani..!!
 
Alafu kuna wajinga kwasababu wanafaidika na vijipesa sasa wanaitetea CCM kwa nguvu zote......ubinafsi umetujaa.....ndio maana mimi bila kupepesa macho naamini Julius Kambarage Nyerere ni mtakatifu......kwani hakuna binadamu asiye na mapungufu......lakini kiwango chake cha uaminifu na utumishi wa dhati....ni zaidi ya utumishi wa kawaida.....
 
Sasa kulia ndiyo solution wakuu mnaolia lia hapa?

MAmbo yote Oktoba kwenye ballot paper. Kama sio mwaka huu basi 2020! Hahaha, inasikitisha lakiniii! Laana ya ma albino iwafikie wapate kushindwa kwa kishindo na kutoka kwa amani kama Goodluck Jonathan wa Nollywood.
 
Back
Top Bottom