Gazeti la Jamhuri lapewa Siku 7 Kukanusha walichochapisha kuhusu familia ya Kikwete

Likifutwa mwanachama mwenzetu manyerere jackson anaweza kufa na njaa kabisa
 
Sio kitu kigeni duniani kwani tawala zote duniani ni katili na huwa hawapendi kuelezwa ukweli.Great thinker mwenye data anaweza kutuwekea hapa idadi ya waandishi wa habari ambao wameuawa kwa kusema ukweli na kufichua uovu.Jaribu kufikiria burundi hakuna chombo chochote cha binafsi kinachofanya kazi sasa hivi.Hivyo mwanahalisi na Jamhuri yakifutwa binafsi sitaona ajabu yoyote ile.Sio magazeti tu hata katika maisha ya kawaida WEMA HAWANA MAISHA!!.UKISEMA UKWELI UJUE UNAJITAFUTIA KIFO!!!!
 
Nape afanye kazi yake ya Uwaziri na asijiusishe na mambo binafsi ............ story ya umiliki wa UDA haihatarishi amani na utulivu nchini.

Ni jukumu la familia ya JK kujisafisha yenyewe au kulichukulia hatua za kisheria hilo gazeti. Kulifungia gazeti hakutaisafisha familia ya Kikwete.
 
kufungia ni kuthibisha ukweli wa taarifa iliyochapishwa , kama kweli wamechafuliwa kwanini wasiombe kusafishwa mahakamani ? mbona rage alihukumiwa kwa kuiba mipira FAT lakini mwishowe akaja kusafishwa mahakamani hadi akaukwaa ubunge wa tabora ? wasiogope waende tu mahakamani .
Tukizungumzia waandishi wa habari ni watu ambao sikuzote wanaongea uhalisia... Sababu wao hawafanyi tafiti ila wanaandika kilichopo....
 
Back
Top Bottom