GEITA: Mnyika, Katambi, Makene wakamatwa na polisi na kuachiwa

John Mnyika, Patrobasi Katambi, Conchester Rwamulaza na Tumaini Makene wako kituo cha polisi Geita wakihojiwa kwa kosa la kuweka Bendera za CHADEMA kwenye gari zao.

# Huu ni utawala wa kuwekwa kwenye kumbukumbu
======

..UPDATE..

Mnyika na wenzake wameachiwa huru baada ya Jeshi la Polisi kujiridhisha juu ya sababu za wao kusambaza bendera za chama pasipo kutoa taarifa.

Inaelezwa kuwa, OCD wa mkoani humo aliagiza jeshi la polisi kuwakamata kufuatia kushangazwa na kuona bendera za chama zinazunguka mjini bila yeye kupewa taarifa yoyote, ambapo wakamueleza kuwa wana ziara ya vikao vya ndani hivyo hawajavunja sheria yoyote kwa kufanya hivyo.

Baada ya maelezo hayo, OCD alilazimika kuwapa ruhusa.
 
========

Taarifa zaidi kutoka Muleba:
Mkutano wa ndani wa CHADEMA umeanza..

View attachment 459861 View attachment 459860
umbea ni kitu kibaya sana yani umesema wamekamatwa kwa kuweka bendera kwenye gari yao lakini habari nzima inasema wamekamatwa kwa kusambaza bendera za chama bila ruhusa.
Acha uchakubimbi......
 
umbea ni kitu kibaya sana yani umesema wamekamatwa kwa kuweka bendera kwenye gari yao lakini habari nzima inasema wamekamatwa kwa kusambaza bendera za chama bila ruhusa.
Acha uchakubimbi......
Hata utapike ujiharishie utabaki kuwa mpiga deki wa lumumba mpaka uzae we
 
Hii habari ni kweli?!Ndio katazo la kufanya siasa?!

Wamevunja sheria gani?Watashitakiwa kwa kosa gani na kwa kutumia sheria ipi?

Hii hatari kuliko maelezo!
Huwa mnapenda tu kukurupuka bure.Mwenzako alikurupuka akasema viongozi wanahojiwa kwa kupeperusha bendera.
Kumbe wamehojiwa kwa kusambaza bendera,wameeleweka wameachiwa kazi kwenu povu limited
 
John Mnyika, Patrobasi Katambi, Conchester Rwamulaza na Tumaini Makene wako kituo cha polisi Geita wakihojiwa kwa kosa la kuweka Bendera za CHADEMA kwenye gari zao.

# Huu ni utawala wa kuwekwa kwenye kumbukumbu
======

Maelezo haya ya ziada ni kwa mujibu wa Tumaini Makene

MSAFARA WA MNYIKA ZIARA VIKAO VYA NDANI WAKAMATWA NA POLISI GEITA

Msafara wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, wakati unajiandaa kuondoka hotelini mjini Geita kwenda kwenye ziara ya vikao vya ndani, umekamatwa na Jeshi la Polisi na kuamriwa kwenda Kituo cha Polisi kuonana na OCD.

Kwa maelezo ya maaskari waliokuwa wamejaa gari nzima wakiwa na silaha za moto, wakiongozwa na OCCID, wamesema kuwa wamepewa maagizo ya kuwapeleka kituoni Mnyika na msafara wake kwa sababu eti wametumwa kuwakamata kwa sababu ni makosa kwa gari kupeperusha bendera ya kibunge katika jimbo la mbunge mwingine.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinazotoa maelekezo ya matumizi ya bendera za kibunge, Mbunge yeyote anaweza kupeperusha bendera mahali popote isipokuwa Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Kanuni ya 151 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Msafara wa Mnyika uliokamatwa na kupelekwa polisi ulikuwa una magari mawili yenye bendera hizo ambazo polisi wanasema ni kosa.

Mnyika aliambana na Mwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi, Ofisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene, Katibu wa Mkoa wa Kagera Conchesta Rwamlaza (MB), Mkiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita Neema Chozaile, Kamanda Anarose na makada wengine.
I say and will always do...This country is governed by a bunch of TWITS!
 
Huwa mnapenda tu kukurupuka bure.Mwenzako alikurupuka akasema viongozi wanahojiwa kwa kupeperusha bendera.
Kumbe wamehojiwa kwa kusambaza bendera,wameeleweka wameachiwa kazi kwenu povu limited
Kwa hiyo kusambaza bendera za chama chenye usajili ni kosa awamu hii?
 
Kwani wanachoogopa ni nini? Au hawakushinda kweli? Na babu alipokea ushauri kwa yule continental consultant? Jaynani vile?
 
Haya ni matokeo ya kuahirisha UKUTA,.....Laiti kama yale maandamano yangefanyika,.....Sizonje angeshika adabu.
Wapinzani wapuuzi tu nao ,kelele mingi hamna vitendo ,ukuta ungepata support kubwa sana na huyu mesiah alhadji subaana wataala angeshika adabu kweli
 
Back
Top Bottom