TangataUnyakeWasu
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 1,268
- 1,587
Hongera Sana mkuu.Damu ya wanyama ina safari ndefu sana. Jaribio la kwanza lilifanyika mwaka 1667 na kusababisha maafa Na tangu hapo imekuwa ni ngoma.
Damu ya wanyama ina blood groups nyingi kama ilivyo ya binadamu na ina mambo mengi ambayo ni marefu kuyazungumzia.
Isipokuwa kumekuwa na utafiti wa KUTENGENEZA damu ya bandia SYNTHETIC na kuna MATUMAINI.
Damu inayokuzwa kimaabara kutokana na chembechebe cells za sehemu fulani mwilini ndo zilizo na tumaini la kuwa na damu hiyo kutumika kuokoa maisha ya watu wengi.
Ikizingatiwa kuwa HUENDA damu hii ikawa UNIVERSAL DONOR kind of.
Kiasi kuwa inaweza kutumika kwa mtu YEYOTE pasipo kuleta madhara ya mwili kukataa damu kama ilivyo sasa.
Sayansi itakuwa imepiga hatua kubwa sana. Hakutakuwa tena na SCREENING ya damu kabla haijapewa mtu ili kuangalia Magonjwa yakuambukiza kidamu kama HEPATITIS (.HBV HCV HDV...), HIV, ZIKA na magonjwa mengine yanayoweza kuambukizwa kupitia DAMU.
Katika utafiti wa awali kulikuwa na uwezekano damu hii kuanza kutumika mwaka huu 2017 ama mwishoni mwa mwaka. Wataalamu hawalali.
Jambo linalozingatiwa ni utengenezaji wa platelets na kisafirisha OXYGEN na mambo kwisha.
As per damu ya wanyama not that soon!
Binafsi nimekuelewa