GEITA: Serikali yatenga zaidi ya Sh. Bilioni 6 za kuchimba visima Chato!

habar wakuu,

Serikal ya JPM imetenga zaid ya bilion 6 kuchimba visima na kusambaza maji kutoka ziwa victoria wilayani chato mkoani Geita

source:itv
hahahahaha hichi ndicho walicho kisema ITV ? HAHAHAHAHAHA
 
hio ndio hatma ya nchi hii ni kuchimba visima tu na kujaza mashimo kila pahala, badala ya kuwa innovative na kuweka mitambo ya maji ya kisasa nchi nzima tanzania inarudi nyuma, kisha ati viwanda kichekesho kikubwa hiki.
jaza mashimo ya visima chato kisha tenga pesa uje ujaze mashimo daresalama na endelea na nchi nzima hehe
Ukiwa pale Chato ziwa unaliona kabisa..kuna wakulima wa nyanya huwa wanavuta maji kwa ajili ya mashamba yao...sasa kuchimba visima vya nini wakati wamaweza sambaza kwa kuweka mitambo tuu...well labda maji ya ziwa hayaruhusiwi!
 
Niliwahi fungua duka huko. Walipoona kaja msukuma Wateja wote wakakakimbia tunaenda kwa msukuma wenzetu hawa jamaa kwa ubaguzi mmmmmm
 
Ukiwa pale Chato ziwa unaliona kabisa..kuna wakulima wa nyanya huwa wanavuta maji kwa ajili ya mashamba yao...sasa kuchimba visima vya nini wakati wamaweza sambaza kwa kuweka mitambo tuu...well labda maji ya ziwa hayaruhusiwi!
Mleta mada mwenyewe umemuelewa?,anasema mradi wa.visima na kusambaza Maji Kutoka ziwa Victoria. Tushike lipi
 
Chato Airport
Chato inajengwa bohari kubwa ya madawa kuhudumia mikoa mitano
Chato inajengwa bandari kubwa ya samaki
Chato TRA
Chato ina taa za barabarani
Chato tatizo la Maji limepewa bajeti kubwa

Nyerere angefanya hivi kwa Butiama tungefika?
Mwinyi angefanya hivi Kisarawe?
Mkapa angefanya haya Masasi?
JK angepeleka kila project kubwa kwake?

Ni Rais wa watz wote sio Rais wa Chato
 
TCU haijakosea kabisa, namna michango ya watu humu ilivyo? Yaani hawaulizi hata kutaka kujua huo mpango ulikuwa wa lini, unajumuisha sehemu gani nyingine za nchi, je kuna sehemu au wilaya myingine zina miradi ya maji mikubwa kama hiyo, je Chato kuna shida au uhaba wa maji, wenyewe ni kutaka kuona watu wa Chato hawa enjoy haki zao kama wananchi wengine wa nchi hii kwa vile tu mtoto wao amekuwa Rais wa nchi. Kufikiri kweli kazi lakini kama imekuwa kazi kubwa namna hii hata kwa watu ambao wana nafasi ya kupata taarifa sahihi wakiwa wamekaa mbele ya gadget zao, basi tuna tatizo kubwa zaidi. Tumekuwa watu wa kupenda uzushi, uongo, uzandiki, fitina na uchonganishi utadhani katika hilo kuna la maana tutakalovuna. Haya tuendelee na kuzikiji haja ya hamu na ashki zetu. Wanasema zoea zoea watu utakuja zoea majini. Endekezeni endekezeni ashki zenu mtakuja kupata ashki za ushoga!
Umedhihirisha kuwa ni kweli TCU haijakosea maana badala ya kuweka facts na jinsi habari unavyoijua umeishia kuongea maneno ya chumbani
 
Wanatengeneza Ziwa 6 billion mbona kama ni nyingi sana kwa nini wasichukue maji kutoka Ziwa Victoria tuu kwa gharama hiyo...
 
Back
Top Bottom