Gazeti la HABARI LEO kwa upotofu huu mtaendelea kudharauliwa daima! Kwamba DPP alimuokoa Tundu Lisu?

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Mmeandika katika gazeti lenu la leo kwamba "Lissu amepata dhamana, DPP amuokoa". Kwanini msingesema na ugonjwa uliompata(automatistic) DPP mpaka akajikuta akimuokoa Tundu Lissu?!

Ni DPP wa nchi hii au wa kuazima kutoka nje?! Hata angekuwa wa kuazima asingethubutu kwa namna yoyote kuonesha nia ya kutaka haki ya dhamana itendeke.

Kaeni mkijua hili: kwamba baada ya DPP kuifuta kesi ya Tundu Lissu tunaoelewa tulijua mchezo upi unachezwa na DPP kwa kutumia madaraka ya kidikteta aliyonayo! Na hii ni kwa niaba ya CCM ili kufanikisha kimfumo kumzuia Tundu Lissu kwenda Arusha kushiriki mkutano na uchaguzi wa Tanganyika Law Society, TLS.

Walitarajia kwamba waifute kesi kisha wailete upya ikiwa ni kesi mpya na kwa hiyo ile dhamana aliyokuwa nayo itakuwa imeishia hapo na atatakiwa tena kuomba dhamana nyingine.

Kwa kuhofia kuwa wasingeweza kuzuia dhamana ya Lissu, Ndipo wakaja na style ya kutaka kesi iendelee. Ni bahati kuwa Mahakama iliwastukia, ikatoa dhamana na kuahirisha kesi. Hapo DPP kamuokoaje?! Acheni utoto!
 
Mawazo ya wendawazimu.
 
Hili ni moja ya magazeti ya udaku na vichekesho kama ilivyokuwa kwa magazeti ya sani, na magazeti ya Yule bwana aliyechapisha na kuuza kofia kwa elfu 50
 
Habari leo si ndo walewale na tbc! Hao tupa kule
Hivyo ni vyombo rasmi vya habari vya Serikali ya JMT. Kwa maana nyingine, habari zinazotangazwa au kuandikwa na vyombo viwili hivi ndio habari rasmi (official) za Serikali na zinazoelezea sera za Serikali. Kwa maana nyingine, hakuna mahali pengine au kwenye chombo kingine chochote duniani utakapoweza kupata habari rasmi na sahihi za Serikali ya JMT kuliko kwenye vyombo hivi.

Kwa kuhitimisha ni kwamba; kama kutatokea upotoshaji wa aina yoyote katika chombo chochote cha habari chini ya Jua kuhusu utendaji au sera za Serikali ya JMT, inategemewa upotoshaji huo utokee kwingine na sio TBC, HabariLeo au The Daily News. Badala yake, vyombo hivi vitatumika kama rejea ya usahihi dhidi ya opotoshaji huo. Upo hapo? Na sio "tupa kule".

Nisiingilie fani za watu; Pascal Mayalla hebu njoo huku fasta uweke mambo sawa.
 
Vombo ambavyo wafanyakazi wake wanafukuzwa kazi kwa kosa la kumsingizia sifa prezidaa unatuambia ndivyo viwe rejea ya usahihi?
 
Vombo ambavyo wafanyakazi wake wanafukuzwa kazi kwa kosa la kumsingizia sifa prezidaa unatuambia ndivyo viwe rejea ya usahihi?
Kiongozi, huoni kufukuza wafanyakazi walioingiza madudu ni hatua muhimu ku-maintain credibility ya hivyo vyombo? Makosa ya hapa na pale hayana budi kutokea la muhimu hatua stahiki zichulikiwe ili kutunza heshima na weledi.
 
Kiongozi, huoni kufukuza wafanyakazi walioingiza madudu ni hatua muhimu ku-maintain credibility ya hivyo vyombo? Makosa ya hapa na pale hayana budi kutokea la muhimu hatua stahiki zichulikiwe ili kutunza heshima na weledi.
Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini team yote ile iwe na mentality ya kufagilia uzushi?
Tutaaminije taarifa zao za juzi na za kesho iwapo wameonyesha kuwa na nia thabiti ta kumpamba mkuu hapa pasipostahili?
 
Kwa maslahi ya Taifa haifai ndugu wakawa kwenye nafasi hizo mbili!! DPP na AG wanaendeleza ukabila tuuu pale ni makosa makubwa! TISS mnashindwa kushauri hilo??
 


Kuna watu huwa wanapenda sana kudanganywa na matukio. Watu huwa hawapendi kusikia ukweli...
Kazi ya hivi vyombo ni kueleza ukweli hata kama huukubali, ingekuwa ni vyombo vya propaganda basi wate wanahabri 9 wa TBC wangepandishwa vyeo...
Habari leo na Dailynews ndo magazeti pekee ya rejea Tanzania, hilo mlijue. Hawaandiki habari ili wafurahishe jamii, wanaandika ukweli ili jamii ielimike...
 
Nadhani sumbuko linakuja pale mtu anapopandikiza chuki ilokubuhu dhidi ya serikali. Takribani kila chombo kilicho chini ya usimamizi wa utawala basi kitaonekana chenye shombo mbele ya pua zake. Mara ngapi tumeshuhudia hata magari ya serikali yakikosolewa hapa na pale, ili mradi tu kinaitwa cha serikali. Huu ni ugonjwa mkubwa ambao umemea kwenye mitima ya wengi kila kona ya dunia.

Sasa mtu anajishangaa kutosoma gazeti, kusikiliza ama kutazama media za serikali ati nalo liwe jambo geni. Unashangaaje watu kusimamishwa kwa makosa yao? Wangebakishwa kungekuwa na kauli gani? Huu ni undumilakuwili, ndimi mbili zinazotafunana na kusigana...ukweli ni kwamba vyombo vya serikali ndio wapeperusha bendera ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…