Gari aina ya Noah yenye namba za polisi (PT) inayotumiwa na trafiki kwa RPC Kilimanjaro ni kero

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
14,255
23,942
Gari hiyo inatumika kubeba matrafic kuzunguka barabara kuu ya kutoka moshi mjini hadi Hai inakusanya rushwa na TAKUKURU Kilimanjaro wana Najua na wana Piga kimya.

Kuna Askari mama mfupi mzee kazi yake ni kupiga magari touch na kufanya makubaliano ya kuomba fedha.

Mashine ya EFD wanayotembea nayo ina Miezi mine haijaingiza fedha Za fain Hata sent tano na RPC Amepiga kimya.

Ninashauri gari hiyo iondolewe barabarani ikafanye kazi Za umma ikiwepo kubeba wagonjwa kuliko kinachofanyika Kwa sasa ni wizi na uonevu mkubwa.

TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Jaribu ni kufanya zoezi la kuwastukiza Askari hao wakiwa kwenye hiyo Noah wakati liwe mtakutana na mamilioni ya fedha Za rushwa ndani ya hiyo gari.
 
Traffic cases zipo kila siku .....we utakuwa mtumiaji wa frequent kwa hicho kipisi....hai-himo kwahyo huwezi kuwakimbia kama umewakariri ivoo.....wewe la Muhimu kamilisha kila kitu ktk chombo chako,kama speed limit ni 50 nenda 45-50....vaa mkanda zingatia mistari....uone kama watakuwa na time na wewe ...
 
Unaishi kenya?
Msamehe bure, ndio wanachofurahia kwa sasa!

Ukisikia "anaupiga mwingi" ujue wanamaanisha "ulaji kwa urefu wa kamba" na hicho unacholalamikia ndo wamekiita "kujipimia" kwa kadiri ya maagizo, kule kulikosemwa kuvimbiwa ni kwa akina "Jan, Nap, Chaaand, Neee100, na genge lote"

Ukibahatika kuwa kwenye mifereji yao, huhitaji kuwa na ubongo.
 
Kwamba miezi mi 4 haijawahi kuandika faini ? Hata mdokoa mboga huwa hamalizi nyama zote mkuu
 
Namba ya takukuru ni 113 alafu nikuone tena na uzi wako hapa naomba msimamizi wa maudhui akupeleke likizo ya lazma maana utakuwa unalet nyuz za kimbea sasa
 
Traffic cases zipo kila siku .....we utakuwa mtumiaji wa frequent kwa hicho kipisi....hai-himo kwahyo huwezi kuwakimbia kama umewakariri ivoo.....wewe la Muhimu kamilisha kila kitu ktk chombo chako,kama speed limit ni 50 nenda 45-50....vaa mkanda zingatia mistari....uone kama watakuwa na time na wewe ...
Wanakosaga makosa hawa? Kuna siku kanipiga mkono akatafuta makosa weee akakosa, akasema leta fire extinguisher nikampa akaanza kucheki kama ime expire, akakuta bado siku tatu akakimaa eti ni kosa na inatakiwa ikibaki mwezi mmoja nikaifanyie services nikamgomea kata kata...
 
ukiweza kutembea kutoka Himo hadi Arusha hujaombwa chambi basi usibadilishe mganga.

kuna ile kona ya kuingia sadala kuna mlima alafu kila ukiupanda unakuta lori au kigari kinachotembea kama kobe, ukiovateki tu ujue mmasai amekutoka.
 
Wanakosaga makosa hawa? Kuna siku kanipiga mkono akatafuta makosa weee akakosa, akasema leta fire extinguisher nikampa akaanza kucheki kama ime expire, akakuta bado siku tatu akakimaa eti ni kosa na inatakiwa ikibaki mwezi mmoja nikaifanyie services nikamgomea kata kata...
sasa kama kosa halikosekani maama yake lipo.

shida ni ujeuri tu wakati wa mazungumzo,unakaguliwa unahisi anakusumbua wakati ni kazi yake hiyo kukukagua barabarani.
 
Kuna kipindi waliibandika namba private T...DRR watumiaji wa hio njia wanaijua sana hio noah nyeupe
 
Gari hiyo inatumika kubeba matrafic kuzunguka barabara kuu ya kutoka moshi mjini hadi Hai inakusanya rushwa na TAKUKURU Kilimanjaro wana Najua na wana Piga kimya.

Kuna Askari mama mfupi mzee kazi yake ni kupiga magari touch na kufanya makubaliano ya kuomba fedha.

Mashine ya EFD wanayotembea nayo ina Miezi mine haijaingiza fedha Za fain Hata sent tano na RPC Amepiga kimya.

Ninashauri gari hiyo iondolewe barabarani ikafanye kazi Za umma ikiwepo kubeba wagonjwa kuliko kinachofanyika Kwa sasa ni wizi na uonevu mkubwa.

TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Jaribu ni kufanya zoezi la kuwastukiza Askari hao wakiwa kwenye hiyo Noah wakati liwe mtakutana na mamilioni ya fedha Za rushwa ndani ya hiyo gari.
Hii ilifikia wapi?
 
Back
Top Bottom